Crypto na ahadi ambayo haijatimia

Crypto na ahadi ambayo haijatimia

Yule jamaa wa Quadriga ali fake kifo chake India, alikua anachukua pesa then na yeye anenda ku trade sehemu nyingine.

Bado namfatilia Sam bankman fried, mzee wa ftx.
Huyu si Kuna taarifa hela zake Bahamas government wamezi cease ama Mana ndiko alikozotoreshea
 
Huyu si Kuna taarifa hela zake Bahamas government wamezi cease ama Mana ndiko alikozotoreshea
Alianzisha kampuni (Alameda Research) ambayo Makao yake makuu yalikuwa Hong Kong. Kwanini Hong Kong? Kwasababu masharti ya kufungua kampuni aina ya Alameda Research ni mepesi zaidi Hong Kong ukilinganisha na Marekani. Hiyo ilikuwa ni 2019. Akaanzisha kampuni nyingine ambayo ndio hiyo FTX. Ile Alameda akamuachia demu wake aisimamie, nyuma ya pazia walikuwa wanafanya uhuni - wanachukua pesa za wateja wa FTX wanazipeleka Alameda. Na ndio chanzo kikuu cha anguko la FTX.

Aliamua kuhamishia shughuli zake Bahamas kwasababu; Kwanza ni jirani na Marekani, na pili masharti yake ni mepesi pia ukilinganisha na Marekani. Na kwasababu Bahamas ni jirani na Marekani, ilikuwa rahisi kwake kusafiri kwenda Marekani mara kwa mara kwa lengo moja kubwa; Kuwashawishi viongozi wa Marekani ili wamlegezee masharti ya kufungua ofisi za FTX na kuzihalalisha shughuli za FTX ndani ya ardhi ya Marekani.

Ukifuatilia utaona alimwaga pesa nyingi sana kwa wanasiasa wa Marekani. Nadhani ni mmoja wa wachangiaji wakubwa wakati wa uchaguzi kwa upande wa Joe Biden. Na kuna party moja aliifanya walijaa wanasiasa maarufu tupu. Bahamas alikuwa na mjengo wa kifahari, na ndiko alikokamatiwa baada ya kampuni yake kufilisika.
 
Mkuu umeichimba hii kitu kwa kweli nimekuvulia kofia.

Mie nimejikita katika contract for tomorrow price.

Mana hizo Mambo zenu investors na ku own some shares and real coins kwangu niliona isn't a big deal. I wanna make money whether on both rising and falling price an given financial instrument Ila najua hatuachani Ila usafiri tofauti.

Yes Bahamas and Cyprus and shelisheli na nchi nyingine kibao huwa hawana vigezo vikali vya kuwabana brokers ili raia wawe salama wasio na financial literacy.

Asic , FSA wamepiga ban mfano leverage maximum ni 1:33 mie hata 1:5/1-10 ndio nazopenda.
Sema Sasa wapo wanaopenda leverage mpaka ya 1:3000 wanapata mfano justforex sijui instaforex ili atimize kiu zao.

USA ilijaribu hata ku ban hizi mambo za cfd Mana none real assets owning so inaonekana Kama Ni kamali. Mana nasema mchele mwaka huu utashuka Bei so najaribu kuanza mchele kwa Bei iliyopo.
Am happy to find like minded niga.

You feel so much happy, we're traveling in bad road and lonely journey na ndio Mana watu wanaanza kufundishana smt ili uwe na your peers .

Uzi wako nimeupitia umechimba na uko aware ambavyo influencers wanaweza nunulika wakainfluence wakazama mazima like Elon musk Ali promote mno dogecoin na Ontario kweli Twitter akawa anafurahi anawavuta saivi sijui anasemaje.

Mie nimeamua ku spealize only in one field na Nina one or two pairs nazo trade I don't bother to look or distribution my fαckin expensive energy to many fαckinn bushηit
 
Kwenda hizo clubs za mpira wa kikapu nimekupata mno. Wahuni wanatumia kila mbinu ili kuvuta masses na ndio navyo trade I don't look or listen so called experts and programmed news to bend our vision.
I don't wanna anybody sway my ideas
 
Mkuu umeichimba hii kitu kwa kweli nimekuvulia kofia.
Mie nimejikita katika contract for tomorrow price.
Mana hizo Mambo zenu investors na ku own some shares and real coins kwangu niliona isn't a big deal. I wanna make money whether on both rising and falling price an given financial instrument Ila najua hatuachani Ila usafiri tofauti.

Yes Bahamas and Cyprus and shelisheli na nchi nyingine kibao huwa hawana vigezo vikali vya kuwabana brokers ili raia wawe salama wasio na financial literacy.
Asic , FSA wamepiga ban mfano leverage maximum ni 1:33 mie hata 1:5/1-10 ndio nazopenda.
Sema Sasa wapo wanaopenda leverage mpaka ya 1:3000 wanapata mfano justforex sijui instaforex ili atimize kiu zao.
USA ilijaribu hata ku ban hizi mambo za cfd Mana none real assets owning so inaonekana Kama Ni kamali. Mana nasema mchele mwaka huu utashuka Bei so najaribu kuanza mchele kwa Bei iliyopo.
Am happy to find like minded niga.
You feel so much happy, we're traveling in bad road and lonely journey na ndio Mana watu wanaanza kufundishana smt ili uwe na your peers .
Uzi wako nimeupitia umechimba na uko aware ambavyo influencers wanaweza nunulika wakainfluence wakazama mazima like Elon musk Ali promote mno dogecoin na Ontario kweli Twitter akawa anafurahi anawavuta saivi sijui anasemaje.

Mie nimeamua ku spealize only in one field na Nina one or two pairs nazo trade I don't bother to look or distribution my fαckin expensive energy to many fαckinn bushηit
I am impressed to find someone who knows what he is doing. Hizi mambo ukienda kwa kuuelewa mchezo wala hupati shida, tatizo linaanzia pale ambapo wengi wanaingia kwa kusikia/ kuwa influenced bila kupewa the Pros and Cons. I like that kuwa unamaintain low leverage... Greedy ndio sababu kubwa inayowafilisi watu especially speculators; Unaanzaje kutumia leverage ya 1:3000 kwa mfano! Kwa vyovyote high levarage will f*ck you up, it is just a matter of time.

