CWT wameishiwa ubunifu, Mei Mosi kuvaa sare inayoendana na ya TLP

Na tatizo mmezidi uchama sanaaa,,, na mwalimu ndo mfanyakazi anayekula bata kuliko nyie wengne in terms of working hours
 
We jamaa unaishi Nchi gani, mbona walimu kibao wenye div 1 na 2 [emoji28][emoji28]
 
Tatizo wabongo mnaushi kwa kukariri [emoji28][emoji28]
 
Dah! Wewe jamaa ni mbishi!! Sasa hao wanafunzi waliopata Div. 1 - 3 mfano kwenye matokeo ya kidato cha nne si wana sifa ya kwenda kidato cha tano? Sasa mwanafunzi anawezaje kuacha kwenda kidato cha tano na kwenda ualimu? Ndiyo maana unakuta walimu wengi wa grade A walipata division four au three za mwisho! Na hawa hufundisha shule za msingi na awali! Na kwa sasa wengi wao wamejiendeleza kielimu na kuwa na diploma, digrii, postgraduate na hata masters katika fani mbalimbali.

Ukija kwa wale waliomaliza kidato cha sita, nitakukatalia mpaka asubuhi! Hakuna chuo kikuu nchini kinacho chukua wanafunzi wenye ufaulu wa division 0 au four, kwenye matokeo ya ACSEE ili kusomea ualimu, au kozi yoyote ile! Vyuo vingi huchukua wanafunzi wenye ufaulu wa kuanzia point tano! Yaani D moja (point 2) na C moja (point 3)! Na hivyo jumla ni points 5! Na hawa wote ni lazima wapate division 1 - 3!! Na huwezi kwenda A level pasipo kuwa na Credit 3!!

Sasa hao walimu waliofeli wanasoma vyuo gani! Au wanafanya kazi kwenye shule zipi? Kafanye utafiti wako leo kwenye shule zote nchini halafu uje uniambie kama yupo mwalimu mwenye diploma au digrii, halafu ana division four au zero kwenye matokeo yake ya kidato cha nne au cha sita!

Siyo vizuri kutumia udhaifu wa serikali kutowajali walimu, na pia baadhi ya walimu walio tokea familia maskini kuamua kusomea hii fani hata kama hawakuipenda! Ili tu kupata ajira ya haraka, na hivyo kuzisaidia familia zao! Kuwanyanyapaa!

Walimu walio wengi katika nchi hii wana elimu ya kutosha sana! Sema tu wengi hawana morali ya kazi kutokana na ujinga unaofanywa na serikali, mfano kuwalipa mishahara midogo, kutowapandisha madaraja yao kwa wakati, kuruhusu hiyo CWT kuwakata 2% kika mwezi, na pasipo na sababu yoyote ile ya msingi, nk.
 
Nchi ambazo waalimu wake hawalalamiki kuhusu mishahara hazizidi 10,, na hao waliweka elimu kipaumbele ila wengine wote hata huyo USA unaemsemea mwalimu analipwa kidogo comparing na unavyofikiri
Sio kweli walimu USA are highly paid !!?
 
wapi nimesema hivyo?
Sasa hao walimu unao waongelea kwamba ni failures ni wa kiwango gani cha elimu? Kuwa specific basi. Kama ni hao wa grade A, kwa sasa wanahesabika! Maana wengi wamejiendeleza!

Isitoshe, bado hawakwenda vyuoni na division 0 (ambayo ndiyo kiwango halisi cha huo ufailure wenyewe), wameingia kwa division four, three, nk! Ambayo kwenye viwango vya ufaulu, ni Pass! Na siyo 'fail'

My problem is that, why are you calling them failures? While it is not true!!!
 
Huyu kiumbe ni mbishi sijawahi kuona! Na hataki kuelewa. Nimejitahidi kumuelimisha, naona hata haelewi! Kiufupi kazi ya ualimu ni ngumu sana ukipata aina hii ya wanafunzi wajuaji (much know)
Kwa u-much know wake ndo ulimfanya apate laana ya walimu ndo hayo matokeo yake dharau kiburi na majivuno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…