Customer care: Kuna shida kubwa sana kwa makampuni mengi hapa nchini kuwa na poor customer care kwa wateja wake. Toa ushuhuda wako hapa!

Customer care: Kuna shida kubwa sana kwa makampuni mengi hapa nchini kuwa na poor customer care kwa wateja wake. Toa ushuhuda wako hapa!

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Kama mteja, uliwahi kukumbana na aina gani ya ugumu pale ulipohitaji msaada kutoka kwa huduma kwa wateja?

impact-of-poor-customer-service.jpg
 
NMB bank kubwa ila hadi leo kutoa hela mpaka mpange mstari kama wanafunzi wa shule ya msingi wanaenda kunywa uji.
Tena ambavyo hiyo benki hawana adabu wamechora mistari ya ribbon zao kukuonyesha mjipange kwa kupindapinda humo ndani.
Kwani wanashindwa nini kuweka vibao vya kielektroniki kama CRDB ambapo ukiingia unaingiza data kwenye system inakupa namba na utaitwa dirisha husika huku ukikaa kwenye bench.
Na kwanini Jumapili mjini ni almost NMB Mlimani City pekee inafanya kazi, matawi mengi yanafungwa nadhani hata la bandari napo wanafungua.

NBC hao unasajiri akaunti unazuiliwa kufanya transaction ya maximum milioni 3 tu kwa siku, huu ni utaratibu nadhani ni BoT wanalazimisha, mnadhani mnaweza zuia mfanyabiashara kufanya transactions? Si anaandikisha kadi hata za babu zake vijijini unakuta mtu mmoja ana kadi 9 za benki moja. Alafu NBC ina wafanyakazi wengi wasiojua huduma zao. Sijui haitoi training, yani wapo ilimradi. Na huwa hawasemi ukisajiri.

Kwa mabenki yote, tabia ya kuwa na madirisha manne ya watoa huduma alafu ni moja tu linafanya kazi muache. Kwani wakati mnaajiri hamkujua wafanyakazi wenu wataenda chooni?
Unakuta madirisha matatu wote hawapo, nani alileta huu utaratibu wa kukalisha sana watu kwenye matawi ya benki Tanzania.
 
Kama mteja, uliwahi kukumbana na aina gani ya ugumu pale ulipohitaji msaada kutoka kwa huduma kwa wateja?
Kuna vibibi viko mapokezi za mahakama zetu, vinakupokea vikitabasamu utadhani vinakupenda, jichanganye na wewe vikenulie meno utatolewa upepo ujute kuzaliwa
 
Niitembeleq Pharmacy, nikamkuta mshangazi nikaulizia dawa akani9nyesha akanitajia na bei batili. Nikajarbu kumuuliza kama "Kunaweza kua na dawa nyingine yenye bei ya chini kidogo"

Akanipokonya dawa akanambia "Me sinaga customer care sibembelezi watu wateja ondoka"

Nilitulia kamadk 5 kimyaaaa kisha nikamwambia "Hongera kama huo ndo ujanja pekee ulonao mpaka umri huo"

Nikajiondokea japo nilitaman nimrie makofi mjinga huyuanaemwaribia Boss wake Biashara.
 
Kadi yangu ilikuwa na matatizo kwenye ATM

Nimekaa benki mpaka saa kumi jioni,nitarudi kesho.
 
Katika makosa ambayo nimefanya ni kununua king'amuzi Cha startimes aisee a big mistake
 
KUNA KAMPUN MJINI NIMEENDA SAA SABA NIMEAMBIWA NA MLINZI NJOO SANANE AWARUHUSU KUINGIA MTU WAKO LUNCH AISEE BADOOOSANA
 
Wananiboa sana makondakta wa daladala.... extremely poor customer care
 
Nakubali.
Wengi hawawezi kutatua changamoto za wateja wao.
Wapunguze nyodo aisee
 
Back
Top Bottom