NMB bank kubwa ila hadi leo kutoa hela mpaka mpange mstari kama wanafunzi wa shule ya msingi wanaenda kunywa uji.
Tena ambavyo hiyo benki hawana adabu wamechora mistari ya ribbon zao kukuonyesha mjipange kwa kupindapinda humo ndani.
Kwani wanashindwa nini kuweka vibao vya kielektroniki kama CRDB ambapo ukiingia unaingiza data kwenye system inakupa namba na utaitwa dirisha husika huku ukikaa kwenye bench.
Na kwanini Jumapili mjini ni almost NMB Mlimani City pekee inafanya kazi, matawi mengi yanafungwa nadhani hata la bandari napo wanafungua.
NBC hao unasajiri akaunti unazuiliwa kufanya transaction ya maximum milioni 3 tu kwa siku, huu ni utaratibu nadhani ni BoT wanalazimisha, mnadhani mnaweza zuia mfanyabiashara kufanya transactions? Si anaandikisha kadi hata za babu zake vijijini unakuta mtu mmoja ana kadi 9 za benki moja. Alafu NBC ina wafanyakazi wengi wasiojua huduma zao. Sijui haitoi training, yani wapo ilimradi. Na huwa hawasemi ukisajiri.
Kwa mabenki yote, tabia ya kuwa na madirisha manne ya watoa huduma alafu ni moja tu linafanya kazi muache. Kwani wakati mnaajiri hamkujua wafanyakazi wenu wataenda chooni?
Unakuta madirisha matatu wote hawapo, nani alileta huu utaratibu wa kukalisha sana watu kwenye matawi ya benki Tanzania.