Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Mahakama Kuu ya Tanzania imempa siku 14 za kazi mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wenzake watatu kumlipa Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu, Benard Membe TZS bilioni 9.92 kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vya habari.

View attachment 2588944

Mahakama imetahadharisha deni hilo lilipwe ndani ya muda vinginevyo hatua zaidi zitachukuliwa.

Chanzo: Swahili Times
Wote ni wakatoliki mtajuana wenyewe
 
Yaani ht kwa hili wale walinda legacy bado wanaona nchi ilikuwa salama chini ya Muovu yule
 
Tunaomba haki itendeke kwa waliomchafua Magufuli pia nae alipwe fidia alitukanwa sana mitandaoni
 
Hivi mfano zikauzwa mali zote za Musiba pamoja na za ukoo wake mzima hiyo bilioni 9 itapatikana?
Nimewaza atatoa wapi pesa ndefu kiasi hicho

Na jinsi alivyokuwa na kiburi sijui itakuaje!!, angemfuata Membe falagha wakayaongee kiutu uzima nadhani yangeisha.
 
Watu huwa wanamchukulia poa sana Membe. Namheshimu sana huyu mzee nje ya siasa.
 
Wacha wakomoane, ila kuna ya kujifunza na hayo na yale yanayoendelea humu Jamvini. Ipo siku kitaelweka.

Naona kuna ugaidi wa kimtandao unaondelea kutokana na Taarifa hizi. Naona kumetokea mwanya wa wale waliokuwa na "visongo vya usasi" kuendelea kutoa nyongo.
chochote kilichosababisha mapenzi yake au harakati zake za kashfa, inaonekana kwangu, ni mapenzi sawa na wengi hapa.... wanaoendeleza upotoshaji wa chuki na kukashifu kwa kuzingatia amri/taarifa hii

Kinachoonekana, ingawa ni haki, kinaweza kutafutwa na kutumiwa na wengi ambao wamefikia pahali sawa na Membe.

Muda utasema. Hata hivyo, mahakama hazipaswi kutumiwa kama silaha ya kulipiza kisasi

Ipo siku Ugaidi huu wa mtandaoni utaenda kutolewa ushauri,hukumu, na hata amri za kukabiliana nao.

Pole Mama Janeth.
R.I.P mwamba.
 
Asipokua nayo watamfanya nini? Unakuta hata mali zake chache ziko kwa jina la mkewe
 
Kama ni kweli, basi kuna dosari kubwa kwa hawa majaji wetu na sheria zetu. Watu wote ni sawa. Hivyo ndivyo tunavyoamini. Na katiba yetu ya nchi inasema hivyo. Vitabu vitakatifu vinasema hivyo. Hivyo thamani ya Membe na thamani yangu na wewe iko sawa. Hivi ni kweli kwamba mimi na wewe tukichafuliwa kama alivyochafuliwa Membe, tutalipwa hizo Tsh billioni 9 kila mmoja kweli?
 
Kwenye sheria ya tort Kuna kitu kinaitwa punitive damages. Ni amri ya mahakama ya kulipa fidia kubwa Kama adhabu ya kutokurudia Jambo Kama Hilo Tena mbeleni.
Hakika

hoja yangu ni kuwa mahakama isitumike kama silaha. Hukumu ilishatolewa ameamriwa kulipa. Hajalipa, Je kuna muda maalum aliyopewa katika hukumu ya awali ya amri hii kutokea?

Kama alipewa muda, sina la nyongeza, ila kama hakupewa muda maalum, naona sasa imefikia pahali Membe anataka kumkomoa.Kwani sioni membe akiwa ana njaa ya hiyo pesa kiasi cha kupeleka/kuomba mahakama kutoa siku kumi na nne ilipwe.

keep in mind, mie sio mwanasheria. ila naona Cyprian anauwezo wa kupinga au kukatia rufaa amri hii
 
Pole sana kaka. Kwa ule ujinga wake, Musiba hatakiwi kabisa kuinjoi hewa hii nzuri ili iwe fundisho kwa wengine. Kuchafuana/kudhalilisha watu kuwe na kipimo
 
Pole sana kaka. Kwa ule ujinga wake, Musia hatakiwi kabisa kuinjoi hewa hii nzuri ili iwe fundisho kwawengine. Kuchafuana/kudhalilisha watu kuwe na kipimo
Na mie nimesema huko juu...wapo wengi kama Musiba hapa jamvini na hata ndani ya uzi huu. Kitaeleweka .
Hilo la Musiba kuto enjoy ndio haswa kisasi kilichopita kipimo....ni hisia kali tu dhidi ya binadamu mwenzako.....its a Saddist view.
 
Back
Top Bottom