Dada aliyekutwa na Corona Tanzania siyo bure

Dada aliyekutwa na Corona Tanzania siyo bure

dubu,
Mugishagwe unajiuliza maswali mepesi halafu unatushawishi tuone ni magumu!?

Watanzania tupewe mabomu ya machozi kwa wingi ili tuukabili huu ugonjwa kwa mbinu za kivita mfano kule segerea.
 
Mwisho amemalizia kwa kusema mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu. Mambo yaliyowekwa rehani na tamko la waziri ni mikusanyiko ya kisiasa na uchaguzi mkuu 2020.
 
Hakuna cha mpango wala nini yani eti tuonewe gere kisa hakuna maambukizi mbona nchi nyingi hazina maambukizi kwanini sisi ndo yawepo na nchi ambazo maambukizi yameonekana kama kenya na Rwanda nazo zimeonewa gere.

Sijui mtoa mada umewazaje aisee nchi imeruusu wageni kuingia na watu kutoka afu unashangaa mtu kuingia akiwa na maambuzi eti yamkini katumwa hilo sio sahihi ata kidogo na maelezo yake yule mama anasema alipokua ubelgiji mume wa mwenye nyumba ndo alikua na maambukizi kwahiyo ana hofu kwamba hapo ndipo alipopatia kwa maana hiyo aliondoka nchini salama akaend tembelea izo nchi nyingine salama ila pale alipoondokea ubelgiji anahisi ndo aliuvaa.

Na mtoa mada uache kutisha watu kua huyu mgonjwa katengenezwa ili kuleta virusi nchini huyu ni mtanzania mwenzetu alierudi nyumbani kuungana na familia yake na kwa upande wangu kwenda hotelini ni sahihi zaidi kuliko angerudi nyumbani kwasababu hizi
kama zilivo desturi za watanzania wengi kusalimiana na kujuliana hali ni jambo la kawaida,kupokea mizigo hasa kwa wanetu pale mtu mzima atokapo safari ndio ustaarabu wetu nadhani nyumbani angeambukiza wengi ambao wangeueneza kwa kasi zaid ni rahisi sana hotelini kutogusa chochote ukawa unatoa maelekez ti kwa wahudumu na ukafanyiwa sio rahis kuwazuia wanao kukulaki pale ufikapo nyumbani
Pia kuna vingi vya kushare ukiwa nyumbani tofaut na hotelini kama asingejihisi mapema basi eneo lake lingekua hatarini zaini

Halafu kuna watu wanamshambulia huyu mama badala ya kumpongeza nadhani kuna waathirika wengi tu wamepita kwenye vizuiz na wana maambukizi na hawajajistukia ilhali labda kuna wengine washaanz kuona dalili lakini huyu mama akasema hapana wacha nijitenge keanza nione na kweli akajifanyia process mwenyewe mpaka sasa hata wewe unajua kuna mgonjwa wa corona na hizo ni jitihada binafsi tu.

Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mgonjwa wetu pamoja na kuendelea kupata nafuu anaweza kutusaidia habari muhimu sana.

Naomba wakubwa na wahusika wote wasimchukulie raia mwenzetu kama mwathirika tu wa ugonjwa. Jicho la tatu la nne hata la tano litumike. Dunia ina mambo mengi hii.

Sina uwezo wala mamlaka lakini ningefuatilia historia ya safari zake zote, uwezeshaji, sababu, kiini na msukumo hasa kipindi hili tete.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi namuona km mstaarab hv. Angekua mwingne wa roho mbaya asingeenda hata hotelini angeenda kushinda club tu akawaachia upupu huko ila yeye aliamua kwenda kujiweka hotelin walau ana kabusara. Kumbuka vipimo vya mwanzo vilidunda ila hakujiamini.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
View attachment 1390616

Nimejaribu kuwaza na kuchambua jinsi huyu Dada aliyebainika kuwa na virusi vya Corona, nimejiuliza maswali mengi sana.

Baada ya kufuatilia kwa kina nimeambiwa jina lake ni Isabela Mwampamba, umri wake ni miaka 46.

Simulizi ya safari yake ndio jambo kubwa limenifanya niwaze sana na kujiuliza maswali ambayo sisi Watanzania tunapaswa kuwa makini, na kujiridhisha kama gonjwa hili limeingia kwa bahati mbaya ama mpango maalum? Kwenye hili sitanii hata kidogo.

Tunaambiwa huyu Dada aliondoka nchini Machi 3, 2020 kwenda Rwanda. Hatuambiwi alikwenda Rwanda kufanya nini?

Baada ya kukaa Rwanda siku 2 Machi 5, 2020 aliondoka kwenda Brussels Ubelgiji, akiwa huko alikwenda Stockholm Sweden, akiwa huko alifikia nyumba iliyokuwa na mgonjwa wa Corona.

Akaondoka hapo kwenda Norway ambako pia amekaa siku kadhaa hadi Machi 14, 2020 alipoondoka huko kurejea nchini kwa kupitia tena Rwanda na kisha akaingia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA.

Simulizi ya huyu Dada inasema baada ya hapo hakwenda nyumbani Arusha bali aliamua kwenda kulala hotelini kwa madai alikuwa ameanza kujishtukia.

Akiwa hotelini alijiona hayupo sawa ndipo akaenda Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru ambako baada ya sampuli kupelekwa Dar es Salaam ndipo ikathibitika kuwa ana virusi vya Corona hiyo jana Machi 15, 2020.

