Dada aliyekutwa na Corona Tanzania siyo bure

Dada aliyekutwa na Corona Tanzania siyo bure

AT THE
Corona Ulaya inatarajiwa kupungua au kuisha majira ya joto yakianza Ulaya. Huyu Dada kaileta Arusha,jirani na Moshi ambapo majira ya baridi yataanza miezi michache ijayo. Mbona kama ni mpango maalum vile?!!!
Korona Virus is not a black man disease.
 
choupa moting,
Huyu mama amekaa kwenye nyumba yenye mgonjwa wa corona, angekuwa na busara angeenda kupimwa kulekule Ubelgiji kujiridhisha kama yuko salama ndio aondoke otherwise angepaiwa matibabu kulekule.
 
historia ya safari zake zote, uwezeshaji, (financial flows zake kabla ya safari zake hizo na kuanzia sasa kwa miezi kadhaa na kuendelea) sababu, kiini na msukumo hasa kipindi hili tete.

Napigia mstari hapa mkuu, dunia inawanjanja wengi sana tena wa kiwango cha juu sana. Karibia dunia nzima imesitisha shughuli muhimu sana za kimaendeleo kutoka na janga hili.

Na ilikuwaje wasiwasi wake huo asiuseme huko kabla hajapanga safari ya kurudi Tanzania mpaka afike hapa ndo achukue hiyo tahadhari! wakati anaujua uwezo wetu ulivyo kimatibabu!.
 
Eti sampuli ikapelekwa dar [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwahiyo watu wa daslam tu ndio wamewekewa kipimo hii nchi hii ni takataka

Sent using Jamii Forums mobile app

Samahani mkuu unajua kipimo cha corona kinapimwa wapi?

Kwa taarifa yako ni kwamba kwa bongo hazizidi sehemu mbili zinazoweza kupima huo ugonjwa

Na ya pili itakuwa imeongezeka hivi karibuni tu ila uhakika ni moja tu.

Kuwa makini na usivyovijua
Vishu Mtata,

Iko hivi ukishakuwa na ukaribu na mgonjwa wa corona inatakiwa uji-isolate mapema kabisa

Kocha mkuu wa ARSENAL alivyogundulika ana vimelea vya CORONA timu nzima ilitengwa kwa muda

Sasa yeye ilikuwaje akaja bongo na asijiweke quarantine huko huko bahati mbaya sana hata zile siku 14 bado hazijaisha?

Huyu mama amekaa kwenye nyumba yenye mgonjwa wa corona, angekuwa na busara angeenda kupimwa kulekule Ubelgiji kujiridhisha kama yuko salama ndio aondoke otherwise angepaiwa matibabu kulekule.


Kile kitendo cha kukaa na mgonjwa tu ilitakiwa asije huku.
 
Huyo alikuwa anajua, Na alikuwa anafanya Kwa maelekezo, hivyo asingefanya kinyume cha maelekezo, angekuwa mstaarabu angeeleza pale uwanja wa ndege lkn alitaka atomize maelekezo ya Kazi yke.
Huwa wanafanya Kwa maelekezo maana wanakuwa wanalipwa .

Acha exageration mkuu. Una uhakika?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama wapo wagonjwa wengine wajitokeze waji isolate watapona ndani ya mda mfupi. Corona ni mafua tu wala haiitaji ku exaggerate mambo kiasi hicho.
Nasikia Paula Paul mpaka leo kajifungia stoo ili kukwepa maambukizi. Kumbe ni mafua tu? Mafua dawa yake ni kula kiporo cha wali na maharage ushushie na K Vant chupa ndogo mbili.
 
Hivi ni mtanzania au? Mbona slizulula sana ana biashara gani?
 
Hakuna cha mpango wala nini yani eti tuonewe gere kisa hakuna maambukizi mbona nchi nyingi hazina maambukizi kwanini sisi ndo yawepo na nchi ambazo maambukizi yameonekana kama kenya na Rwanda nazo zimeonewa gere.

Sijui mtoa mada umewazaje aisee nchi imeruusu wageni kuingia na watu kutoka afu unashangaa mtu kuingia akiwa na maambuzi eti yamkini katumwa hilo sio sahihi ata kidogo na maelezo yake yule mama anasema alipokua ubelgiji mume wa mwenye nyumba ndo alikua na maambukizi kwahiyo ana hofu kwamba hapo ndipo alipopatia kwa maana hiyo aliondoka nchini salama akaend tembelea izo nchi nyingine salama ila pale alipoondokea ubelgiji anahisi ndo aliuvaa.

