CRDB bank inafilisika?

CRDB bank inafilisika?

Wewe peleka feedback CRDB...wateja tuna kero...badala ya kuwa busy kutujibu...
Ndio tatizo ya ngozi nyeusi...badala ya kusema kero yenu tunashughulikia unatafuta ku justify kila kitu...

Huo umuhimu wameuona baada ya TIGO na VODa kukamata fursa?

Huko Brazil unakozungumzia kuna TIGO na M Pesa? Unajua kuwa hizi sijui M Pesa haziko latin America??????
Sisi tumeshafikiwa na huduma za kutuma na kupokea pesa kwa simu...wao waboreshe huduma za kibenki badala ya kuwa ambitious kufikia kila mtu...na kuishia kuwapoteza hata walio nao mkononi...
Unaweza kujenga hoja bila kuwa stereotype!
 
Kuna u 'sawa' gani? Hueleweki....

Unajua maana ya stereotypes ...

Kwa heri nsijekuwa si saizi yako...nikaku....
acha semantics...ni sawa na mimi kusema wanawake wote ni malaya wakati si mjui mama yako!
 
Kuna u 'sawa' gani? Hueleweki....

Unajua maana ya stereotypes ...

Kwa heri nsijekuwa si saizi yako...nikaku....

Usitoke nje ya hoja shangazi. Unaongea pumba ukiambiwa ukweli unakimbia. Hoja ya kuwa ngozi nyeusi ina matatizo ua mapungufu haina mashiko. Watu wadizaini zako hawana nafasi tena dunia hii.
 
tajiri alienunua shea 80% ameandika notes ya kutoa shea yake

Je unamjua jina???? Katika taarifa za CRDB kampuni mbili ndizo zina hisa zaidi ya 10%.
DANIDA Investment Fund yenye hisa 467,781,934 sawa na 21.5%, na PPF Pension Fund yenye hisa 217,401,749 sawa na 10%.
Kweli miezi kadhaa ya nyuma, kadiri ya ripoti, faida ya kabla na baada ya kodi ilishuka ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Huku, amana na fedha za wanahisa zikiongozeka. Faida ilishuka kutokana na kusitisha mikopo. Mikopo ilisitishwa ili wakusanye madeni waliokuwa wanadai, pia ule mgogoro baina ya NMB na CRDB.
Si rahisi kupunguza gharama ndani ya muda mfupi bila ya kuleta madhara makubwa kwa kampuni.
Muda si mrefu benki ilianza kutoa mikopo. Ifahamike CRDB ni mshindani mkubwa katika kutoa mikopo hapa nchini.
Ningekuona mjanja kama ungekuja na takwimu. Hizo ni hisia zako ndugu. Hisia na viashiria dhaifu sanaaa... Katika uwekezaji, watu kama akina Mshiiri wanaitwa CYNICS, na tabia yao inaitwa CYNICISM.
 
Unanichekesha ujue...

Kati yangu mimi na wewe na wenzio anayekimbia hoja ni nani...??????

Ni nyie ambao nimeandika paragraph nzima mmekimbilia nusu sentence na kuanza kuijadili badala ya kujadili substance...

Ha ha ha

Ukisikia mtu anaelezea hoja zake akitumia F-word ....utachukua lipi? hoja ua F-word na kukazana kuwa ametukana????

Kwa hiyo huo ushauri unawahusu nyie...rudini kwenye mada...ngozi nyeusi ina laana ina laana hutaki kajichubue...

Usitoke nje ya hoja shangazi. Unaongea pumba ukiambiwa ukweli unakimbia. Hoja ya kuwa ngozi nyeusi ina matatizo ua mapungufu haina mashiko. Watu wadizaini zako hawana nafasi tena dunia hii.
 
Lengo la Benki ya Ulaya kuikopesha Benki ya CRDB ni kwa ajili wa wajasiliamari na sio kuwa benki haina uwezo wa kuwakopesha. Hili ni jambo la kawaida kabisa kwani hata African Devt Bank hupokesha benki nyingi hapa nchini ili nazo zitoe mikopo kwa wateja. Acha kukurupuka!
Hiyo NBC yako unayoishabikia ndio mabingwa wa kupika, jiulize katika kipindi cha miaka kumi iliyopita benki yako imeshabadili na kufukuza Ma CEo wangapi? If all is well as you potray?.Tufanye kazi jamani tuache siasa kwenye mambo ya msingi.

pia, je imetoa gawio kiasi gani kwa wanahisa??
NBC ni benki yenye migogori mikubwa isiyokwisha.
 
