Kumbe wewe ni mgumu kuelewa eeh?
lifecoded anasema ufahamu wako ndio uhalisia wako, ndio wewe na ndio uhai wako (yaani unavyojihisi hai hiyo ni kutokana na ufahamu wako)
Hiyo chip itakayowekwa itakuwa inakopi taarifa mbalimbali kama zilivyo kutoka kwenye ufahamu wako wa Sasa na kuzihifadhi. Happy kazi ya chip itakuwa ni kuhifadhi hizo taarifa tu.
Siku ukifa utatengenezwa mwili mwingine ambazo unafanana na wako kwa kila kitu kisha ile chip itawekwa pale na ikiunganishwa fresh basi ufahamu wako kutoka kwenye mwili wako wa awali utahamia kwenye huu mwili mpya. Kwa kuwa uhalisia wako wote na huo uwewe unatokana na ufahamu wako Basi hapo utajiona ni wewe tu yule yule na wala hutojua kuwa upo kwenye mwili maingine maana utajihisi tu kuwa umeamka kutoka usingizini.
Hapo nimejaribu kufafanua maelezo ya
lifecoded na Kama nimekosea atanikosoa. Ila kutokana na maelezo haya mimi ninamkanganyiko kidogo,
Huu mwili mpya na ufahamu wake vyote ni copy. Mtu halisi anakuwa amekufa na ufahamu wake ule halisi, kwa hiyo atakuwa huko kwa wafu (Kama kweli kupo)
Ikitokea labda kafufuka, au labda hakuwa amekufa sawa sawa so karejea kuwa hai atakuwa na ufahamu ule wa zamani kabla hajafa ila muendelezo wa ufahamu wake utakuwa tofauti na muendelezo wa ufahamu wa yule ambaye ni copy, Sasa hapa ndo feki atakapofeli maana huyu real atakuwa real so muendelezo wake utakuwa real halafu yule copy muendelezo wake utakuwa feki feki tu.
Nipo sahihi
lifecoded?