Let's keep going!
 
Nakufuata inbox
 
Kila kitu gharama ama cost so sio wote tulio tayari kuzilipia hizo gharama. That's why value iko reflected by a willing buyer to pay it in terms of cost.
Mie binti anaweza akaniambia nimsubiria miaka miwili ili nimuoe nikakataa Ila mwingine akakubali hata miaka kumi pia ilimradi asije akamkataa huko mbeleni.

So this is value tumetoa for the same product. Our subjectivity and biasennes ndio inayofanya dunia Ina run Mana unaniuzia kiwanja hakina value kwako Ila hela ndio yenye value kwako namie kwangu your land has value in my life kuliko hela nilizo nazo so we exchange our values,tunauziana ama tuna trade each to make dunia iende.

Ama nauza muda wangu na utalaamu wangu kwako wewe unanipa hela so hapa kila mtu Ana value.
Ujue wanasisitiza mno time management Ila inatakiwa iwe energy and value Management. Mana unaweza ukaniajili nikakaa kwa 30yrs nisiwe na value yoyote ingawa nilikuwa namanage time sema sikuwa na value.
 
Umeongea vitu vigumu kinoma mzee; sema I know - darasa la Economics halijawahi kuwa rahisi 😄🙌
 
Umeongea vitu vigumu kinoma mzee; sema I know - darasa la Economics halijawahi kuwa rahisi 😄🙌
Na fani yangu sio hii ya uchumi Ila may be iko by nature. Huwa namwambia mtu kuwa mwizi ama malaya Ni mtafutaji ama Ni wafanyabiashara sema Sasa wao value ya maisha yao is meaningless kwa wao binafsi kuliko pesa ama Mali wanayoitafuta.

Sema hao watu ukiwapata ukabahatika kuwabadilisha mindset zao ukaowanyesha biashara ama kazi nzuri mno yenye faida wakaielewa wakaifanya wanakuwa Ni watu wakubwa mno. Since they don't afraid to risk Sasa mtu Ana risk maisha yake kuyapoteza ataogopaje kupoteza hela sasa. Unamuona akina Pablo Escobar na muuzaji mmoja wa bangi wa jamaika alikuwa USA akawa deported na kufungiwa viza milele no USA entrance labda sijui afanyeje.

Watu Kama Ni higher risk takers,ama vijana wa west Africa wanaozamia na kukaa kwenye nanga ya melini siku 11 majini , they're traded their values mwingine anashangaa Ila yeye Ni normal kabisa Mana anaona value kwa kile anachotaka kuliko alicho nacho. I really real appreciate watu wenye mioyo iyo. Sio kitu kidogo mtu akakata tamaa Ila Sasa nakujaga kushangaa men take large risk when are seeking pиссi ujue. Yaani wako tayari hata watemewe mate ama wapoteze hata miaka kumi anawinda that pusci sema Nini man life liko Kama lilivyo ili dunia izunguke. Wakati unamshangaa naye anakushangaa Mana akaiona value for dat pusie
 
Oh boy! To some people "nyau" is everything. Kuna mchizi namjua alijinyonga kisa kakataliwa na mdada ambae ni 'mhudumu wa bar.' And the guy had everything, good business, gari kali, you name it... lakini akajichomoa kwaajili ya p*ssy; sad!

We value things differently, I guess that's nature.
 
Hilo la influencers Ni sawa la ma educators ukiwacheki education yao inamnuifaisha broker kwa kiasi kikubwa. Mana educators wanalipwa kuwapa elimu newbies wanazama wengi brokers wanapiga hela so wanapata hela na faida walizolipa educators ,hela zinaenda kwa educators wanawavuta new people in the arena wanapewa education wanajiona kuwa wamaelewa na emotions like greed and ego zikiwa kazini mtu ama fund akaunti naye anajiona amekuwa financial currency speculator anaanza kutangaza umma kuwa natredi the way to boast do you our ego how is working. Mana katika hii arena many losses yaani failure rate Ni kubwa hii 95% they don't lie with this statistics, it's true so ukianza ku trade tu Kuna Mambo kadhaa broker akikucheki anajua huyu tayari wetu hamalizi miaka ama miezi kadhaa Kama Ile 90/90/90 yao walivyo establish.
Hii elimu sahihi haipo hata kwenye mavitabu ambayo Ni easily available Mana yameandikwa highest sucker .
Elimu sahihi nimeipata kwa vitabu sahihi not more than five books they're unpopular na baadhi hata haviuzwi Kama vinavyojazwa mapeji ili ujione uko sahihi kutoa hela yako. Vitabu vya real traders Ni vingapi Kama sio vya journalists and educators waliokomaa kupata trading knowledge wakijua kuwa ndio key wakashindwa kufungua mpango ikabidi wa switch to teaching section and mentoring. Ila Sasa ukitaka kumu asses muulize show me 3yrs trading history ya kwako approved by third part, atatoa matusi Kama Nini ,yaani failure anatoa elimu

Kuna YouTube channel nzuri mno sema hazijawa monetized so don't appear oftentimes in our search engine so watu hawana nazo time.

Yaani we love sweet things and easily found shoot
 
Oh boy! To some people "nyau" is everything. Kuna mchizi namjua alijinyonga kisa kakataliwa na mdada ambae ni 'mhudumu wa bar.' And the guy had everything, good business, gari kali, you name it... lakini akajichomoa kwaajili ya p*ssy; sad!

We value things differently, I guess that's nature.
Sure nigger we see the same thing but we don't have the same vision and we don't see equally.
2,7,890,9000,76, are the same (both are numbers that quantify things) but not equal. Hii swaga enzi za 17-24 ndio nilikuwa nachukulia cat kirahisi mno
 
Yaani mpaka uje ugundue huyu mentor ama educators wa trading ana Mana gani ama hichi kitabu Ni Cha journalists na sio Cha trader it takes time and effort. Kwanza real traders hawana time ya kuandika vitabu Mana make more money trading than writing or teaching
 
NB: Uzi ni mrefu, kinoma 👽

Uchumi wa dunia umekuwa ukidorora kwa miezi (Kama sio kwa miaka) kadhaa sasa, na mdororo huo umeathiri pia thamani ya cryptocurrencies kwa kiwango cha kutisha. Watu wamepoteza mabilioni ndani ya muda mfupi, kiasi ambacho wengine wamechukua maamuzi magumu ya kujiondoa duniani kwasababu walichotarajia, hakikutimia.

