Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Musiba aliposema kuwa Tundu Lissu na Freeman Mbowe wanastahili kuuawa, siku chache baadae Tundu Lissu akashambuliwa kwa risasi. Hakuna mamlaka yoyote iliyomhoji. Sio polisi, sio DCI. Hata Waziri wa usalama wa ndani alikaa kimya. Rais naye akakaa kimya.

Juzi gazeti la Tanzanite na Fahari yetu yanayomilikiwa na Musiba na ambayo kimsingi yanalindwa na mamlaka kwa ajili ya kuchafua watu yameripoti kuwa kuna njama zimepangwa za kumuua Musiba. Magazeti hayo ya Musiba yamewataja Wanaharakati, wanasiasa, polisi, wanadiplomasia na watu mashuhuri katika mpango huo wa mauaji. Haraka sana mamlaka zile zile zilizofumbia macho na masikio taarifa za kuuawa Tundu Lissu na Freeman Mbowe zimeanza kuwahoji watuhumiwa katika sakata hilo ambapo tayari Mkurugenzi wa Jamii Forum Bwana Mello ameshahojiwa.

Ndiposa Abdulrahaman Kinana na Yusuf Makamba ambao nao hawajasazwa katika ubatizo wa moto unaotokana na Joka walilolifuga na kulilisha wao wenyewe leo wanahoji tena ni nani aliyeko nyuma ya Musiba?

Nani namuuliza Makamba hivi uliposema Kikwete alibatiza watu kwa maji lakini Magufuli atawabatiza kwa MOTO ulidhani wewe na familia yako mpo salama sana kiasi kwamba ubatizo huu moto usibgewahusu?

Hakuna aliyeko salama na yeyote anayedhani yuko salama huyo ndiye hana usalama hata kidogo. Hili Joka la mdimu likimaliza au kukinahi kula watoto wa majirani huwa lina tabia ya kurudi ndani na kula watoto nyumbani.

Siungi mkono vitendo viovu vya Musiba vya kuchafua mtu yeyote. Lakini pia na ninyi jifunzeni kulaani watu wengine wanapochafuliwa. Mlikaa kimya wengine walipochafuliwa na pengine nanyi mlikuwa sehemu ya kuchafua wengine ndio maana sasa watu wapo kimya ninyi mnapochafuliwa.

The law of Karma is REAL! What goes around comes around.

Acheni kuzunguka mbuyu, Musiba ni Spika tu, yeye ni kipaza sauti. Na anayezungumza kupitia kipaza sauti hicho (Spika) mnamfahamu na mnamjua vema. Onesheni uanaume mumkabili hadharani na kiume. Tusi likitolewa kupitia Spika huwa hatupambani na Spika bali tunapambana na mzungumzaji. Ukiivunja Spika na kumuacha mzungumzaji halisi atatafuta spika/kipaza sauti/forum nyingine na ataendelea kukutukana.

#MwagaPombe2020

Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
nimeipenda hii hashtag #MwagaPombe2020
 
.
20190715_173046.jpeg
 
Yanayoendelea CCM,ni kazi ya Mungu ila kwa akili za kibinadamu si rahisi kuona wala kuelewa.

CCM hii haina tena baraka za mwenyezi Mungu.

Mungu karuhusu Shetani na aunge mkono juhudi!
 
HUYO NDO ACHUMAN NGABANGA!
NA HII NI TAFAKURI BAADA YA HABARI:

Sijui ni utani au vipi, lakini kuna visa vingi vya kuchekesha vinavyowahusu watani zangu wamakonde, na kifuatacho ni kimoja kilichotaka kuhatarisha mbavu zangu 😂 😂 😂 !

Jamaa mmoja alipotea porini na baada ya kutangatanga sana humo porini, jioni, akafika kwenye mji wa wamakonde katikati ya pori na baba mwenye nyumba akamkirimu mgeni wake ipasavyo.

Ulipofika muda wa kulala mwenyeji akamuonesha mgeni chumba cha kulala huku akimtandikia huyo mgeni chini lakini mgeni alipolalamika kwanini anatandikiwa chini mwenyeji wake akamwambia "humu kuna vitanda viwili tu, kimoja nalalia mimi na chemeeji yako na hicho kingine analala mwenyewe Achuman Ngabanga."

Mgeni bado hakuridhika:"Sasa mbona kitanda cha Achuman Ngabanga kikubwa tu na kinatosha kulala watu wawili? naomba tuchangie kitanda na Achumani."

Mwishowe mwenye mji akamruhusu mgeni achangie kitanda na Achuman Ngabanga ambaye mpaka hapo alikuwa hajarudi nyumbani.
Usiku wa manane mgeni akahisi kuna kitu kama mnyama kinambugudhi kitandani na alipoamka akajikuta ana kwa ana na mbwa mkubwa ambaye naye anataka kulala hapo kitandani, na hapo sasa ikawa tena apiga yowe kumuamsha mwenyeji wake na kulalama "huyu mbwa vipi hamjampa mafunzo, mbona anataka kulala na binadamu kitandani?"

Jibu la mwenyeji lilimuacha hoi mgeni:
"HUYO NDO ACHUMAN NGABANGA MWENYEWE AMERUDI, UNAMPUKUCHIA NINI? ....ACHA KUMPUKUCHAPUKUCHA ACHUMAN NGABANGA NAYE ALALE" 😂😂😂


SASA WAZEE WETU KULIALIA KOTE KWANINI TENA? HUYO NDIE GAMBA WA MAGAMBA MWENYE GAMBA LAKE IN ACTION!

NDUKI 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️😂😂😂😂😂😂!



SIGNATURE
 
Ibara ya 18 ndiyo ilikuwa nyuma ya Lissu akapigwa risasi nusu kufa. acheni unafiki. kuna kitu kingine tofauti kipo nyuma ya huyu boya siyo Ibara ya 18.
 
JE, KINACHOMLINDA MUSIBA CHAJULIKANA?




JADILI!

Wewe mkonongo! jibu swali hili mbona ni Musiba peke yake! anaruhusiwa kufuata ibara ya 18? Huoni Ben saanane alivyopotea kwa sababu tu ya kuhoji PHD ya JPM? Huoni ubaya wa msiba anavyosema watakaomsema JPM watafanywa viwete? Seriously unamtetea Musiba? Rubbish thinker hata huko wewe ni mzibua vyoo tu.
 
Back
Top Bottom