Mabenki mengi kama sio yote Tz ni majanga matupu. Tukikutanika wateja watatu au wanne tukaandika kero, kadhia na adha tunazokutana nazo nadhani tunaweza tukaandika volumes kama sio series za best-selling novels na tukauza mbaya! Mnaoshabikia na kushadadia huduma za hizi benki pengine hamjawahi kuona benki bora zinafanyaje kazi; mngejua mngekua wapole na kujisikitikia mlichoandika.
 
Mabenki mengi kama sio yote Tz ni majanga matupu. Tukikutanika wateja watatu au wanne tukaandika kero, kadhia na adha tunazokutana nazo nadhani tunaweza tukaandika volumes kama sio series za best-selling novels na tukauza mbaya! Mnaoshabikia na kushadadia huduma za hizi benki pengine hamjawahi kuona benki bora zinafanyaje kazi; mngejua mngekua wapole na kujisikitikia mlichoandika.

Nadhani hapa wanachofanya ni kuangalia the lesser of two evils.

Na unachosema ni sahihi kabisa kwamba mabenki mengi bongo kama si yote ni majanga tu.

Na si mabenki tu. Karibu kila huduma ni majanga matupu. Iwe hospitali, magengeni, madukani, taasisi za serikali, you name it....

Kwenye mahakama huko ndo pasikie tu. Usiombe upatwe na jambo la kukupeleka mahakamani maana hata kama ni jambo linahusu haki yako waweza hata kukata tamaa na kulipotezea mazima.

Umeme nao shida tupu. Maji nayo ndo mulemule tu. Usafiri nao ndo yaleyale tu.

Kuna sekta yenye nafuu bongo? Labda ngono...ingawa huko nako migonjwa inakusubiri.
 
Nilishangaa nilitumia kadi ya ATM ya CRDB nikiwa Dubai, Lyon-France kutumia katika kulipa huduma za usafiri na nikiwa Montpellier. CRDB iko juu.

crdb is de best labda tawi la kijijini kwao ndo linazingua
 
Nilishangaa nilitumia kadi ya ATM ya CRDB nikiwa Dubai, Lyon-France kutumia katika kulipa huduma za usafiri na nikiwa Montpellier. CRDB iko juu.

Hata kadi za NBC zenye nembo ya MasterCard na VISA zinafanya kazi sehemu nyingi tu duniani.
 
"ndio tatizo la ngozi nyeusi"??? Statement hiyo tu inaonyesha ulivyo na upeo mdogo na mtindio wa akili. Mama yako mzungu?

wewe jamaa unadharau,,,,kwaiyo ngozi nyeusi ina ingiaje sasa hapa,,,washkaji wengi wanatoa maelezo kwa point ila wewe umeepanic had unaonesha mapungufu yako,,,,,punguza jazba kaka,,,,kwani we mwenzetu mzungu nn
 
wewe jamaa unadharau,,,,kwaiyo ngozi nyeusi ina ingiaje sasa hapa,,,washkaji wengi wanatoa maelezo kwa point ila wewe umeepanic had unaonesha mapungufu yako,,,,,punguza jazba kaka,,,,kwani we mwenzetu mzungu nn

Umechanganya madesa arifu.

Jamaa hakuleta mambo ya rangi ya ngozi.

Aliyeyaleta mwingine kabisa.
 
wewe jamaa unadharau,,,,kwaiyo ngozi nyeusi ina ingiaje sasa hapa,,,washkaji wengi wanatoa maelezo kwa point ila wewe umeepanic had unaonesha mapungufu yako,,,,,punguza jazba kaka,,,,kwani we mwenzetu mzungu nn

Soma vizuri kaka. Mimi wala sikuja na hayo mambo.
 
Ahsante sana ndugu yangu kwa kusema yale uliyoayona kuwa mazuri ktk ya niliyoandika.

Kiongozi kuwa mwanasiasa na mchumi inaweza kuwa taabu na imekuwa taabu kwa nchi za ulimwengu wa 3. Tatizo linakuja ni kwamba elimu zetu hazitujengi kuwa wabunifu na watu wenye uwezo wa kutoa mmamuzi huru. Si ajabu kusikia viongozi waliosoma uchumi na kufaulu kwa alama za juu ila wakawa wana uelewa tofauti kuhusu soko huria. Tofauti hizi sio kwa kuwa wote wapo sahihi na wana mawazo mapya na tofauti,Lah hasha, wote wamepotoka.

Mfano mzuri ni wafanyakazi ktk wizara pamoja na serikali kulipa hela nyingi kuwapiga msasa kuhusu matumizi ya computer kwakutumia package rahisi km microsoft windows office, zaidi ya nusu yao hawajui chochote cha msingi ingawaje wanajua kutaja misamiati sijui niite maalum (terminologies) ktk mazungumzo.