Hii imezua maswali juu ya ahadi iliyotolewa na wavumbuzi + chawa wa Crypto - kwamba sarafu za Crypto ni pesa ambazo ziko nje ya mifumo ya kawaida ya kibenki, kwahiyo ni salama na "stable" zaidi kwasababu hakuna mtu, wala kampuni, wala mamlaka ya serikali inayoweza kuzi-control. Lakini, uhalisia unaonesha crypto imeanza kwenda kwa kutumia mifumo ile ile ya kawaida ya kibenki ambayo waanzilishi na mashabiki kindakindaki wa crypto walikuwa wanaikwepa.

Nimeona si vibaya nikaweka uzi wangu juu ya kinachoendelea katika ulimwengu wa crypto. Asomaye na afahamu; Mimi pia ni mtumiaji wa crypto, huku niliko tunaendesha programu ambayo kwa 95% pesa zake zipo katika crypto na mpaka sasa tumeshafanya miamala ya zaidi ya TZS 25M. Lakini uamuzi wangu wa kuleta uzi huu ni kutokana na kwamba sijaona mtu alieiongelea crypto kama ambavyo nitafanya hapa. Karibu!​

KWANI, HALI YA CRYPTO IKOJE KWA SASA?
Mpaka Disemba 2022, crypto zilikuwa zimepoteza wastani wa asilimia 60 ya thamani zake. Hizi hapa chini ni crypto maarufu zaidi duniani, acha zitusaidie kupata uelewa wa pamoja wa hali ilivyo kwa sasa;​
  1. Terra: Imepoteza asilimia 100% ya thamani yake.
  2. Solana: Imepoteza asilimia 93% ya thamani yake.
  3. AMP: Imepoteza asilimia 93%
  4. Cardano: imepoteza asilimia 80%
  5. Ether: Imepoteza asilimia 67%
  6. Bitcoin: Imepoteza asilimia 63%
  7. Dogecoin: Imepoteza asilimia 55%
Kwa pamoja hizi crypto zote unazozisikia, katika ubora wake zilikuwa na thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani Trilioni 3. Na sasa zina thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni 1 kwa ujumla, maana yake kuna Trilioni 2 zimeyeya!​

DUH! LAKINI SI NDIO HALI YA UCHUMI ILIVYO? KAMA UCHUMI WA DUNIA UNAPOROMOKA KWANINI UNADHANI CRYPTO ZISINGEPOROMOKA?
Well, Crypto zilibuniwa ili zije kuwa mbadala wa masoko ya fedha ya kawaida. Waanzilishi wa Crypto walikuwa wanazipigia debe kama mbadala wa fedha za kawaida ambazo zinasimamiwa na benki kuu za nchi mbali mbali. Kwahiyo, matarajio ni kwamba fedha za kawaida zinapoporomoka kimbilio liwe ni crypto, ila ndo kama hivyo hali imekuwa tofauti.​

MH! SIJAELEWA BADO - FAFANUA ZAIDI.
Ok, twende kwenye Historia kidogo: Asili ya crypto ni kipindi kifupi kilichofuatia baada ya anguko la uchumi wa dunia la mwaka 2008. Katika anguko lile tulishuhudia kifo cha moja ya benki kubwa duniani iliyofahamika kama Lehman Brothers ambayo imekuwepo duniani kwa miaka 158! Ulikuwa ni msiba mkubwa.

Mabenki wakati huo yalifanya ujinga ambao watu hatutarajii wasomi wa benki waufanye kwa kutumia pesa zetu ambazo tunawapelekea watutunzie. Mabenki yaliwakopesha sana watu ambao hawastahili kukopeshwa, mabenki yalikuwa yamelegeza vigezo vya kukopa, ili raia wakope sana. Ilitokea hivyo kwasababu benki kuu zilikuwa zimepunguza riba; mfano - Marekani ilipunguza riba kutoka 6.5% mwaka 2000 mpaka 1% mwaka 2003%.

Ukiona Benki Kuu ya nchi yoyote inatangaza kupunguza riba ujue lengo ni kuifanya pesa iwe rahisi kupatikana kwa raia wa kawaida, hali ambayo ina-boost uchumi uliosinyaa. Kwahiyo watu wakakopa sana kwasababu riba ni ndogo, wengine wakachukua nyumba za mikopo, watu wakanunua magari kwa wingi n.k.

Ili kuchochea moto zaidi, Federal Reserve ya Marekani ikapunguza hitaji la kiwango cha chini cha mtaji ambacho benki zinatakiwa kuwa nacho (Kwa benki tano kubwa za Marekani). Lengo lilikuwa ni kuzihamasisha hizi benki zichukue "risk" zaidi ya kuwakopesha raia. Matokeo yake hizi benki zika-leverage mitaji yake kwa zaidi ya mara 30 hadi 40. Maana yake benki nazo zilikopa kwa zaidi ya 30 ya uwezo wake ili nazo zikopeshe!

Waneni husema hakuna hali ya kudumu; eventually Federal Reserve ya Marekani ikaanza kupandisha riba mwaka 2004 ambapo ilipanda mpaka asilimia 5.25 iliyodumu mpaka mwaka 2007. Mdogo mdogo mabenki yakajikuta yana orodha ndefu za wadaiwa sugu ambao hawana uwezo wa kurejesha mikopo kwasababu walikopa wakati riba iko chini sana, na sasa wanatakiwa kulipa wakati riba iko juu sana. Vivyo hivyo wale waliokopa nyumba, ikawa ni mtihani mzito kwenye kuzilipia, na kuziuza ikawa haiwezekani kwasababu zilikuwa zinaporomoka thamani yake siku hadi siku (Housing Bubble).

