CV ya Makamu wa Rais. Vijana/Wasomi acheni kuchunguza chunguza mambo mpeni tu Ushirikiano.

CV ya Makamu wa Rais. Vijana/Wasomi acheni kuchunguza chunguza mambo mpeni tu Ushirikiano.

Unaishi mapori ya wapi?
Ulaya hakuna ulazima ukimaliza sekondari ukimbilie high school
Kwanza wengine huwa wanatafuta kazi wanafanya, huko kazi kila sehemu na kuna kazi za watoto under 18 kama kwenye migahawa ya KFC na McDonalds
siku akiamua kurudi shule anarudi muda anaotaka, sio elimu yenu tia maji ya necta uunge ukale ugali na maharage Alevel.
Hasira za nini? O level kamalizia Tanzania. Toka 98 mpaka 2002?. Na pia najua kuna kuchukua gap year ila ni baada ya kumaliza form six sio four. Na huwa ni one year sio mingi. Alisoma O level ya kawaida. Primary na advance ndo ameonesha kasoma international.
 
Haina shida, alivyofika kule karudia tena, kwani kuna shida ?
Ulaya elimu ya lazima ni mpaka GCSE, sio lazima usome A level au college, hapo vijana wanaamua kufanya kazi kwa muda halafu baadae anaamua kurudi shule, na hata akimaliza Alevel anaweza kukaa hata miaka 5, ndio siku aamue kwenda kusoma Uni, Haina shida kabisa
Maisha ya huku ni tofauti sana
Unaweza kuta mtu kaomea Engineering degree, halafu Masters anasoma Finaace na kufanya kazi benki, au mtasema kaunga unga ?
 
Cv haijaandikwa karudia. Wananchi wanaopngozwa wana haki ya kuhoji kwa staha juu ya viongozi wao. Ndo maana mwanzoni walivyokataa hawezi kuanza shule na 5 years nikasema no, kwa international inawezekana ila kwa serikalini miaka hiyo hapana.
Kama alirudia angeandika. Gape ni refu kwa maisha ya kawaida ya kusoma.
 
Ni hiyo hiyo moja, merton college, ni college ya university of Oxford.
Sio bana

Ndio ipo Merton College ya Oxford, hio ni tofauti na inameremeta iko chini ya Oxford University, kwa vipanga tu

Hii nyingine aliosomea iko London, ni college ya A Level na Vocational studies.
 
Cv haijaandikwa karudia. Wananchi wanaopngozwa wana haki ya kuhoji kwa staha juu ya viongozi wao. Ndo maana mwanzoni walivyokataa hawezi kuanza shule na 5 years nikasema no, kwa international inawezekana ila kwa serikalini miaka hiyo hapana.
Kama alirudia angeandika. Gape ni refu kwa maisha ya kawaida ya kusoma.
wabongo mna vichwa vizito sana
Kwanini aandike karudia ile iweje, ?
Huyu yeye unakuta hata alikuwa hana mawazo ya kurudi, ni vile mbinde ya kuishi ulaya kakumbuka nyumbani ana konekneshi karudi
Hio ilikuwa mipango yake, au wazazi waliiiona ni bora aanze upya kule sababu elimu ya sekondari hapa alisomea ya NECTA huko kigurunyembe, na ingekuwa rahisi zaidi aanze mfumo GCSE tena ili aende nao mpaka vyuo vya huko, kule unatakiwa uwe na GSCE pass ya Maths na English ndio uruhusiwe kuingia University zao.
 
Sio bana

Ndio ipo Merton College ya Oxford, hio ni tofauti na inameremeta iko chini ya Oxford University, kwa vipanga tu

Hii nyingine aliosomea iko London, ni college ya A Level na Vocational studies.
Hapo sawa.
 
Amezaliwa 1983
Ameanza Darasa la kwanza mwaka 1988 akiwa na miaka Mitano (5)
Amemaliza Darasa la saba mwaka 1995 akiwa na miaka 12.
Amesoma Darasa la kwanza mpaka la Saba kwa miaka 8.😨😨😨

Ameanza Secondary mwaka 1996 mpaka 2004 yaani amesoma Form one mpaka Form six kwa miaka 9😨😨😨

Darasa la kwanza mpaka form 16 amesoma kwa miaka 16.😨😨😨

Hii Elimu inawezekanaje kupatikana kwa miaka hii inayotajwa?