Na mtoa mada uache kutisha watu kua huyu mgonjwa katengenezwa ili kuleta virusi nchini huyu ni mtanzania mwenzetu alierudi nyumbani kuungana na familia yake na kwa upande wangu kwenda hotelini ni sahihi zaidi kuliko angerudi nyumbani kwasababu hizi
kama zilivo desturi za watanzania wengi kusalimiana na kujuliana hali ni jambo la kawaida,kupokea mizigo hasa kwa wanetu pale mtu mzima atokapo safari ndio ustaarabu wetu nadhani nyumbani angeambukiza wengi ambao wangeueneza kwa kasi zaid ni rahisi sana hotelini kutogusa chochote ukawa unatoa maelekez ti kwa wahudumu na ukafanyiwa sio rahis kuwazuia wanao kukulaki pale ufikapo nyumbani
Pia kuna vingi vya kushare ukiwa nyumbani tofaut na hotelini kama asingejihisi mapema basi eneo lake lingekua hatarini zaini

Halafu kuna watu wanamshambulia huyu mama badala ya kumpongeza nadhani kuna waathirika wengi tu wamepita kwenye vizuiz na wana maambukizi na hawajajistukia ilhali labda kuna wengine washaanz kuona dalili lakini huyu mama akasema hapana wacha nijitenge keanza nione na kweli akajifanyia process mwenyewe mpaka sasa hata wewe unajua kuna mgonjwa wa corona na hizo ni jitihada binafsi tu.

Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapana usitake kumtetea, kosa la huyo mama ni kutotoa taarifa pale tu alipowasili nchini. Yeye kujitenga ni jambo sawa lakini alipokwenda jitengea sio mahali sahihi kwani hakuna control measures zozote za kiafya pale. Na ndio maana hata serikali na wataalam wa afya hawatuambii tukijihisi kuumwa au kumwona mgonjwa wa corona basi tumpeleke hotelini au kumwacha home, bali tutoe taarifa kwao ili wao kama wataalam ndio waje na kumpeleka mahali ambapo ni sahihi kwa ajili ya quarantine.
Naelewa self quarantine ipo lakini amesafiri umbali na kukutana na watu hapo katikati ambao kwa namna moja ama nyingine kawaweka ktk hatari ya kuwaambukiza. Ningemuona wa maana kama pale alipowasili tu angetoa taarifa na kuomba basi hata afanyiwe self quarantine bila ya kusafiri mpaka hotelini.
Anapaswa kulaumiwa kabisa kwa namna moja ama nyingine na kikubwa zaidi ni kwa sababu alishajua kabisa kuwa mahali alipotoka kulikuwa na mgonjwa wa corona so hata yeye alikuwa kwenye hatari ya kuambukizwa.
 
1584431944327.png
1584431944327.png
 
View attachment 1390616

Nimejaribu kuwaza na kuchambua jinsi huyu Dada aliyebainika kuwa na virusi vya Corona, nimejiuliza maswali mengi sana.

Baada ya kufuatilia kwa kina nimeambiwa jina lake ni Isabela Mwampamba, umri wake ni miaka 46.

Simulizi ya safari yake ndio jambo kubwa limenifanya niwaze sana na kujiuliza maswali ambayo sisi Watanzania tunapaswa kuwa makini, na kujiridhisha kama gonjwa hili limeingia kwa bahati mbaya ama mpango maalum? Kwenye hili sitanii hata kidogo.

Tunaambiwa huyu Dada aliondoka nchini Machi 3, 2020 kwenda Rwanda. Hatuambiwi alikwenda Rwanda kufanya nini?

Baada ya kukaa Rwanda siku 2 Machi 5, 2020 aliondoka kwenda Brussels Ubelgiji, akiwa huko alikwenda Stockholm Sweden, akiwa huko alifikia nyumba iliyokuwa na mgonjwa wa Corona.

Akaondoka hapo kwenda Norway ambako pia amekaa siku kadhaa hadi Machi 14, 2020 alipoondoka huko kurejea nchini kwa kupitia tena Rwanda na kisha akaingia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA.

