Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kila inapozungumziwa Cuba mara nyingi sifa zake huwa ni mfumo mzuri wa afya tu ulioweza kuzalisha madaktari wengi hadi wa ku export na sekta ya uzalishaji madawa iliyoshamiri. Huwezi kusikia kingine cha kuvutia na kusisumua huko Cuba.
Hivi karibuni ndio nilimsikia Balozi Polepole akija na jambo lingine la kwamba miji ya Cuba imepangiliwa vizuri sana kiasi cha kuweza kuweka rula mtaa mzima bila kupinda. Hata hivyo miji ya Cuba huwa inaonekana kama magofu ya kale, sijui raia hawana pesa za kupaka rangi na kufanya maboresho ya nyumba.
Hivi nchi ya Cuba ina kingine cha maana cha ziada zaidi ya sekta nzuri ya afya? Ukiangalia GDP per capita yao ni kama Botswana tu, ni hasara sana kuwa pua na mdomo na Marekani halafu uwe lofa kiasi hicho, viburi vingine havina maana kabisa.