Dada aliyekutwa na Corona Tanzania siyo bure

Dada aliyekutwa na Corona Tanzania siyo bure

View attachment 1390616

Nimejaribu kuwaza na kuchambua jinsi huyu Dada aliyebainika kuwa na virusi vya Corona, nimejiuliza maswali mengi sana.

Baada ya kufuatilia kwa kina nimeambiwa jina lake ni Isabela Mwampamba, umri wake ni miaka 46.

Simulizi ya safari yake ndio jambo kubwa limenifanya niwaze sana na kujiuliza maswali ambayo sisi Watanzania tunapaswa kuwa makini, na kujiridhisha kama gonjwa hili limeingia kwa bahati mbaya ama mpango maalum? Kwenye hili sitanii hata kidogo.

Tunaambiwa huyu Dada aliondoka nchini Machi 3, 2020 kwenda Rwanda. Hatuambiwi alikwenda Rwanda kufanya nini?

Baada ya kukaa Rwanda siku 2 Machi 5, 2020 aliondoka kwenda Brussels Ubelgiji, akiwa huko alikwenda Stockholm Sweden, akiwa huko alifikia nyumba iliyokuwa na mgonjwa wa Corona.

Akaondoka hapo kwenda Norway ambako pia amekaa siku kadhaa hadi Machi 14, 2020 alipoondoka huko kurejea nchini kwa kupitia tena Rwanda na kisha akaingia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA.

Simulizi ya huyu Dada inasema baada ya hapo hakwenda nyumbani Arusha bali aliamua kwenda kulala hotelini kwa madai alikuwa ameanza kujishtukia.

Akiwa hotelini alijiona hayupo sawa ndipo akaenda Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru ambako baada ya sampuli kupelekwa Dar es Salaam ndipo ikathibitika kuwa ana virusi vya Corona hiyo jana Machi 15, 2020.

Kinachonisumbua mimi, mzunguko wote huu hatuelezwi alikuwa anafanya shughuli gani? Najiuliza hivyo kwa jinsi Ulaya ilivyotikiswa na Corona unawezaje kwenda huko ukaishi kwenye nyumba yenye mgonjwa wa Corona na bado ukarejea nchini kwako ambako umeambiwa ugonjwa haujaingia bila hata kusema hayo yote ili tahadhari ichukuliwe mara baada ya kushuka kwenye ndege?

Ni bahati mbaya kweli au ni mpango maalum ulipangwa ili Tanzania nayo itangazwe duniani kuwa imepatwa na Corona?

Najiuliza hivi, ni bahati mbaya kweli kwamba huyu Dada alianzia safari yake Rwanda?

Najiuliza ni bahati mbaya kweli kwa huyu Dada kwenda kuumwaga upupu Kilimanjaro na Arusha kwenye kiini cha utalii wa nchi yetu?

Hivi ni bahati mbaya kweli mtu atoke safari aende kujipiga quarantine hotelini ambako kuna muingiliano wa watu wengi? Kwa nini hakwenda nyumbani kwake na kuwaambia jamaa zake waondoke au atengewe chumba chake kama ilivyokuwa huko safarini Ulaya alikofikia kukiwa na mgonjwa wa Corona?

Nimejiuliza zaidi kwamba labda kwa kutokuwa na mgonjwa wa Corona kulionewa donge na hivyo ikatengenezwa namna ya kutuweka kundi moja?

Kwa mawazo haya, nakumbuka jambo moja tu, Watanzania tunapaswa kuwa makini kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa kuwa ni janga la dunia basi nasi tuungane na dunia kujihadhari na Corona. Tuepuke mikusanyiko isiyo ya lazima, tuepuke kugusana, tuepuke kubusiana, tunawe mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na tutumie viua vijidudu yaani sanitizers.

Kama sio lazima tuache safari hata kutembeleana nyumba kwa nyumba, tukae ndani tutulie. Tuwakinge Wazee na watoto wetu sana kwa sababu hawa ndio wameonekana kupatwa na madhara makubwa ya ugonjwa huu ambayo ni kifo.

Inaelezwa mpaka sasa Corona imesababisha vifo zaidi ya watu 5,000 na watu zaidi ya 150,000 wameugua. Hili ni balaa kubwa, tusichukulie poa hata kidogo.

