D Voice amebakisha siku chache kutambulishwa WCB, dogo ameshaula tayari

D Voice amebakisha siku chache kutambulishwa WCB, dogo ameshaula tayari

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Hayawi hayawi sasa yamekuwa.

Hatimaye ile ndoto ya muda mrefu ya msanii wa singeli kutokea Temeke ukipenda muite London boy D voice jinii inakaribia kutimia siku chache zijazo.

Msanii D voice yupo wasafi muda mrefu sana, kula yake, vaa yake mpaka sehemu anapoishi yote ipo chini ya wasafi.

D voice ameshawahi kutamba na ngoma kadhaa kama vile kuachana Sh ngapi aliyomshirikisha Barnaba Classic, Mchanganyiko aliyomshirikisha Baddest.

Pia aliwahi kutamba na wimbo wa madanga ya mke wangu alioshirikishwa na Meja Kunta.

D Voice aliachana na management yake ya awali mwishoni mwa mwaka jana hivyo Wasafi wakaona wasiache hiki kipaji kipotee hivi hivi wakaamua kumchukua na mpaka sasa yupo mikononi mwao anasuburiwa tu kutambulishwa rasmi hiyo tarehe 16.

Ukimya wake D Voice utakuwa na kishindo kikuu.

Kila la heri kwake ila asianze kuwavimbia wenzake awe kama mwanzo na tabia ile ile ya kuwaheshimu wenzake walimtangulia kwenye muziki wa singeli.


-1805718260.jpg
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa .

Hatimaye ile ndoto ya muda mrefu ya msanii wa singeli kutokea temeke ukipenda muite London boy D voice jinii inakaribia kutimia siku chache zijazo...
Kumbe huyu dogo ndo alieimba madanga ya mke wangu,, aisee lile songi ni Kali ila maudui yake ni ya kishenzi sana.
 
D Voice anajua hatari.
D Voice ana nyimbo kibao kama
1. Jiangalie, kashirikishwa na Nay wa Mitego
2. Nikwambie
3. Ratifa
4. Itikeli
5. Ex wangu
7. Madanga ya Mke wangu kashirikishwa na Meja Kunta
8. Kuachana Shilingi Ngapi, kashirikishwa na Barnaba

#YNWA
Kikubwa nidhamu tu.

Atafika mbali akiwa na nidhamu.
 
Back
Top Bottom