Cyril Ramaphosa: China haina lengo la kuiingiza Afrika kwenye mtego wa madeni

Cyril Ramaphosa: China haina lengo la kuiingiza Afrika kwenye mtego wa madeni

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa hivi karibuni alidokeza kuwa hakubaliani na dhana ya kwamba uwekezaji wa Taifa la China barani Afrika unapelekea bara hili katika "mtego wa madeni,"

Ramaphosa alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa kilele cha China na Afrika huko Beijing, ambapo wajumbe kutoka zaidi ya mataifa 50 ya Afrika walikusanyika wiki hii.

"Sikubaliani na dhana ya kwamba China (inapowekeza) ina nia ya kuhakikisha kwamba nchi hizo mwisho wake zinaishia katika mtego wa deni au katika mgogoro wa deni,"

Ramaphosa alisema hayo, alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu ahadi ya China kwenye mkutano wa kutoa $51 bilioni katika ufadhili mpya kwa Afrika.

Source: Reuters
 
Ramaphosa ni raisi wa hovyo sana, na ni kama dish lilishayumba. Anajua fika kilichokuwa kinatokea wala sio mbali, ila kwa jirani yake tu hapo- Zambia. Mikopo ya China ni hatari kama nchi isipojipanga vizuri.
 
Usd bil 51 miaka 3 hakuna hela hapo rail yetu tu n usd bil 10 sjui tuna maviongoz ya aina gan tuna majitu majinga majinga sn sn aisee. Yan hii ndo hela wachina wamewaitia viongoz wote wa afrika seriously kweli hv viongoz wa afrika wameshndwa wao kuitana na kutafuta namna kuendesha uchumi wa nchi zetu paspo kutegemea hao wanyonyaji au kwa vile mikataba yao inawanufaisha viongoz na family zao tu.
 
Kila mtu kaenda na proposal yake
 
Back
Top Bottom