Lakini pia ukijijua umeambukizwa tafadhari usiambukize wengine, hayo ni mauaji. Nenda Hospitali wataalamu watajua cha kufanya.

Ni hayo tu lakini kwa kweli imeniuma ugonjwa huu kuingia nchini mwetu kwa mtindo huu.

Usiku mwema.

Jotham Mugishagwe Jr.
Ilala, Dar es Salaam.
Machi 15, 2020.
Kweli, inafikirisha Mkuu.
Ukichanganya na Utamaduni wetu wa kupenda kusalimiana kwa kushikana mikono, basi unachoka kabisa....[emoji856][emoji856][emoji856]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mgonjwa kapita airport , kapimwa lakini hakugundulika mpaka alipoamua kujitenga mwenyewe hotelini.

Hii ni hatar sana,wageni wangapi washaingia nchini na hawajagundulika kuwa na maambukizi,huenda ni vifaa duni ,

Inakuaje Sampuli za mgonjwa zisafirishwe mpaka Dar es salaam kwa vipimo,ina maana hatuna maabara za kutosha tena za kisasa kuweza kugundua magonjwa kama haya.

Hii ni hatari sana tuchukue hatua,pata taswira Daladala ,Treni na mikusanyiko mbali mbali Mashuleni ,vyuoni ,Makanisani,Misikitini,Sokoni nk jinsi watu wanavyojazana tutaepuka kweli maambukizi mapya.
 
Hakika story yake inatia mashaka sana. Mamlaka husika zinapaswa kulichunguza hili kwa umakini zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata waliompima wachunguzwe au vipimo vyenyewe ndo tatizo iweje mtu ambaye yeye mwenyewe amejihisi ni Mgonjwa vipimo visibaini kitu? Au alihonga wapimaji ili akajitenge eneo lenye hadhi aliyotaka yeye? na hawa Rwanda ni Rafiki zetu kweli wa kufa na kuzikakana?
 
Huyo alikuwa anajua, Na alikuwa anafanya Kwa maelekezo, hivyo asingefanya kinyume cha maelekezo, angekuwa mstaarabu angeeleza pale uwanja wa ndege lkn alitaka atomize maelekezo ya Kazi yke.
Huwa wanafanya Kwa maelekezo maana wanakuwa wanalipwa .
Halafu alienda alikokwenda bwana yulee
 
Nashangaa mnaosambaza picha za mgonjwa sijui jf ili mnalichukuliaje? Uyu mama ni mfanya bihashara mwaka jana nimekutana naye Sweden akiwa katika arakati zake za kutafuta marafiki ikizingatiwa shule yake nishule ya gharama kubwa ila yeye utoza karo ndogo sehemu kubwa ya karo ulipwa na wafadhili.

Nawashangaa kwanini msipige kelele Waziri mwenye dhamana asiondoke maana alituhakikishia kuwa mipaka yetu iko salama lakini hataki kusema kama hawana vifaa kabisa.

Niwaombe ndugu zangu kwa pamoja tufuate njia wanazotumia wenzetu kukabiliana na ugonjwa huu hatari niwaondoe wasiwasi kuwa dawa za ugonjwa zipo na wengi wanapona kwa dawa hizo ambazo zinapatikana katika maeneo mengi nchini.

Kule ilipoanzia China [emoji630] tayari wameidhibiti kwa kutumia vitunguu swahumu, machungwa, limao na maji ya moto.

Ombi jingine tusiwatishe watu wakafa kwa hofu kabla ya ugonjwa wenyewe. Kumbuka Africa kuna mafua ya kawaida kutokana na mazingira kama vumbi, hali ya hewa nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mgonjwa wa corona aliepona kabisaa??
Soma hizi takwimu
ETS0bPhXkAIGidx.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Narudia kusema tena waafrika kaeni kwa amani huu ugonjwa ni kwa ajili ya mtu mweupe sisi Nature ya miili yetu hairuhusu ugonjwa kama huu....