Hatimae Benki ya Uswisi ikawa ya Benki kubwa ya kwanza kutangaza hasara, ambapo ilitangaza kuwa imepata hasara ya Dola za Kimarekani Bilioni 3.4 kutokana na 'mikopo ya kimchongo'. Benki kuu mbalimbali duniani zikajaribu kuokoa jahazi kwa kumwaga pesa kwenye mabenki ili kuzuia mporomoko wa uchumi, lakini kama wasemavyo "La kuvunda halina ubani". Mabenki mengi tayari yalikuwa yamevuka mstari mwekundu; yakawa yanashindwa kukadiria kiasi cha hasara ambacho watapata kutokana mikopo mingi ya kimchongo waliyonayo kwenye hesabu zao.

Februari 2008 Serikali ya Uingereza ikalazimika kuitaifisha benki ya Northen Rock. Machi 2008 moja ya Benki kubwa ya uwekezaji duniani iitwayo Bear Stearns ambayo ilikuwa ni mhimili wa Wall Street kuanzia mwaka 1923 nayo ikatangaza kufilisika, ambapo ikanunuliwa na benki ya JP Morgan Chase kwa thumni za dola! Fahamu kwamba Wall Street ni kama center ya masuala ya uuzaji na ununuzi wa hisa duniani. Ikafuata IndyMac Bank nayo ikafariki, na ndiposa mwezi Septemba 2008, Lehman Brothers ika-rest in pieces.​

ENHE, KWAHIYO? HAYO YANAHUSIANA VIPI NA KUANZISHWA KWA CRYPTO?
Anguko la uchumi la mwaka 2008 liliwaumiza wananchi wengi wa kawaida (Rudia tena kusoma neno "Wananchi wengi wa kawaida"). Wengi walipoteza ajira zao, wengi walipoteza nyumba zao, na wengi walipoteza akiba zao. Hasira ziliwapanda wananchi hawa wa kawaida kwasababu, baada ya 2008 benki nyingi ziliweza kusimama tena kwa kuwa zilipata pesa(Bailout) kutoka serikalini (Ambazo ni kodi za wananchi). Kwa wengi ilionekana si sahihi kwa serikali kuwapa pesa za walipa kodi watu ambao walizichezea pesa za wavuja jasho. Ikaonekana kama Serikali na mabenki lao moja - kuwanyonya wananchi kwaajili ya kujineemesha wao.

Japo kwa ujumla kitendo cha serikali kuingilia kati kwa kutoa pesa kwa mabenki kilisaidia kuurudisha uchumi mahali pake, lakini kwenye akili za raia wengi ilionekana ni kama serikali ilikuwa inawazawadia watu wa benki badala ya kuwaadhibu kwa uzembe uliogharimu uchumi wa dunia.

Anguko la uchumi la 2008 lilionesha udhaifu wa mifumo ya kibenki na Serikali. Hapo ndipo watu wakaanza kufikiria kuanzia mfumo ambao utakuwa ni mbadala wa mfumo huu mbovu uliopo.​

OK, KWAHIYO HAPO NDIPO TUKASIKIA BITCOIN IMEVUMBULIWA SI NDIO?
Yap! Bitcoin kama Crypto ya kwanza kabisa, iliingia kama sarafu ambayo hakuna wa kuidhibiti. Ni pesa mtandao, sarafu ya kidijitali ambayo kila muamala wake unarekodiwa katika Kitabu cha kimtandao cha kumbukumbu kinachofahamika kama "Blockchain". Vijana wengi wakaipokea Bitcoin kwa mikono na miguu yote, wakaingia wazima wazima kwasababu walikuwa wamechoshwa na sarakasi zinazofanywa na mabenki na serikali.

Bitcoin ilionekana ni pesa inayomlinda mtu dhidi ya Serikali. Kivipi? Utaniuliza. Well, Serikali inaweza kuzisimamia na kuzidhibiti pesa zako zilizopo benki - mfano inaweza kuzuia usizitoe, inaweza kuongeza tozo, inaweza kuongeza riba, inaweza kupunguza riba, inaweza kuzibadilisha, na inaweza ikafanya maamuzi ambayo yanaathiri thamani yake. Lakini hakuna kitu serikali inaweza fanya kwenye Bitcoin, na sarafu mtandao zingine.

Kwahiyo, maono ya waanzilishi wa Crypto ni kuwa na jamii ambayo watu wanaweza kufanya miamala kwa kutumiana pesa, kununua na kuuziana vitu wao kwa wao pasipo kuingiliwa na/au kuitegemea mamlaka ya serikali yoyote ile au taasisi binafsi yoyote ile duniani.​

AISEE! SASA NDOTO HIYO ILITIMIA?
Mwanzoni mambo yalienda vizuri kabisa. Lakini usisahau kuwa, watu wa mwanzo kabisa kuikimbilia Bitcoin kwa wingi walikuwa ni wahalifu, hususani wauza madawa ya kulevya.

Kulikuwa na soko mtandaoni linaitwa Silk Road ambalo kwa asilimia kubwa lilikuwa linategemea crypto. Mtu alikuwa ananunua madawa ya kulevya kule Silk Road, halafu mzigo unamfikia mpaka mlangoni kwake na yeye analipia kwa Bitcoin. Ukawa ni mfumo ambao watu wanauamini na kuutumia kwa malipo ya biashara haramu.

Ilikuwa ni njia rahisi na ya haraka ya kutuma pesa umbali mrefu mfano kutoka nchi moja kwenda nyingine, bara moja kwenda jingine n.k, ikarahisisha namna ya ku-track miamala, na ikaweza ku-maintain thamani.

