Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14


Katiba yetu Ina mwanya. Inaposema kila mtu ni sawa , jiulize mbona Rais hashtakiwi au mbona Rais halipi Kodi?.

Pia kwenye sheria ya tort Kuna kitu kinaitwa punitive damages , yani fidia Kama adhabu.
 

Kwanza muda wa Rufaa ulishapita. Hukumu ilitolewa mwaka 2021 , tarehe 28 oktoba. Inakaribia mwaka mmoja na miezi sita. Sasa baada ya muda kupita Membe ameenda mahakamani kuomba kikazia hukumu Yani execution of decree.

Sasa Hapo, kazi sio ya Membe Bali ya mahakama. Kama Hatalipa ndani ya muda huo mahakama itatumia madalali wake kushikilia Mali zake na baadae kuzipiga Bei, na Kama Deni halitatimia watamkamata na kumfunga jela kwa gharama za Membe.

Mimi naona Membe anataka Musiba awekwe kizuizini mpaka Deni lilipwe.
 
Dunia inaenda kas sana, sasa hakuna namna akamuangukie membe tu na kulia kwa kwikwi huenda membe huruma ikamjia

Nadhani amejaribu hivyo ila Membe amekataa. Unajua alimdharilisha Sana , Tena mbele ya waandishi wa habari.
 
Na mie nimesema huko juu...wapo wengi kama Musiba hapa jamvini na hata ndani ya uzi huu. Kitaeleweka .
Hilo la Musiba kuto enjoy ndio haswa kisasi kilichopita kipimo....ni hisia kali tu dhidi ya binadamu mwenzako.....its a Saddist view.

Lazima ujue huwezi kufungua kesi ya madai kwa member humu Jamii forum labda awe verified user. Unatakiwa kufungua kesi ya madai kwa Jamii forum in general kitu ambacho ni kigumu. Maana Jamii Forum yeye ni social media platform sio mtoa maoni au makala.
 
Katika hiyo team, kuna waliokuwa wanachukia mitusi yake..!! Ni kama alikuwa anamharibia JPM. Walikosa namna ya kufanya kumtuliza.

Nadhani kitendo Cha kumuachia kilimpa kiburi Sana. Ngoja avune alichopanda na majivuno yake. Ila miaka kumi ijayo Musiba atakuwa mtu mzuri Sana.
 

Basi kamshauri afungue kesi ya madai dhidi ya Jamii forum na Facebook au istagram. Maana kwa mtu mmoja mmoja Yale ni maoni, tunaita fair comment ambayo Ni defence.
 
Kusema Mama Janeth naye aje kupata uwakilishi nayo kwa mujibu wa Sheria zetu sio sahihi?

Umenisoma vizuri au na wewe umekurupuka tu?
[/QUOTE]
Sheria yetu ya defamation hairuhusu madai kama hayo .
Sheria yetu kuhusu defamation inamhusu yule mtu directly aliyeumizwa/kushambuliwa ndiye anaweza kudai fidia .
Mama Janeth kisheria hawezi kufungua kesi ya defamation eti kaumizwa Kwa sababu mume wake alishambuliwa .
Kwa Sheria zetu hayo madai hayakubaliki.
Kuhusu kwamba Membe alijiwakilisha yeye mwenyewe mahakamani, inawezekana alitumia mwanasheria kumuwakilisha hilo ni suala lingine.
Ninachosema Sheria inakataa mtu mwingine kulalamika kwamba ameumizwa kutokana na mtu mwingine kutukunwa.
Hata kama Mama Janeth atumie mwanasheria haitakubalika eti mwanasheria awasilishe hoja kwamba namwakilisha mteja wangu ( Mama Janeth) ambaye analalamika kwamba ameumizwa Kwa kitendo cha Mume wake (Magufuli) kutukanwa hivyo naomba fidia
 
Jipe faraja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…