Sasa hii inaendelea hadi kwa hao wasomi wa uchumi na blah blah nyingine, ni wajuzi wa kutumia hizo terminologies hasa zile ambazo ndizo zipo ktk matumizi ya leo duniani ila ukipitia vichwani mwao na kuona ni picture ipi wanayo kichwani utacheka au kuishiwa nguvu kabisa. Sasa huu upotoshaji unajiongeza hadi kwa raia. Ila matokeo yake utayaona ktk mikataba iliyoandikwa km ile ya enzi za wazee wetu na wakoloni.

Kitu muhimu ni kuhimiza elimu sahihi kuhusu siasa na mambo yahusuyo raia,uchumi na soko huria. Kuwe na baraza la kuhakiki public understanding. Serikali ijaribu kutumia parameters za uchumi na sheria halali za kulinda soko huria na democrasia. Kuzipanga hizi paremeters ndiko kutakuwa kunatuweka ktk optimum setting au equilibrium. Kama sisi hii itatushinda basi social activities ziajirekebisha zenyewe kwa hasara yetu hadi tupate kuelewa na kuanza upya.

Mchumi bora hatoshindwa define democrasia ktk mtazamo wa soko huria. Mimi kwangu tofauti si kubwa sana kwani ni kubadili parameters tuu ila skeleton ni sawa.

Ok, nimekuelewa kwa mfano wako japo sijaafiki kutumia hapa kwani masuala ya dini yana complication sana. Well, kuhusu reference (sijui niite dira), hatuna hapa Tanzania labda tuandae au tufuate za nchi kama Marekani kwa kugushi. Naamanisha kama masai wanavyovaa tairi km kiatu kwani tumetofautiana na wale jamaa sana.

Kuhusu wananchi, ni kwamba uelewa wa raia wengi na muhimu ni mdogo.Wengine wana uelewa potofu. Mfano ni kama kijijini kwetu wazee wengi bado hawajaweza ona umuhimu wa kukabidhiana mali kwa maandishi hata pale mazingira yanaporuhusu. Ni km pale raia wasivyoona haja ya kutupa uchafu sehemu sahihi ktk miji yetu.

Ni pale raia wanapoona hakuna nhaja ya bima, kuweka hela bank. Bado wananchi hawajawa tayari kukubali kuwa utandawazi, demokrasia na soko huria etc vipo nasi hapa na kinachohitajika si kukataa ila ni kutafuta njia za kuishi ktk hizi hali kwa faida yetu. Na hizi njia zipo ktk maandishi etc na wenzetu wanazitumia na kufanikiwa.Huwezi amini wageni wanakuja hapa wanatengeza utajiri kwa kipindi cha chini ya miaka 5, na kuondoka kabla grace period haijaisha.

Wengine wameweza tengeneza hela ya kula maisha yao yote bila kuimaliza.Wamechukua hela ya kutosha kununua hisa na products nyingine za kifedha ambazo zitaingiza hela zaidi ktk maisha yao yote.

Kikubwa cha kuanza ni kushusha gharama za kuanzisha makampuni ya kizalendo ili hata vijana kutoka vyuoni wenye taalunma inayoweza kuwa mtaji waweze hilo. Sasa kazi ibaki kwao kuimarisha nafasi yao ktk soko huria. Wakishindwa basi wanaanguka. Hii inahimiza ufanisi na elimu sahihi kwa jamii.kwani hata mtumiaji naye atajikuta akipata elimu sahihi ili aweze pata huduma sahihi.

Raia wenye uelewa mkubwa wanawapa wanasiasa wakati mgumu wa kubabaisha. Kwa hiyo vyma vitaumiza vichwa kujijenga na kujiremba kuliko kupoteza muda wa kuhubiri chuki na kugombania ruzuku. Hapa vyama vitakuwa na nguvu vyote na hivyo kuleta upinzani km ktk ligi ya mpira. Timu iliyo bora ndio itakayokuwa na nafasi ya kushinda. Ila kila chama kitajiuza kwa ubora na si nguvu ya hela na dola.

Pole kama ulipata huduma isiyoridhisha kwenye tawi lako. Acha lumumba nenda hata Iringa au Mbeya, Mlimani city wateja walo level seat. Unapendekeza benki gani mbadala?
 
Tako we CRDB wana huduma nzuri nenda NMB Mbeya kudadeki hamna ata pa kupangia foreni, huduma zao ni kelo, Benki ka sacoss maafaka
 
Back
Top Bottom