Lakini kuna watu hawakuipenda taswira hii ya Crypto na uhalifu, walitaka kuionesha dunia kuwa crypto inaweza kusafishwa na kuwa njia mbadala ya malipo na ikatumiwa na kila mmoja duniani pasipo kuhusisha uhalifu.​

NIMEKUPATA, SASA CRYPTO ILIWEZAJE KUPENYA NA KUKUBALIKA NA WATU WENGI NJE YA WAUZA UNGA?
Wajasirimali. Kwa kutumia mbinu za kimauzo ikiwemo mbinu ya kupandikiza kitu kinachoitwa FOMO (Fear Of Missing Out), wajasiriamali wengi waliibeba agenda ya Crypto kama fursa ya kiuwekezaji. Wakawashawishi watu kuwa Crypto itakuja kuziondoa pesa za kawaida. Kwamba ndani ya miaka kadhaa hakutakuwa na haja tena ya kuwa na Shilingi, au Dola, au Paundi, Au Euro n.k. Kwamba ndani ya miaka kadhaa hakutakuwa na haja ya kuwa na mabenki kwasababu watu watakuwa wanamalizana wao kwa wao bila kuwa na haja ya uwepo wa Serikali au "Mtu kati".

Mdogo mdogo watu wakaanza kuelewa somo, uhitaji wa Bitcoin ukaanza kuongezeka. Bitcoin ikaanza kupanda thamani kwasababu ya demand kubwa. Kampuni mbalimbali zikaibuka kwaajili ya kutumia fursa zitokanazo na Bitcoin. Na kwa kuona mafanikio ya Bitcoin, Crypto zingine zikaanza kuibuliwa pia. Zingine zilipata umaarufu kimasihara tu mfano Dogecoin🐶!​

NOMA SANA, NASIKIA WATU WANASEMA MLIPUKO WA KORONA ULIWEZESHA THAMANI YA CRYPTO KUPANDA, NI KWELI?
Ni kweli. Kila baada ya kipindi fulani Dunia huwa inashuhudia jambo linaibuka, linafikia kilele cha umaarufu, kisha linaporomoka ghafla na pengine linapotea kabisa. Kisha linaibuka jingine linaenda mzunguko uleule - wenyewe wanaita "Boom and bust cycles".

Hakuna watu wanaweza kumshukuru "aliyetengeneza" kirusi cha Korona kama watu wa Crypto. Maana Korona ilipelekea marufuku za watu kuzurura mitaani, kwenda makazini, kusafiri n.k. Hali hiyo ilipelekea watu kutumia muda mwingi wakiwa wamejifungia ndani. Lakini maisha ilikuwa ni lazima yaendelee; miamala ilikuwa ni lazima ifanyike. Na njia rahisi ilikuwa ni kulipa kwa njia ya mtandao. Hapo ndipo tukashuhudia crypto zikipanda thamani kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa kabla.

Watu wengi walijikuta wako majumbani, na hivyo muda mwingi walikuwa wanautumia mitandaoni. Hata manunuzi yakawa yanafanyika mtandaoni. Na kuna baadhi ya nchi raia walikuwa wanalipwa pesa kiasi kwaajili ya kujishikiza - maana yake watu wakaanza kupata pesa ambazo hawajazitolea jasho. Na kwakuwa watu walikuwa na pesa zisizo na jasho wakaanza kuzitumia hata kwa vitu "risky" kama vile kuwekeza kwenye crypto. Na tukaanza kushuhudia mtu anawekeza Dola 10 anapata Dola 100. Mtu anaweka TZS 500,000/= inapanda mpaka milioni kadhaa ndani ya muda mfupi. Tazama Bei ya Bitcoin ilivyoongezeka miezi mitatu tangu WHO walipotangaza kuwa COVID-19 ni Pandemic (Mwaka 2020).

View attachment 2473358

Hapa ndipo makampuni kibao yakaibuka. Na mengi yalikuwa yanahimiza watu kuwekeza kwenye crypto. Ilikuwa kila kona unakutana na matangazo ya Crypto. Watu maarufu duniani wakaanza kuwa ma-influencers wa Crypto. Kuna uwanja unaitwa Staples Center ambao unatumiwa na timu maarufu ya mpira wa kikapu ya LA Lakers nchini Marekani - ulibadilishwa jina na sasa unaitwa Crypto.com Arena.

Kuna tangazo moja linamhusisha muigizaji maarufu wa Marekani aitwaye Matt Damon; HILI HAPA kwenye hilo tangazo (La Crypto) anatoa ujumbe rahisi tu lakini ni mzito, kwamba "Fortune Favors The Brave." Matangazo ya hivi yalikuwa mengi sana.

Haya matangazo na hawa influencers walichokuwa wanajaribu kuwaambia watu ni kwamba; "Wekezeni kwenye crypto kabla hamjachelewa, mkiikosa hii nafasi leo mtakuja kuijutia kesho." Na karibu matangazo yote ya Crypto yanaegemea kwenye kitu kimoja - FOMO. Kwamba usiponunua crypto leo basi wewe ni mjinga, wewe hujielewi, wewe unapitwa na wakati, wewe ni mshamba, wewe ni muoga, na message zingine kama hizo.

Hii "hype" ya wakati wa pandemic ndio ilikuwa "Golden era" ya crypto. Watu wengi hawakutaka kupitwa kama ambavyo matangazo yanawashawishi. Hapa ndipo Crypto ikaingia "mainstream", ikawa habari kubwa duniani. Kila mtu akawa ni "mtaalamu" wa crypto, unapita kijiweni pale Njombe kwetu unakuta bodaboda wanaongelea biashara ya "Kucheza Bitcoin" 😝😆😆 na ikaambatana na biashara ya "Kucheza FOREX" na ikaambatana na biashara ya "Kuweka mikeka" 😎​

TUKO PAMOJA, NINI KIKAFUATA?
Well, nimeongelea mara kadhaa kuwa kampuni nyingi ziliibuka wakati huo wa pandemic. Ambacho sijasema ni kuwa hizi kampuni hazikuwa zinatengeneza crypto mpya, bali nyingi ziliingia kwaajili ya kuwawezesha watu kufanya miamala ya crypto. Chukulia mfano wa Benki; benki hazitengenezi pesa, bali zinawawezesha watu kutunza na kufanya miamala ya pesa.​

Kwahiyo, kampuni nyingi zilizoibuka zilikuwa ni kama "Crypto Banks".

