Uchaguzi 2020 CUF yatangaza kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wowote

Uchaguzi 2020 CUF yatangaza kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wowote

Hapa wanachotaka ni hiki.

CDM pamoja ACT nao wakubaliane na matokeo ili nao wadai KATIBA MPYA.

Kitendo cha kukubali matokeo na kudai katiba mpya ni kaburi ambalo vyama vya upinzani watakuwa wamelichimba na kuingia wenyewe.

Uwezekano wa kupata Katiba Mpya haupo, awamu ya 5 ni ya kinyama, bunge lote ni yellow and green, nani wakuijadili hiyo Katiba?

CUF hapa inatumika kama chambo tu ili kunasa vyama vingine vya upinzani ili viingie mkenge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila tume huru ya uchanguzi hakuna lolote la haki. Washirikiane pamoja kuandaa vuguvugu la kutadai na mabadiliko ya tume ya uchaguzi kwa miaka hii mitano ijayo.
 
Baada ya chaguzi ndogo za marudio, uchaguzi wa serikali za mitaa na dosari zote za tume ya uchaguzi na katiba tuliyonayo sasa, huu ndo ulitakiwa uwe msimamo wa vyama vyote vya upinzani kutoshiriki chaguzi zote mpaka tume huru na katiba mpya. Kuandamana kwa sasa ni upumbavu to be honest
 
View attachment 1617788

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Lipumba, ametangaza kuwa kutokana na uchaguzi mkuu ulivyoendeshwa nchini, chama hicho hakitashiriki uchaguzi wowote na badala yake kitajikita katika harakati za kudai katiba mpya, ili kupatikana kwa Tume huru ya Uchaguzi...
Hii itakuwa danganya toto ili kujaribu kusafisha jina la chama. CUF kwa sasa ni mali ya sisiemu
 
huu ndo ulitakiwa uwe msimamo wa vyama vyote vya upinzani
Hilo haliwezekani kwa kuwa vingi kwny kundi hilo vinamilikiwa na CCM. So, wengine mkigoma baadhi vikafuata maelekezo ya mwenye mali vikashiriki Kama kawa, hakuna impact yoyote itapatikana. Itakuwa sawa tu na kususia ngedere shamba la mahindi
 
View attachment 1617788

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Lipumba, ametangaza kuwa kutokana na uchaguzi mkuu ulivyoendeshwa nchini, chama hicho hakitashiriki uchaguzi wowote na badala yake kitajikita katika harakati za kudai katiba mpya, ili kupatikana kwa Tume huru ya Uchaguzi.

“CUF tunawaomba Watanzania wote wapenda haki kuungana na sisi katika ibaada siku ya Alhamis, ambapo tutafunga kwa kutokula mchana na tufanye dua na maombi kila mmoja kwa imani yake ili kuomba hukumu ya haki kutokana na kile kilichofanyika”- Prof. Lipumba.
Stupid

Kajua lini?
 
Hapa wanachotaka ni hiki.

CDM pamoja ACT nao wakubaliane na matokeo ili nao wadai KATIBA MPYA...
Hata kama hawatakubaliana na hoja ya Cuf ni ndoto kuamini kwamba Tanzania hii kutakuwa na uchaguzi wa haki bila tume huru
 
Wazo jema, pawe na mikakati dhabiti kudai katiba bora sambamba na mifumo ya taasis imara.
 
Atangaze kufuta na chama chake maana kimepoteza mvuto kabisa
Huo ni ushauri mzuri, bora vyama vyote vya siasa vikarudishe fomu zao za usajili ili kuwepo na chama kimoja kuliko kupoteza wakati, fedha na kudanganyana kwa uchaguzi wa maigizo.
 
Uyu jamaa kwenye mkutano wa CCM ALIOMBA apewe viti vitano vya ubunge,

Naona kapewa kimoja, anakuja apa kulia Lia.

Pumbavu kabisa[emoji3525]
 
Back
Top Bottom