Kinachonisumbua mimi, mzunguko wote huu hatuelezwi alikuwa anafanya shughuli gani? Najiuliza hivyo kwa jinsi Ulaya ilivyotikiswa na Corona unawezaje kwenda huko ukaishi kwenye nyumba yenye mgonjwa wa Corona na bado ukarejea nchini kwako ambako umeambiwa ugonjwa haujaingia bila hata kusema hayo yote ili tahadhari ichukuliwe mara baada ya kushuka kwenye ndege?

Ni bahati mbaya kweli au ni mpango maalum ulipangwa ili Tanzania nayo itangazwe duniani kuwa imepatwa na Corona?

Najiuliza hivi, ni bahati mbaya kweli kwamba huyu Dada alianzia safari yake Rwanda?

Najiuliza ni bahati mbaya kweli kwa huyu Dada kwenda kuumwaga upupu Kilimanjaro na Arusha kwenye kiini cha utalii wa nchi yetu?

Hivi ni bahati mbaya kweli mtu atoke safari aende kujipiga quarantine hotelini ambako kuna muingiliano wa watu wengi? Kwa nini hakwenda nyumbani kwake na kuwaambia jamaa zake waondoke au atengewe chumba chake kama ilivyokuwa huko safarini Ulaya alikofikia kukiwa na mgonjwa wa Corona?

Nimejiuliza zaidi kwamba labda kwa kutokuwa na mgonjwa wa Corona kulionewa donge na hivyo ikatengenezwa namna ya kutuweka kundi moja?

Kwa mawazo haya, nakumbuka jambo moja tu, Watanzania tunapaswa kuwa makini kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa kuwa ni janga la dunia basi nasi tuungane na dunia kujihadhari na Corona. Tuepuke mikusanyiko isiyo ya lazima, tuepuke kugusana, tuepuke kubusiana, tunawe mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na tutumie viua vijidudu yaani sanitizers.

Kama sio lazima tuache safari hata kutembeleana nyumba kwa nyumba, tukae ndani tutulie. Tuwakinge Wazee na watoto wetu sana kwa sababu hawa ndio wameonekana kupatwa na madhara makubwa ya ugonjwa huu ambayo ni kifo.

Inaelezwa mpaka sasa Corona imesababisha vifo zaidi ya watu 5,000 na watu zaidi ya 150,000 wameugua. Hili ni balaa kubwa, tusichukulie poa hata kidogo.

Lakini pia ukijijua umeambukizwa tafadhari usiambukize wengine, hayo ni mauaji. Nenda Hospitali wataalamu watajua cha kufanya.

Ni hayo tu lakini kwa kweli imeniuma ugonjwa huu kuingia nchini mwetu kwa mtindo huu.

Usiku mwema.

Jotham Mugishagwe Jr.
Ilala, Dar es Salaam.
Machi 15, 2020.
Mzee umeona mbari sana. Hili nijambo fikiriki, lakini mm imenifanya nifikiri mbere zaidi!
Nimda Sasa Kwa waziri Na naibu waziri wake wakae pembeni!
Sababu Ni hii...
Waziri wa afya alisema wamefunga mitambo sehem zote nyeti kuwapima wageni wanao ingia nchini vikiwemo viwanja vya ndege! Nawalisema Mgeni akipimwa lazima awekwe kizuioni kusubiri majibu ya Vipimo vyake
Swari nikwamba walimpima pale airport ? Namajibu yakaonyesha kuwa hana virusi ! Je tuamini kuwa Vipimo vyao nifeki?au having uwezo wakuona Mara moja? Nakama havina uwezo huo kwanini wavitumie kinyume Na uwezo wake?
Waziri Na naibu wake nadhani nimda wakuwajibika maana nimeona wamefrahia kupewa 500ml. Za gharama za gonjwa hili.
Mi nadhani Serikari iliangalie hili Kwa nguvu zote!
Itume watu wake makini kuchunguza hili jambo japo ugonjwa huu tayari upon.
Waziri hawezi kutupa tahadhari akichekacheka Na mizaha kibao eti tayari waziri mpango ametupa 500ml.
Huku unasema tusipanic.
Kwenye kufa! Hili hapana. Cyo bule kunakitu , safari za mgonjwa najisi alivyojiriport nikweli inatia shaka, harafu Arusha nimazingira km ya ulaya ulaya hali Yake yahewa, Na corona anapenda hali yahewa km hyo.
Hapa kunakitu.
 
Mi namuona km mstaarab hv. Angekua mwingne wa roho mbaya asingeenda hata hotelini angeenda kushinda club tu akawaachia upupu huko ila yeye aliamua kwenda kujiweka hotelin walau ana kabusara. Kumbuka vipimo vya mwanzo vilidunda ila hakujiamini.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Huyo alikuwa anajua, Na alikuwa anafanya Kwa maelekezo, hivyo asingefanya kinyume cha maelekezo, angekuwa mstaarabu angeeleza pale uwanja wa ndege lkn alitaka atomize maelekezo ya Kazi yke.
Huwa wanafanya Kwa maelekezo maana wanakuwa wanalipwa .
 
Fikiria namna yakugundua dawa sio hizo hadithi zako za sasa.
 
Kuna watu wanajua kujenga imagination za ajab ajab sijui wameathirika na movie
 
Back
Top Bottom