Cristiano Ronaldo aondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ureno

Cristiano Ronaldo aondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ureno

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
1791012534915.png

Cristiano Ronaldo amesema amefanya uamuzi wa kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ureno baada ya mkutano na waandishi wa habari wa kocha wa timu hiyo na mazungumzo ya moja kwa moja na Rais wa Shirikisho la Soka la Ureno.

Ronaldo amesema:

“Baada ya mkutano wa waandishi wa habari wa kocha wa Ureno, na kufuatia mazungumzo ya moja kwa moja na Rais wa Shirikisho la Soka la Ureno, nimeamua kuondoka kwenye kambi ya timu.”
Ameongeza:

“Kwa wakati muafaka, nitawaeleza watu wote wa Ureno ukweli kuhusu sababu zilizonifanya kuondoka kwenye timu ya taifa, ambayo nimejitolea kwa ajili yake tangu siku yangu ya kwanza.”
Ronaldo pia amewatakia kila la heri Ureno pamoja na wachezaji wenzake wote, bila kumtenga yeyote.

🚨 𝐌𝐀𝐉𝐎𝐑 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆- 𝐂𝐑𝐈𝐒𝐓𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐑𝐎𝐍𝐀𝐋𝐃𝐎 𝐇𝐀𝐒 𝐋𝐄𝐅𝐓 𝐏𝐎𝐑𝐓𝐔𝐆𝐀(1).jpg
 
Attachments

  • 🚨 𝐌𝐀𝐉𝐎𝐑 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆- 𝐂𝐑𝐈𝐒𝐓𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐑𝐎𝐍𝐀𝐋𝐃𝐎 𝐇𝐀𝐒 𝐋𝐄𝐅𝐓 𝐏𝐎𝐑𝐓𝐔𝐆𝐀.jpg
    🚨 𝐌𝐀𝐉𝐎𝐑 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆- 𝐂𝐑𝐈𝐒𝐓𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐑𝐎𝐍𝐀𝐋𝐃𝐎 𝐇𝐀𝐒 𝐋𝐄𝐅𝐓 𝐏𝐎𝐑𝐓𝐔𝐆𝐀.jpg
    194.1 KB · Views: 86
Mkitaka kugundua effect ya Ronaldo tazameni mechi zijazo baada ya jamaa kuondoka kambini.

Kwanza tiketi zitauzwa kwa bei ya hasara na katika hao wachache wataoingia kutakuwa na mabango mengi ya kulaani hii dhihaka ambayo Portugal wanamletea CR7.

Ngoja nisubirie Ronaldo aseme yale waliyoongea pamoja na raisi wa shirikisho la Ureno.
 
Portugal, before CR7:

❌ Played in 3/17 World Cups
❌ Played in 3/11 European Championships
❌ 0 titles

Portugal, with Cristiano Ronaldo:

✅ Played in 6/6 World Cups
✅ Played in 6/6 European Championships
✅ European Championship winner 🏆
✅ Nations League winner 🏆
✅ Nations League winner 🏆

Portugal didn't exist before CR7.
 
Mkitaka kugundua effect ya Ronaldo tazameni mechi zijazo baada ya jamaa kuondoka kambini.

Kwanza tiketi zitauzwa kwa bei ya hasara na katika hao wachache wataoingia kutakuwa na mabango mengi ya kulaani hii dhihaka ambayo Portugal wanamletea CR7.

Ngoja nisubirie Ronaldo aseme yale waliyoongea pamoja na raisi wa shirikisho la Ureno.
Kucheza mmejaza mashabiki uwanjani huku timu haishindi mechi zake faida ni Nini? Ronaldo alitakiwa astaafu baada ya kombe la dunia kama alivyofanya Messi na Neymar sasa hivi amekuwa kituko uwanjani akili unataka ila mwili hautaki, dalili zote zilianza kuonekana wakat wa kombe la dunia ni vile kocha Martinez alikuwa anamuogopa ila Jorge Jesus anamjua vizur Ronaldo maana wamekuwawote pale Al Nasr hajataka kupepesa maneno.

Wakati Messi anaagwa Kwa heshima Ronaldo anaondoka kwenye Kambi ya timu ya taifa Kwa hasira baada ya kuwekwa benchi, ni aibu
 
Angetusikiliza wala yasingemkuta mambo ya aibu kama haya.

