The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Labda mkuu hujalielewa kile kinachomaanisha clone
Clone ni kiumbe pacha kwa subject yeyote ile _ni kwamba kama umekufa wanaweza kuchukua cell yako na kuikuza na kupatikana kiumbe anayefanana na wewe kimuonekano kwa [emoji817]%
Ila tofauti yake ni kwamba hatokuwa na kumbukumbu zako za awali_ sasa katika hilo ndipo likatokezwa wazo la chip implant tech ambayo mkuu coded anatutaarifu inavyohisiwa kufanya kazi kwa kusaidia huyo clone kuwa Kama wewe wa awali
Sawa mkuu
Huko nimeshaelewa. Ukifa ukahifadhiwa kwenye mazingira rafiki, ukiwekewa chip iliyokua kwa mtu mwingine, utaishi? Tuweke suala la kuwa na replica kando, tujikite kwenye uhai kwanza.
Na endapo clone ya binadam aliyewekewa chip inawezekana, kwanini nikifa kama nilikua na chip wasishughulikie mwili wangu usiharibike kisha wakatumia hiyo chip yangu kunirejeshea maisha?
Na hapo ndio nikauliza endapo nna chip tayari tokea niko tumboni, kwanini nife?
Karibu