beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Lipumba, ametangaza kuwa kutokana na uchaguzi mkuu ulivyoendeshwa nchini, chama hicho hakitashiriki uchaguzi wowote na badala yake kitajikita katika harakati za kudai katiba mpya, ili kupatikana kwa Tume huru ya Uchaguzi.
“CUF tunawaomba Watanzania wote wapenda haki kuungana na sisi katika ibaada siku ya Alhamis, ambapo tutafunga kwa kutokula mchana na tufanye dua na maombi kila mmoja kwa imani yake ili kuomba hukumu ya haki kutokana na kile kilichofanyika”- Prof. Lipumba.