Tatizo analazimisha ugoti kwa kutaka kufikisha magoli 1000 matokeo yake anataka kucheza wakati nguvu zimeshaisha uwanjani anageuka kituko na mzigo kwa timu.

Mwambieni atulie akileta ubishi ataishia kupata aibu kama hivi.
 
kwa heshima mwamba inabidi astaafu tu timu ya taifa ,mchango wake uwanjani unaendelea kupungua siku baada ya siku.. games nyingi za timu za taifa zimekuwa za ushindani mkubwa sana na yeye uwezo wake na kasi vimepungua.

na pia nothing lasts forever ,true maturity is knowing when your role is complete and leaving with dignity.
 
Jamaa anatamaa kama ya fisi yaani. Si alisema baada ya kombe la Dunia anastaafu kuichezea timu ya Taifa.

Ona mwenzake Messi anastaafu na anaagwa kwa hishima, huku yeye anatoroka kambini 😁

Sijawahi kumuona mtu mzima hivyo kama Ronaldo maishani mwangu.
 
Kucheza mmejaza mashabiki uwanjani huku timu haishindi mechi zake faida ni Nini? Ronaldo alitakiwa astaafu baada ya kombe la dunia kama alivyofanya Messi na Neymar sasa hivi amekuwa kituko uwanjani akili unataka ila mwili hautaki, dalili zote zilianza kuonekana wakat wa kombe la dunia ni vile kocha Martinez alikuwa anamuogopa ila Jorge Jesus anamjua vizur Ronaldo maana wamekuwawote pale Al Nasr hajataka kupepesa maneno.

Wakati Messi anaagwa Kwa heshima Ronaldo anaondoka kwenye Kambi ya timu ya taifa Kwa hasira baada ya kuwekwa benchi, ni aibu

Hili jambo ni gumu sana kujadili bila kuweka notion ya wishful thinking.

So, kwasababu Messi na Neymar wamestaafu timu zao za Taifa basi kwasababu hizo hizo unataka kuona na Ronaldo akistaafu?

Kama kustaafu kuna thibitisha mwisho wa kiwango cha mchezaji, mbona Messi hajastaafu kucheza ligi ya vilabu?

Mbona Okwi ambaye ana umri mdogo kwa Messi amestaafu kucheza mpira kiujumla kwanini Messi ana ng'ang'ania kucheza MLS?

Kingine ambacho hamuwezi kukiongea ni Ronaldo aliwahi kufikiria kustaafu timu ya Taifa na tayari rumors zilianza kusambaa.

Lakini Raisi wa Portugal alimuomba Ronaldo asifanye hayo maamuzi ya kustaafu.

Na hata yeye alipoulizwa kwenye interview alijibu kuwa "If they no longer want to depend on me, I can leave today, I have no problem with that"

Kwa hiyo walimuita kwasababu waliona ana mchango bado kwenye timu yake ya Taifa.

Hivyo disrespect yeyote ya Kocha ku-undermine uwezo wake pamoja na kumfanyisha warm up ya dakika 45 (ambayo kocha ame admit kuwa alifanya kosa) inamfanya awe sahihi kuchukua maamuzi ya kusepa.
 
Angetusikiliza wala yasingemkuta mambo ya aibu kama haya.

Tatizo analazimisha ugoti kwa kutaka kufikisha magoli 1000 matokeo yake anataka kucheza wakati nguvu zimeshaisha uwanjani anageuka kituko na mzigo kwa timu.

Mwambieni atulie akileta ubishi ataishia kupata aibu kama hivi.
Messi analindwa na media ndio maana ups and downs zake hazijadiliwi kwa ukubwa.

Mfano we angalia tu, katika mechi 10 alizocheza Inter Miami ni mechi moja tu ndio kashinda.

Hakuna EPSN, GOAL, BR, 433 wala Fabrizio aliyeripoti hiyo taarifa.

Ni kwasababu Messi ni product ya media.

Nakupa na hii
Screenshot_20260827-115458.png

Lakini kwa Messi habari ni tofauti
Screenshot_20260827-115604.png

Kwa hiyo Mkuu hiki anachopitia Ronaldo saizi ni kitu kidogo sana wala hakiwezi kumyumbisha kabisa.

Umesahau hadi BBC waliwahi kuandika hivi baada ya Ronaldo kukosa penalti?

1790846821785.png
 
Back
Top Bottom