CPA(T) v/s MASTERS

CPA(T) v/s MASTERS

Mkuu umeshauri vizuri sana. Cha kuongezea hapo kwenye data entry - kama anatamani kuingia kwenye proffessional advisory firms kama consulting au audit basi achangamkie apate CPA asap.
CPA ni nzuri sana kwa mhasibu, japokuwa siku hizi inakuwa under rated sana watu wanazo na bado maisha ya kuunga unga tu.. Zamani ilikuwa ukiipata umetoboa maisha but siku hizi elimu ni uwezo, network na surname unayotoka sio vyeti...

Nina watu nawajua wana cpa lakini hawaeleweki mwaka wa pili huu..

Ila kwa ushauri anza na CPA kama akili nzuri sababu bei yake ni rahisi kuliko masters.. Maana masters unaweza ingia gharama na bado isikusaidie mtaani kama hauna network ya kutosha...

Na pia siku hizi kazi zinafanywa na management systems tofauto tofauti unaishia kufanya data entry tu.. Ndo maana CPA sijui masters zinachukuliwa poa as hakuna kazi ngumu system inafanya karibu yote..

Finance manager peke yake labda na chief accountant ndo anaumiza kichwa but wengine wote data entry
 
Wewe ni employer au employee?
CPA(T) ni uchafu na ni kwa ajili ya tanzania tu ukienda beyond borders unaicha kwenye exit point sasa kwa nini upoteze muda kusoma huu ujinga kwenye utandawazi, masters nayo ni uchafu mwingine inakuwa na maana kama utaenda chuo kuwa tutor kwani masters kazini hakuna employer anaehitaji labda awe mjinga.
 
Kusoma sana sio kuwa na Pesa chamsingi unataka kuwa nani
 
Obama wa bongo or whatever u call ur self,pls watch ur mouth hatupo hapa kwa ajili ya matusi sawa,kwanza wewe mwenyewe ni bonge la mburura kwa kushadadia majina ya watu maarufu,ebu jiite lile jina ulilopewa na wazazi wako tulisikie lilivyo la ajabu,kama uwezi kucomment kaa kimya sio matusi,vijitabia vyenu vya facebook hatuvitaki humu ndani.........!ok,wadau tuendelee na mjadala wetu huyu sijui ndo obama anataka kutuvuruga humu
mkuu samahani kama ni metumia lugha kali,ila sijatukana mtu!
mimi nimetoa mawazo yangu as great thinker unaweza kuyakubali au kuyakataa,wala sipo hapa kuvuruga mawazo ya watu,mimi naamini tupo hapa kujenga zaidi sio kubomoa

mambo ya avatar au username yangu nafikiri is out of discussion,fanya lililo kuleta hapa jf
kind regards
obama the president
 
acha kukremu ...tena umemeza vibaya ...eti inauhusiano na tutors

Mwambie Bwana, huyu jamaa hana uhakika na anachosema halafu yuko kimbelembele kutoa comments. Nafikiri anaziota CPA na masters kwenye ndoto zake.

Tiba
 
Kusoma sana sio kuwa na Pesa chamsingi unataka kuwa nani

Acha zako hizo.Mwenzako kaomba ushauri wewe unaongea kitu tofauti kabisa.Kwa ujumla CPA ni bora kuliko MASTERS kwa sababu elimu ya undergraduate mara nyingi inatosha kufanyia kazi za kihasibu.Unahitaji CPA ili uweze kuhudhuria semina mbalimbali zinazoandaliwa na NBAA pamoja na kujiunga na chama cha Wahasibu(TAA) na kuweza kupata access nzuri ya current issues za accounts.
 
hi, members Masters za kibongo ni uzushi tu tunawaona makazini weupe kinoma CPA kwa kweli bado wamemaintain stustas yao mtu mwenye CPA tofauti kabisa na mwenye masters
 
Anayesma CPA (T) ni Uchafu huyo imemshinda na Tunashaka na uzalendo wake kabisa Hata Multnational zilizopo Tanzania wakitangaza nafasi za Finance wanataja ACCA,CIA na CPA(T) leo hii anatuambia nini kama umekosa cha kuongea bora ujinyamazie kuliko kulopoka kwenye mtandao mwezako anaomba ushauri wewe unapotosha huo ni ujinga na uendawazimu tunataka tujenge Tanzania ya wasomi wewe unaturudisha nyuma acha polojo za mtaani bhana tulioko kwenye system tunajua umhimu wa CPA acha hizo bhana kama imekushinda si useme?
 