Simulizi ya huyu Dada inasema baada ya hapo hakwenda nyumbani Arusha bali aliamua kwenda kulala hotelini kwa madai alikuwa ameanza kujishtukia.

Akiwa hotelini alijiona hayupo sawa ndipo akaenda Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru ambako baada ya sampuli kupelekwa Dar es Salaam ndipo ikathibitika kuwa ana virusi vya Corona hiyo jana Machi 15, 2020.

Kinachonisumbua mimi, mzunguko wote huu hatuelezwi alikuwa anafanya shughuli gani? Najiuliza hivyo kwa jinsi Ulaya ilivyotikiswa na Corona unawezaje kwenda huko ukaishi kwenye nyumba yenye mgonjwa wa Corona na bado ukarejea nchini kwako ambako umeambiwa ugonjwa haujaingia bila hata kusema hayo yote ili tahadhari ichukuliwe mara baada ya kushuka kwenye ndege?

Ni bahati mbaya kweli au ni mpango maalum ulipangwa ili Tanzania nayo itangazwe duniani kuwa imepatwa na Corona?

Najiuliza hivi, ni bahati mbaya kweli kwamba huyu Dada alianzia safari yake Rwanda?

Najiuliza ni bahati mbaya kweli kwa huyu Dada kwenda kuumwaga upupu Kilimanjaro na Arusha kwenye kiini cha utalii wa nchi yetu?

Hivi ni bahati mbaya kweli mtu atoke safari aende kujipiga quarantine hotelini ambako kuna muingiliano wa watu wengi? Kwa nini hakwenda nyumbani kwake na kuwaambia jamaa zake waondoke au atengewe chumba chake kama ilivyokuwa huko safarini Ulaya alikofikia kukiwa na mgonjwa wa Corona?

Nimejiuliza zaidi kwamba labda kwa kutokuwa na mgonjwa wa Corona kulionewa donge na hivyo ikatengenezwa namna ya kutuweka kundi moja?

Kwa mawazo haya, nakumbuka jambo moja tu, Watanzania tunapaswa kuwa makini kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa kuwa ni janga la dunia basi nasi tuungane na dunia kujihadhari na Corona. Tuepuke mikusanyiko isiyo ya lazima, tuepuke kugusana, tuepuke kubusiana, tunawe mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na tutumie viua vijidudu yaani sanitizers.

Kama sio lazima tuache safari hata kutembeleana nyumba kwa nyumba, tukae ndani tutulie. Tuwakinge Wazee na watoto wetu sana kwa sababu hawa ndio wameonekana kupatwa na madhara makubwa ya ugonjwa huu ambayo ni kifo.

Inaelezwa mpaka sasa Corona imesababisha vifo zaidi ya watu 5,000 na watu zaidi ya 150,000 wameugua. Hili ni balaa kubwa, tusichukulie poa hata kidogo.

Lakini pia ukijijua umeambukizwa tafadhari usiambukize wengine, hayo ni mauaji. Nenda Hospitali wataalamu watajua cha kufanya.

Ni hayo tu lakini kwa kweli imeniuma ugonjwa huu kuingia nchini mwetu kwa mtindo huu.

Usiku mwema.

Jotham Mugishagwe Jr.
Ilala, Dar es Salaam.
Machi 15, 2020.
Haya yalikuwa mawazo yangu pia usiku wa kuamkia leo,huyu dada sio kwamba katumika deliberately aulete nchini?watu wa siku hizi ni risk takers, wanaweza hata kujilipua kwa kupatiwa kitita cha kutosha ili kuichafua nchi.Cha muhimu afuatiliwe hasa nini ilikuwa dhumuni la safari yake...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili gonjwa ni hasara kwa Dunia nzima . Tanzania ipo duniani na Dunia ni kijiji kutokana na maendeleo ya miundombinu na hivyo magonjwa ya uambikizi huwa ni rahisi sana kusambaa .
Viwanda vimepunguza uzalishaji, malighafi za viwanda zimeshuka Bei ,makampuni ya usafirishaji yapo hali mbaya , nk
Turudi makanisani kuomba Mungu ulinzi wake hasa sisi afrika bara maskini .
Marekani inasemekana 5% ya GDP itapotea kwa sababu ya hili gonjwa .
Leo wameanza majaribio ya chanjo Tusubiri matokeo yake
 
Back
Top Bottom