Dada aliyekutwa na Corona Tanzania siyo bure

Watu tusimlaum tu huyo mgonjwa. Iko hivi nchi za wenzetu watu wakitua tu airport Cha kwanza wanawekwa isolation siku 14 sisi tz tunawapitisha tu je ni wangapi wameingia nchini na wako mtaani wanadhurura tu, hivi ni kwa sababu hatujali au? Wenzetu walishapiga marufuku ndege kuingia Wala kutoka sisi hakuna hivi sisi na marekani ni wapi wako vizuri kitabibu. Cha kusikitisha watoto wetu wapo mashuleni Kama unavyojua wamejazanaadarasani bila effective measures. Jamani hivi Tanzania ni kweli tumechukua tahadhari?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1390616

Nimejaribu kuwaza na kuchambua jinsi huyu Dada aliyebainika kuwa na virusi vya Corona, nimejiuliza maswali mengi sana.

Baada ya kufuatilia kwa kina nimeambiwa jina lake ni Isabela Mwampamba, umri wake ni miaka 46.

Simulizi ya safari yake ndio jambo kubwa limenifanya niwaze sana na kujiuliza maswali ambayo sisi Watanzania tunapaswa kuwa makini, na kujiridhisha kama gonjwa hili limeingia kwa bahati mbaya ama mpango maalum? Kwenye hili sitanii hata kidogo.

Tunaambiwa huyu Dada aliondoka nchini Machi 3, 2020 kwenda Rwanda. Hatuambiwi alikwenda Rwanda kufanya nini?

Baada ya kukaa Rwanda siku 2 Machi 5, 2020 aliondoka kwenda Brussels Ubelgiji, akiwa huko alikwenda Stockholm Sweden, akiwa huko alifikia nyumba iliyokuwa na mgonjwa wa Corona.

Akaondoka hapo kwenda Norway ambako pia amekaa siku kadhaa hadi Machi 14, 2020 alipoondoka huko kurejea nchini kwa kupitia tena Rwanda na kisha akaingia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA.

Simulizi ya huyu Dada inasema baada ya hapo hakwenda nyumbani Arusha bali aliamua kwenda kulala hotelini kwa madai alikuwa ameanza kujishtukia.

Akiwa hotelini alijiona hayupo sawa ndipo akaenda Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru ambako baada ya sampuli kupelekwa Dar es Salaam ndipo ikathibitika kuwa ana virusi vya Corona hiyo jana Machi 15, 2020.

Kinachonisumbua mimi, mzunguko wote huu hatuelezwi alikuwa anafanya shughuli gani? Najiuliza hivyo kwa jinsi Ulaya ilivyotikiswa na Corona unawezaje kwenda huko ukaishi kwenye nyumba yenye mgonjwa wa Corona na bado ukarejea nchini kwako ambako umeambiwa ugonjwa haujaingia bila hata kusema hayo yote ili tahadhari ichukuliwe mara baada ya kushuka kwenye ndege?

Ni bahati mbaya kweli au ni mpango maalum ulipangwa ili Tanzania nayo itangazwe duniani kuwa imepatwa na Corona?

Najiuliza hivi, ni bahati mbaya kweli kwamba huyu Dada alianzia safari yake Rwanda?

Najiuliza ni bahati mbaya kweli kwa huyu Dada kwenda kuumwaga upupu Kilimanjaro na Arusha kwenye kiini cha utalii wa nchi yetu?

Hivi ni bahati mbaya kweli mtu atoke safari aende kujipiga quarantine hotelini ambako kuna muingiliano wa watu wengi? Kwa nini hakwenda nyumbani kwake na kuwaambia jamaa zake waondoke au atengewe chumba chake kama ilivyokuwa huko safarini Ulaya alikofikia kukiwa na mgonjwa wa Corona?

Nimejiuliza zaidi kwamba labda kwa kutokuwa na mgonjwa wa Corona kulionewa donge na hivyo ikatengenezwa namna ya kutuweka kundi moja?