HEH!?! BENKI TENA? MIMI NILIJUA WATUMIAJI WA CRYPTO WANAZICHUKIA BENKI? INAKUWAJE KUNAKUWA NA "BENKI" ZA CRYPTO?🤔
Kwakweli hata mimi nashindwa kushangaa; ni ajabu na kweli. Lakini ninachojua hizi kampuni hazijiiti benki. Na wala hazisimamiwi kama benki. Lakini kiuhalisia zinafanya kazi kama benki 🤓 (Rudia tena kusoma). Unaweka crypto yako, unaiacha kwa muda fulani - inazalisha faida vile vile kama ambavyo ukiweka pesa benki kwenye "savings account" zinazalisha faida.​

Nitatoa mfano mmoja: Kuna kampuni inaitwa Celsius ambayo ilikuwa inajinadi kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 1.5

View attachment 2473475

Hii kampuni ilianzishwa na mtu anaitwa Alex Mashinsky. Huyu mchizi ana historia ya utapeli-tapeli, anaongea sana na muongo muongo - ila ana nguvu ya ushawishi (Very charismatic). Kwahiyo, baada ya kupiga utapeli kwenye biashara zingine huko - akakutana na Crypto, akavutiwa na fursa zake, akaanzisha kampuni.​

ALIWEZAJE KUWASHAWISHI WATEJA?
Ni rahisi tu; alikomaa na pointi moja kwamba "Benki za kawaida zinawadanganya watu na kuwaibia pesa zao!". Hiyo ndio ilikuwa "Selling point" yake. Kwamba, "Sikieni nyie watu; Mfano una hela zako, unazipeleka benki, benki wao wakishazipokea wanazikopesha mikopo ambayo ina riba mpaka asilimia 25%, wakati huo wewe wanakupa chini ya asilimia 1% (Kwa akaunti ya kawaida). Hilo ni tatizo, kwasababu imefika mahali tunaona ni sawa na tunaendelea kuwapa pesa zetu na wao wanaendelea kutajirika wakati sisi maisha yetu yanabaki vile vile."

Baada ya kuwagonga watu na hiyo pitch, then anawaambia kuwa Celsius itafanya kinyume chake; Itachukua crypto zako, itawekeza na kuzalisha faida kubwa, kisha asilimia kubwa ya faida utachukua wewe!🥳 Kwahiyo, Celsius inakuwezesha wewe kutumia pesa zako kutengeneza pesa kirahisi kabisa!

Jamaa alikuwa anaweka videos YouTube kila wiki kama dozi. Akawa ana-tweet kinoma. Na kwasababu wakati huo watu wengi walikuwa majumbani, wameshiba, wananenepeana tu, ujumbe ukawa unawafikia barabara kabisa. Boom, wateja wakaanza kuzipeleka crypto zao Celsius. Jamaa alikuwa anahubiri injili ya Crypto kisawasawa na ikawa inawaingia watu; na watu wanaokoka kwenda kwenye Crypto kupitia Celsius kutoka benki za kawaida 🤪​

KWANI FAIDA ILIKUWA NI KIASI GANI UKIWEKEZA CELSIUS?
Kama ilivyokuwa kwa crypto banks nyingi, ilikuwa ni 18%. Hii haikuhitaji kufikiria mara mbili, hakuna benki itakupa riba ya asilimia 18% kwenye akaunti ya kawaida. Na kumbuka; hii haikuwa kama hisa au cryptocurrency zenyewe ambazo unanunua ukiwa na matumaini kuwa thamani yake itapanda (Japo moyoni una uhakika itashuka 🤣), hawa Celsius walichokuwa wanakifanya ni hivi;

Wewe unaweka crypto yako kwa kuanzia kama mtaji. Kisha baada ya hapo inakuwa ni mwendo wa kupokea 18%, huwazi suala la thamani kushuka wala nini. Inakuwa kama umepanda crypto hivi, baada ya hapo ni mwendo wa kuzivuna 🤑🤑🤑🤑

Na amini usiamini, wajinga duniani hawatokuja kuisha. Watu hawakuona kuwa huu ni utapeli, bali wengi waliamini hizi ni "Hela za bure" zinazotolewa na Celsius... asalaleee!!!🥱​

EBWANAEEEE! LAKINI, WAO CELSIUS FAIDA WALIKUWA WANAITENGENEZAJE?
Haijawahi kueleweka, lakini kitu kimojawapo ambacho Celsius walikuwa wanakifanya; ni kuchukua pesa (crypto) za wateja, kisha wanazikopesha kwa wawekezaji wakubwa na wafanyabiashara professional, na wale wawekezaji walikuwa wanakopa kwa riba, kwahiyo wakilipa na wao Celsius wanazisukuma kwenda kwa mteja. Lakini "Common sense" inagoma kukubaliana na hili.

Namba zinagoma, haiingii akilini kuwa kwa kufanya hivyo waliweza kuwahudumia wateja wote hawa zaidi ya 1.5M. Kuna mengi ambayo hatuyajui yaliyokuwa yanafanyika nyuma ya pazia.​

MH! KWANI HAKUKUWA NA WAKOSOAJI? HAKUKUWA NA WATU WA KUUANIKA HUU UTAPELI?
Walikuwepo; wanauchumi, wataalamu wa masuala ya kibenki na masoko ya mitaji n.k. Walijitahidi kwakweli kuwaelimisha watu kuwa hakuna pesa za rahisi namna hiyo katika mifumo ya kifedha. Wengi walikuwa wanawatahadharisha watu kuwa hii ni "Ponzi Sheme"

Kitu kingine kilichokuwa kinaleta hofu zaidi kwa wataalamu wa uchumi ni kwamba; Akiba ambazo watu huwa tunaweka benki huwa zinakatiwa bima, lakini kwa Celsius - akiba za watu hazikuwa na bima yoyote! Lakini kwa namna moja ama nyingine, ni vigumu sana kumshawishi mtu anaekaribia kutapeliwa kuwa atatapeliwa; huwa ni wabishi kinoma!

