Customer Care wote wa CRDB, NMB, Voda & Tigo - jiandaeni kufukuzwa kazi

Customer Care wote wa CRDB, NMB, Voda & Tigo - jiandaeni kufukuzwa kazi

Internet-Money

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2021
Posts
493
Reaction score
1,135
Ni swala la muda muda tu , watu wengi wataachishwa kazi kwenye makampuni makubwa, kutokana na kukua kwa teknolojia.

Kuna robot anaye-trend huku mtandaoni , anaitwa ChatGPT. Huyu robot anauwezo wa kukujibu swali lolote kwa sekunde 1.

Tukija kwenye swala la customer care wetu, mko wengi sana na mpaka mteja ahudumiwe atasubiri hata kwa zaidi ya dakika 15.

Hii ni tofauti kwa huyu robot , ndani ya sekunde unajibiwa swali lako.

Makampuni mengi yatawafukuza, kutokana na gharama ya mishahara na kazi zao kutoonekana.

Gharama ya robot wa ChatGPT inaweza isizidi 20 Million , ukilinganisha na kulipa mabilioni ya ela kwa customer care.

Sekta zingine ni waalimu , madereva - hawa wote waachishwa kazi.

KUMBUKA: Dunia ipo kasi sana,
2011 - Smartphone zilikua za kusebu Tanzania . Lakini miaka 12 baadae , yaani leo , kila mtu ana smartphone ( Hadi Mama yangu mzazi )

Gari likijipaki lenyewe , bila ya dereva - Parking Assistant

 
Customer care wa Tanesco, Tigo na Sales executive wa Total energies wote wana ugonjwa wa kutokuwajibika. Hawa watu ukipata tatizo ukawapigia wanakuambia andika email ioneshe kama ni formal complain siju wanakariri wanvyofundishwa kuhudumia mteja. Hivi mteja ana shida aandike email ili ionekane ana file formal complaint kweli.
Hizi fani ni bora akaletwa robot.
 
Customer Care kuwa assisted na robots wala haikuanza leo wala jana ni waay back....

Na kabla ya hapo hizi kazi badala ya kufanywa na raia wa nchi husika ambapo ilikuwa gharama nyingi zilikuwa shipped sehemu kama India kwenye cheap labour...

Ofcourse automation has been coming and will continue eating away jobs lakini care / human touch huku huenda pasipigwe sana hata leo ukipiga simu utapelekwa kwenye mashine kwanza binadamu atakuja mwisho kama haujapata msaada
 
Haujawahi kuisikia ChatGPT?
Ijaribu . Utarudi ukiwa umeshangaa zaidi
Mara ya kwanza nilipoanza kuitumia niliipenda ila sikuona kama inaweza kureplace watu, lakini hii chat gpt version ya 4, ina hadi accuracy ya kiswahili kwa 78% imeanza kunitia hofu.
Aisee kuna kazi nyingi zitapotea. Copy writing, personal assistance, kutuma na kujibu emails, kuandika blog posts na mambo mengi yani itapotea. Sasa wako kwenye training ili bots ziweze kusoma na kuandika lugha mbalimbali hapo ina maana sasa hata simu zitaweza kupokea.
Chat gpt version 4 inafanya hadi kazi baadhi za photoshop tena accurately
 
Back
Top Bottom