Kwa mawazo haya, nakumbuka jambo moja tu, Watanzania tunapaswa kuwa makini kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa kuwa ni janga la dunia basi nasi tuungane na dunia kujihadhari na Corona. Tuepuke mikusanyiko isiyo ya lazima, tuepuke kugusana, tuepuke kubusiana, tunawe mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na tutumie viua vijidudu yaani sanitizers.

Kama sio lazima tuache safari hata kutembeleana nyumba kwa nyumba, tukae ndani tutulie. Tuwakinge Wazee na watoto wetu sana kwa sababu hawa ndio wameonekana kupatwa na madhara makubwa ya ugonjwa huu ambayo ni kifo.

Inaelezwa mpaka sasa Corona imesababisha vifo zaidi ya watu 5,000 na watu zaidi ya 150,000 wameugua. Hili ni balaa kubwa, tusichukulie poa hata kidogo.

Lakini pia ukijijua umeambukizwa tafadhari usiambukize wengine, hayo ni mauaji. Nenda Hospitali wataalamu watajua cha kufanya.

Ni hayo tu lakini kwa kweli imeniuma ugonjwa huu kuingia nchini mwetu kwa mtindo huu.

Usiku mwema.

Jotham Mugishagwe Jr.
Ilala, Dar es Salaam.
Machi 15, 2020.
Mkuu umejiuliza maswali mengi sana, labda na mimi nikuongezee swali moja tu, una uhakika gani kuwa hiyo story ya safari yake ni kweli? Vp kama story imetungwa? Anyway inatafakarisha sana

Swali jingine kwa nn hakupima huko kote amezunguka na amekaa na mgomjwa yani asipime kote hukooo aje kupima TZ? Ni kama mkakati rasmi wa kutuangamiza waanze kumchek vzur huyo.mama isijekuwa kapewa pewa aueneze makusudi.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu unamuandiko mzuri na kuchora pia😜
Ahaaah ahaaah mkuu wewe. Points zote hizo nzuri alizomwaga hapo hukuziona, wewe umeona mwandiko wake mzuri na michoro tu? Ni kweli lakini!!
 
Nasikia Paula Paul mpaka leo kajifungia stoo ili kukwepa maambukizi. Kumbe ni mafua tu? Mafua dawa yake ni kula kiporo cha wali na maharage ushushie na K Vant chupa ndogo mbili.
Sio stoo. Ni ndani hamna kutoka.
Kupika kula na kulala. Mgeni akija anapokelewa kwa kuchunguliwa dirishani aseme shida yake huko huko nje.
 
Hahaha ndio maana sijamuona siku mbili tatu. Bora lakini ajifungie tu asije akaumwa mafua nitamhurumia sana.
Nipo busy na Dostoevsky's Notes from Underground baada ya kumaliza Victor Frankl's Man's Search For Meaning.
Nalala nacho, naamka nacho napika nacho hata muda wa kuja huku unakuwa mfinyu.
 
..
BF30FD13-4F4E-46A9-BFBE-13973FA72719.jpeg
AAB1F127-A8C6-4C35-A07E-CCAC87A90B0F.jpeg
 
Mimi bado nawaza kuhusiana na huyu mtu wa kwanza kukutwa na coronavirus nchini.

1. Je, wakati yupo Ubelgiji, alifahamu kuwa anaishi na mtu ambaye ana coronavirus, alifaham haya kabla yupo huko?

2. Ni kwanini aliamua kujiweka lockdown hotelini. Je, alijifahamu kama anaweza kuwa navyo?

3. Wakati anasema hakupenda kwenda nyumbani kwake maana angeambukiza familia yake. Je, alifikiria pia familia za wenzake tukianzia yule dereva aliyembeba pale KIA?

4. Na je, ni biashara gani hiyo muhimu iliyomfanya asafiri mwezi March tena kwenda bara la Ulaya ambapo virusi ndio vilitapakaa tukiachana na China?

5. ....
 
Back
Top Bottom