Usiniulize Serikali huwa hazioni au la, kwasababu hata mimi sijui!​

SASA, IKAWAJE? CELSIUS IKAISHIAJE?
Uchumi wa dunia ukaanza kuyumba yumba, Urusi ikaivamia Ukraine, mataifa bado yalikuwa yana "hangover" ya Korona, mifumo ya usambazaji wa bidhaa duniani ikaathirika kwa kiwango kikubwa sana. Benki kuu zikaanza kuongeza riba, lengo ni kuwafanya watu wasitumie akiba zao ovyo na hiyo inamaanisha mtelezo wa kwenda juu ukawa umeishia hapo. Watu badala ya kununua hisa, wakaanza kuziuza kwa kasi, hisa zikaanza kuporomoka bei, na vivyo hivyo crypto nazo zikaanza kuporomoka. Ghafla watu wengi wakaacha kuziamini crypto hivyo wakaanza kuzitoa (Ku-withdraw). Bei za crypto zikawa zinashuka kama mwewe.

Hata coin inayoitwa Terra USD ambayo ilibuniwa kwa namna ambayo thamani yake inaenda sambamba na thamani ya dola, kwenye ule mporomoko nayo haikuachwa salama.

Ikawa kama muvi la kutisha vile; project nyingi za crypto zikaanza kuanguka kwa pamoja ndani ya muda mfupi. Wazungu wanaita "Domino effect" - kikianguka kitu kimoja kinasababisha vingine vingi vianguke. Mabilioni ya dola yakageuka moshi ndani ya siku chache.

Kwahiyo, hata wateja wa Celsius wakawa wanataka kutoa pesa zao pamoja na riba ambazo wamejikusanyia kwa kipindi chote na ambazo walikuwa hawajazichukua. Kikatokea kitu ambacho mabenki huwa yanakiogopa , kinaitwa "Bank run". Bank run ni pale ambapo wateja wengi wanataka kutoa pesa zao zote kutoka benki kwa mkupuo. Mara nyingi huwa inakuwa ni dhahama kubwa kwasababu uwezekano wa kuwepo pesa za kutosha watu wote kutoa kwa mara moja unakuwa ni mdogo sana, kiasi ambacho mara nyingi ikitokea "Bank Run" benki huwa zinalazimika kusitisha miamala.

Basi buana, Celsius ikasitisha miamala. Hiyo ilikuwa ni mwezi wa sita mwaka jana. Kuna utani mtaani kuwa, kwenye ulimwengu wa crypto ukisikia wametangaza kuwa wamezuia kufanya miamala kwa muda basi ujue ndo mazishi hayo. Ni nadra sana kwenye crypto wakasitisha miamala kisha wakaruhusu baada ya muda, sikumbuki kama imewahi kutokea.

So, tangazo la Celsius la kusitisha miamala likazidi kuutikisa ulimwengu wa crypto. Bei zikazidi kushuka kwa kasi ya 6G. Na hatimae wiki chache baadae Celsius ikatangaza kuwa imefilisika🤒. Watu wakabaki njia panda - crypto zao watapata au hawazipata tena? Well, mpaka leo haijulikani ni nini kitatokea.​

PHEW! KWAHIYO SASA INAKUWAJE; KWANI INA MAANA WATU HAWAKUJUA KUWA CRYPTO NI KAMA KAMARI?
Watu wengi waliowekeza kwenye crypto kwa ushawishi wa ma-influenza na matangazo na mwisho wa siku wakapoteza pesa zao - huwa wanajihisi wametapeliwa. Kwamba wakati wanawekeza huwa wanaahidiwa usalama wa pesa zao, na uhakika wa faida. Wengi wamepoteza akiba zao za maisha, wengine wamepoteza mitaji yao ambayo waliiwekeza wakitumaini itakua mikubwa ili wawekeze zaidi n.k. Na kuonesha hali ilivyo mbaya, wapo wengi waliojinyonga kwasababu ya kupoteza pesa katika uwekezaji wa crypto.

Wengi wanawalaumu watu maarufu kwa kutumika vibaya kuwashawishi watu kuingia kwenye biashara ambazo mwisho wake huwaumiza watu wa hali ya chini.​

ENHE, ULISEMA CRYPTO KUNA AHADI HAIJATIMIZA - NI AHADI IPI HIYO?
Crypto ilidizainiwa kuwa mbadala wa mifumo ya kibenki; mifumo ambayo kuna "mtu" anasimamia na kufanya maamuzi juu ya pesa za watu wengine. Na kwasababu ni mtu mmoja au kikundi cha watu wachache ndio kimepewa mamlaka ya kusimamia pesa za watu wengi - uwezekano wa makosa kufanyika ni mkubwa. Nimeeleza kilichotokea kabla ya anguko la uchumi la 2008. Maamuzi mabovu ya watu wa benki yalipelekea watu kupoteza pesa zao. Crypto ilitengenezwa ili kuzuia hilo lisitokee tena, lakini kama ulivyoona, yanatokea yale yale ambayo watu wa crypto walikuwa wanayakwepa.

Kwahiyo; ahadi ambayo haijatimia ni ahadi ya crypto kuwa mbadala wa pesa za kawaida ambazo zinazimamiwa na serikali na kuratibiwa na mabenki na taasisi za fedha kwa sheria na kanuni mbalimbali. Mijadala inaendelea kuhusu kama kweli crypto itaweza kuleta suluhisho la mapungufu yaliyopo katika mifumo ya kibenki. Kuna watu wanaona cryto ni utapeli tu na ni suala la muda kabla haijapotea kabisa, na kuna watu wanaona crypto ndio future. Inawezekana wote wapo sahihi, inawezekana wote wanaota ndoto za Abunuwasi, sisi acha tuendelee kuishi.​

SO, CRYPTO IMEKUFA AU?😪
Ni mapema sana kulisema hilo. Ni kweli crypto imepoteza thamani kubwa, lakini bado kuna watu wanaendelea kuwekeza. Na sio kampuni zote za crypto zimekufa, kuna zingine bado zinaendelea kuwahudumia wateja mpaka sasa tunavoongea.

Kuna watu wapo katika ulimwengu wa crypto sio kwaajili ya faida au hasara; wao wanavutiwa na namna crypto ilivyoundwa na inavyofanya kazi. Na wanatumia teknolojia ambayo ni msingi wa crypto kuleta mapinduzi mengine ya teknolojia.