Arusha tunawakilisha tiba mbadala amna ku panic
 
Nashangaa mnaosambaza picha za mgonjwa sijui jf ili mnalichukuliaje? Uyu mama ni mfanya bihashara mwaka jana nimekutana naye Sweden akiwa katika arakati zake za kutafuta marafiki ikizingatiwa shule yake nishule ya gharama kubwa ila yeye utoza karo ndogo sehemu kubwa ya karo ulipwa na wafadhili.

Nawashangaa kwanini msipige kelele Waziri mwenye dhamana asiondoke maana alituhakikishia kuwa mipaka yetu iko salama lakini hataki kusema kama hawana vifaa kabisa.

Niwaombe ndugu zangu kwa pamoja tufuate njia wanazotumia wenzetu kukabiliana na ugonjwa huu hatari niwaondoe wasiwasi kuwa dawa za ugonjwa zipo na wengi wanapona kwa dawa hizo ambazo zinapatikana katika maeneo mengi nchini.

Kule ilipoanzia China [emoji630] tayari wameidhibiti kwa kutumia vitunguu swahumu, machungwa, limao na maji ya moto.

Ombi jingine tusiwatishe watu wakafa kwa hofu kabla ya ugonjwa wenyewe. Kumbuka Africa kuna mafua ya kawaida kutokana na mazingira kama vumbi, hali ya hewa nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
[/quoted]acha upumbavu mkuu ada 1m na nusu afu useme anatoza ada kidogo huyo alikuwa na mission zake nyingine Europe




never die with flu😷😷😷😷
 
Katoka nje ya nchi kafika hapa dar lets say kapanda Uber.kamwambukiza dereva abiria tuseme 10 watakaopanda Uber hiyo.

Au katumia gari ya nyumbani.amekuja dereva kumpokea dereva yule ataenda ambukiza walioko kwake.

Na yeye ataambukiza walioko kwake.kama ana watoto wanasoma shule wataambukiza wanafunzi wenzao nao wataenda ambukiza wazazi wao nao wataenda ambukiza wafanyakazi wenzao na wataenda ambukiza watoto wao nyumbani nao wataenda ambukiza wanafunzi wenzao shule,nao wataenda ambukiza wazazazi wao....mzunguko wa maambukizi unaendelea.

Kama aliyetoka nje ya nchi alimwambukiza house girl naye ataenda mwambukiza muuzaji dukani au gengeni naye ataenda ambukiza wa nyumbani kwao nao wataambukiza wenzao na watoto wao nao wataenda ambukiza wanafunzi wenzao n.k

Usije ukadhani wewe upo salama.ujue daladala ,train mwendo kasi,uber,boda na bajaji tayari zinaambukiza Corona watu muda huu.

Usibishe.anza kujikinga.wakati wa kujilinda sasa na kidhaa dhaa.
Mgawanyiko uko hivyo
e38d982aa67a4fc2bce23689105c9b8c.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni mtanzania au? Mbona slizulula sana ana biashara gani?
Mzururaji tu we unajua kabisa mwenyeji wako anacorona afu unakubali kuingia ndani kwake nakuishi 2. Kwann alipogundua kuwa ameishi nyumba yenye mgonjwa kwanini asiende Hospital hukohuko achungunguzwe kabla haja safiri kuja Africa mi na muona pumbavu tu huyo dada

From Timbuktu
 
Hivi ni bahati mbaya kweli mtu atoke safari aende kujipiga quarantine hotelini
Ndugu Mtoa mada; Usipate Hofu; Huyu dada ni Jirani yangu Arusha, (Njiro Corona, Block....) ndipo anapoishi; Lakini pia tumekuwa naye sana Huku Ughaibuni mara nyingi tuu;
Ana Shule zake, Huwa most of time anafanya machangizo kwa ajili ya Shule hizo. Kwenye Trip Yake nashangaa Hajapanda France and Switzerland huko ni mara nyingi huwa anaenda kwa ajili ya Machangizo hayo.

Hivyo Hata kama ni kweli alikuwa ana nia Mbaya; Lakini kiukweli huwa na utaratibu wa kusafiri kutafuta wadhamini wapya na kufanya Presentation zake kwa ajili ya kurudisha mrejesho kwa wadhamini wake. Hivyo Kwa kadiri ya imani yangu sidhani kama alifanya safari zake kwa intention ya Ku-spread.
 
Back
Top Bottom