anza na mastaz coz ni rahisi kuipata kuliko cpa pia mastaz kimtaa inasifika hata ukifa kaburini wakiwa wanasoma historia fupi ya marehemu utauza mbaya japokuwa utakuwa tayari kuliko CPA ambayo mtaani hata hawaijui wanaweza fikilia ni jina lingine la unesi au mtu wa monchwari.

hahahahahahahahahahahahaha...............hahaahahahahaha..................hahahahahaaa........, khaah jamani, hahahaha (the very big lol)
 
hi, members Masters za kibongo ni uzushi tu tunawaona makazini weupe kinoma CPA kwa kweli bado wamemaintain stustas yao mtu mwenye CPA tofauti kabisa na mwenye masters

Inategemea mkuu, kuna watu wana Masters ni wazuri tu, na wengine na CPA lakini ni weupe tu, and vice versa!. Tunao wengi ofisini wa namna hii!
 
hi, members Masters za kibongo ni uzushi tu tunawaona makazini weupe kinoma CPA kwa kweli bado wamemaintain stustas yao mtu mwenye CPA tofauti kabisa na mwenye masters

Mkuu hii inategemea bana,coz hata wenye cpa wapo weupe 2 kichwani!.....kwani unafikiri masters ni nn?
 
CPA ni hitaji la kisheria la uhasibu na wala sio maarifa/ skills alizonazo mtu. Kuipata kwake ni kweli ni kwa kubahatisha. Kwa kuwa NBAA wanatoa maswali ya mitumba kutoka ACCA CMA etc, kufaulu kwake ni kwa kubahatisha pia kama umewahi kuliona swali la aina hiyo mahali na una uwezo wa kugandamizia (kukariri swali na majibu) vinginevyo nishida kufaulu mtihani wake. Waalimu wanaokutungia mtihani sio wanaokufundisha (kama inavyotakiwa katika elimu), hivyo hawajui kitu gani kimefundishwa, wao .pia wanabahatisha tu.Mwalimu akibahatisha 1/2 mwanafunzi atabahatisha 1/4
Master is an international academic qualification. Inatambulika duniani kote. CPA (T) inatambulika Tanzania tu. Hutapanda cheo kuwa Accountant officer ii mpaka uwe na CPA. Bachelor Degree ya uhasibu inakupa cheo cha Accountnt ii-i, basi zaidi ya hapo uwe na CPA. Kinachoipa nguvu CPA ni sheria sio ujuzi na maarifa anayokuwa nayo mwenye CPA. Matangazo ya kazi yanaweka CPA kama mojawapo ya sifa muhimu ili uajiriwe katika nafasi nyingi za uhasibu.
Hitimisho langu ni kuwa ukitaka kutambulika kama mhasibu na uweze kupandishwa cheo (Tanzania) katika fani ya uhasibu sharti uwe na CPA hata kama huna kitu kichwani. CPA haitoi wahasibu wazuri,inatoa good claimers. Ukitaka maarifa na ujuzi wa kazi Master,s inafaa, lakini hutapanda cheo chochote katika fani ya uhasibu. Uamuzi ni wako, kusuka au kunyoa
CPA ni nzuri sana kwa mhasibu, japokuwa siku hizi inakuwa under rated sana watu wanazo na bado maisha ya kuunga unga tu.. Zamani ilikuwa ukiipata umetoboa maisha but siku hizi elimu ni uwezo, network na surname unayotoka sio vyeti...

Nina watu nawajua wana cpa lakini hawaeleweki mwaka wa pili huu..

Ila kwa ushauri anza na CPA kama akili nzuri sababu bei yake ni rahisi kuliko masters.. Maana masters unaweza ingia gharama na bado isikusaidie mtaani kama hauna network ya kutosha...

Na pia siku hizi kazi zinafanywa na management systems tofauto tofauti unaishia kufanya data entry tu.. Ndo maana CPA sijui masters zinachukuliwa poa as hakuna kazi ngumu system inafanya karibu yote..

Finance manager peke yake labda na chief accountant ndo anaumiza kichwa but wengine wote data entry
 
Tumewasikia Ngwini. Hiyo masters inategemea ni ya nn. Na hiyo CPA mmmh mwajuwa wenyewe jinsi ya kuipata.
 
Back
Top Bottom