Kama ambavyo wakati intaneti inaingia, kampuni nyingi zilikufa (Dot Com Bubble) lakini zile chache zilizoweza kupenya zimekuwa ni kampuni kubwa sana duniani hivi sana. Inaweza kutokea hivyo hata kwenye crypto, tumeshuhudia kampuni kubwa za Crypto zinafilisika, lakini chache bado zinaukaza mwendo. Ni nani ajuaye pengine tukivuka hapa Crypto itasimama tena. Yote kwa yote crypto haionekani kuwa ni kitu kinachoweza kupotea ghafla, bado tunayo sana; na baadhi yetu tuna shauku ya kujua ni nini kitafuata baada ya hapa.

Homework: Fuatilia kuhusu Quadriga CX na FTX, kuna mengi utajifunza kuhusu crypto.​

Naweka kipaza chini.

Mimi... ninashukuru.
Elimu murua sana.

Binafsi hela za kudownload mitandaoni huwa naziogopa sana.

Mkuu wewe umepoteza kiasi gani?
 
Elimu murua sana.

Binafsi hela za kudownload mitandaoni huwa naziogopa sana.

Mkuu wewe umepoteza kiasi gani?
Kwanza hili neno la "Hela ya kudownload" nadhani limekuwa coined na watu wanaotaka kuuaminisha umma kuwa trading ni rahisi, kitu ambacho hata wao wanajua si kweli. Kwa maoni yangu, hakuna hela za kudownload, kwamba ziko mahali wewe kazi yako ni kuzipakua tu. Ninachojua ni either unafanya biashara kwa kujua unachokifanya au una-bet/unabahatisha (Una-download).

Ndio maana mabenki yanafanya hizi trading, yameajiri watu mahsusi kwaajili ya speculative trading. Utofauti wao na sisi traders wa mtaani ni kuwa wao wanasimamiwa na sheria and so kuna kiwango cha mtaji ambacho ni lazima wa-maintain. Kwahiyo hawawezi ku-bet na ku-risk kwa kiwango ambacho kitaathiri shughuli za benki. Kwa lugha nyepesi; wana-trade professionally, na sio kwa mihemko au tamaa.

Binafsi nimechoma pesa kama ilivyo kwa kila trader duniani; japo siwezi kutaja kiwango hapa 😉 However, kwa sasa sifanyi speculation; nipo najaribu namna zingine.
 
Duu Kama umeamua ku quit it's okay. Ila hii game Kuna mahala nilifika nikasema Ni halali success rate iwe only5% ,yes Ni halali. Huu mlima huwezi kuupanda ovyo ovyo. The main source of driving force ndio inayoweza ikakufanya uupande. Yaani hapa nilipofikia uniambie kesho niamke kichwa kipo tupu about trading halafu niambiwe nianzie upya sianzi yaani sijaribu Ni Moto mkali mno na Tena unachoma mno. Inahitaji uwe jasiri mno uutembee usiyasikie hayo maumivu.
Ila your pains behind if it's greater than the pain of trading am sure you'll pass.
Kiukweli binafsi siwezi mshauri mtu aingie Mana ataangamia nasema kuwa lazima ataangamia tu yaani lazima ataangukia pua apende asipende. Sasa mie nishauri mtu akaumie jamani ama afilisike.
Ila akiwa tayari kutenga miaka 7-10 ndio nitaweza kumwambia pita katika bahari ya Moto. Unaungua na huku hujui unapoelekea waves zinakupeleka popote na huku unaungua.
 
Kwanza hili neno la "Hela ya kudownload" nadhani limekuwa coined na watu wanaotaka kuuaminisha umma kuwa trading ni rahisi, kitu ambacho hata wao wanajua si kweli. Kwa maoni yangu, hakuna hela za kudownload, kwamba ziko mahali wewe kazi yako ni kuzipakua tu. Ninachojua ni either unafanya biashara kwa kujua unachokifanya au una-bet/unabahatisha (Una-download).

Ndio maana mabenki yanafanya hizi trading, yameajiri watu mahsusi kwaajili ya speculative trading. Utofauti wao na sisi traders wa mtaani ni kuwa wao wanasimamiwa na sheria and so kuna kiwango cha mtaji ambacho ni lazima wa-maintain. Kwahiyo hawawezi ku-bet na ku-risk kwa kiwango ambacho kitaathiri shughuli za benki. Kwa lugha nyepesi; wana-trade professionally, na sio kwa mihemko au tamaa.

Binafsi nimechoma pesa kama ilivyo kwa kila trader duniani; japo siwezi kutaja kiwango hapa 😉 However, kwa sasa sifanyi speculation; nipo najaribu namna zingine.
Sasa ma trader mbona mnakatisha vijana tamaa?
Binafsi naamini huwezi shindana na algorithim watu wanazotengeneza ili kujipatia hela za watu wanaotaka hela kirahisi mtandaoni. Yes I call them hela za kudownload.

Yani you are just sitting there wait for the chat kupanda na kushuka upate hela. While hayo mambo yapo controlled na watu wengine wanaosubiri ukosee akulambe....

Biashara zote ziwe za mtandaoni au shambani zina hasara na faida. Ila risk za mitandaoni ni kubwa sana. Kukimbizana na algorithim za watu ni kazi kuliko kazi yenyewe....

Ndio mambo ya kaylanda, yule jamaa wa mazao, mr. Kuku na vitu kama hvyo. Kuwa leta hela nikufanyie kazi halafu subiri faida. Yani mtu hataki kusikia kuwa kuna hasara tugawane yeye anataka faida tu kila mwezi. Hizi system kuna siku lazima zi collapse tu ni suala la muda....

Hakuna hela ya kupanda na kuivuna kirahisi..
 
Bado sio guarantee kuukwea mlima anaweza asifike kileleni Ila atakuwa na knowledge ya trading so ataishia kuandika vitabu na kufundisha na elimu anayotoa iko sahihi sema hawezi akaitumia kupatia hela tokea sokoni
Ukweli mchungu ambao sio wengi watausema.... especially wale wanaofaidika na kuuza signals and kozi za trading 🤓
 
Back
Top Bottom