Miaka ya 1970-1990 Mwanafunzi anaanza Darasa la kwanza akiwa na miaka kuanzia 7 na kuendelea lakini mwamba alianza na miaka Mitano (5)

Nikisema WanaCcm wanapenda NAMBA lakini hawajui HESABU huwa sikosei.

Taifa linaangamia kwasababu tumekubali kufanywa Wajinga na Watu wachache

Elimu ya kuunga unga.
Elimu mbalimbali
 
Huyu jamaa aliniuzia router ya Smile. Ilikuwa inakula bando balaa
walugaluga na waporipori wakisoma posti yako wataamini kabisa ulimkuta dukani akakuhudumia mkagalalizana bei ukanunua
 
Ndugu mtoa mada,
Ushauri wako wa kutaka vijana na wasomi wampe ushirikiano Makamu wa Rais mteule bila "kuchunguza chunguza" una nia njema ya kuleta utulivu, lakini kiuhalisia unakinzana na misingi mikuu ya elimu, weledi, na uwajibikaji wa kijamii (accountability). Elimu na usomi haviishii kwenye kupokea taarifa tu, bali vina misingi ya kuhoji (critical thinking) ili kujiridhisha na ukweli wa mambo, hasa yanapohusu viongozi wa ngazi za juu kabisa za maamuzi ya nchi.
Kama mdau Komeo Lachuma alivyoichambua hiyo wasifu (CV), kuna maswali ya msingi ya kimahesabu na kiutaratibu yanayojitokeza na ambayo hayawezi kupuuzwa:
  1. Muda wa Elimu ya Msingi: Kama mtu alianza darasa la kwanza mwaka 1988 na kumaliza mwaka 1995, huo ni muda wa miaka minane (8). Katika mfumo wetu wa elimu, darasa la kwanza hadi la saba ni miaka saba (7). Hapa kuna ziada ya mwaka mmoja inayohitaji maelezo—je, alikariri darasa, au kuna makosa ya kiuandishi (clerical error) kwenye CV yake?
  2. Muda wa Elimu ya Sekondari (Kidato cha 1 hadi cha 6): Taarifa inaonesha alianza sekondari mwaka 1996 na kumaliza kidato cha sita mwaka 2004. Huu ni muda wa miaka tisa (9). Mfumo wa elimu wa Tanzania unaruhusu miaka minne ya O-Level na miaka miwili ya A-Level, jumla miaka sita (6). Miaka tisa kwa ngazi hii inaacha maswali mengi ya kiakademifu.
  3. Umri wa Kuanza Shule: Katika muongo wa miaka ya 1980 na 1990, sheria na taratibu za nchi zilikuwa madhubuti kuhusu umri wa kuanza shule (miaka 7). Kuanza shule akiwa na miaka 5 katika kipindi hicho, ingawa si jambo lisilowekana kabisa kwa shule za binafsi za sasa, lilikuwa jambo lisilo la kawaida kabisa kwa mifumo ya shule za serikali za miaka hiyo.
Tunapozungumzia nafasi ya Makamu wa Rais, tunazungumzia mtu ambaye kwa mujibu wa Katiba, ndiye msaidizi mkuu wa Rais na anaweza kuwa Rais wa nchi wakati wowote iwapo kiti kitakuwa wazi. Hatuwezi kuongoza nchi kwa kuangalia nyaraka muhimu kama CV "juu juu".
Kuhitaji ukweli na uwazi kuhusu wasifu wa viongozi wetu si "uchokozi" au kukataa kutoa ushirikiano. Ni haki na wajibu wa kila mwananchi anayelitakia mema taifa lake. Ili vijana na wasomi watoe ushirikiano wa dhati na wenye imani kubwa, ni lazima mamlaka au mhusika anyooshe maelezo ya namba hizi ili kuondoa hisia za uwepo wa "elimu ya kuunga-unga" au wasifu wa kubumba. Viongozi bora huangaziwa kwa uwazi, si kwa kuficha mapungufu
Ngoja waje watetezi watakuambia mambo mngiiii
 
Kwan humu JF hakuna watu ambao wanakutana kwa viongozihata wa chama au serikalini na kuwauliza jamani haya mambo yanayoenda ni Sawa nahis kuna wengine ndgu zao kabisaaa je mkipata nafasi hua munawauliza nni au mnaogopa kisa wengine mnalipiwa Ada maaana sie hata mtu alieko huko serikalini hatuna jamani muwe mnaleta wanasemaje ahata kwa maandishi maannadu hatari sana kweli TANGANYIKA NDIO IMEFIKIA HAPA inatisha
 
Back
Top Bottom