Dada aliyekutwa na Corona Tanzania siyo bure

Dada aliyekutwa na Corona Tanzania siyo bure

Mgonjwa wetu pamoja na kuendelea kupata nafuu anaweza kutusaidia habari muhimu sana.

Naomba wakubwa na wahusika wote wasimchukulie raia mwenzetu kama mwathirika tu wa ugonjwa. Jicho la tatu la nne hata la tano litumike. Dunia ina mambo mengi hii.

Sina uwezo wala mamlaka lakini ningefuatilia historia ya safari zake zote, uwezeshaji, sababu, kiini na msukumo hasa kipindi hili tete.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani mfadhili wa hizi safari, ni hiyo shule tu peke yake?? Hasa uwezeshaji

Kiukweli inatia shaka...

Everyday is Saturday..................... 😎
 
Huyu mama anapaswa apelekwe jeshini angakau miezi kadhaa, ukifikiria kwa umakini utagundua kama kafanya makusudi. Kwanini arudi nchini wakati alikoenda kakutana na mgonjwa? Kwanini asingekaa huko huko mpaka athibitike hana ndiyo arudi? Hii inaonyesha namna gani hatuko makini, akipona inabidi ahojiwe vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaelezwa mpaka sasa Corona imesababisha vifo zaidi ya watu 5,000 na watu zaidi ya 150,000 wameugua. Hili ni balaa kubwa, tusichukulie poa hata kidogo.

Nakazia hapa
1) Tuepuke mikusanyiko isiyo ya lazima
2) Tuepuke kugusana, tuepuke kubusiana
3) Tunawe mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na tutumie viua vijidudu yaani sanitizers.
4) Kama sio lazima tuache safari hata kutembeleana nyumba kwa nyumba, tukae ndani tutulie.
5) Tuwakinge Wazee na watoto wetu sana kwa sababu hawa ndio wameonekana kupatwa na madhara makubwa ya ugonjwa huu ambayo ni kifo.

Serikali ingepiga marufuku mikusanyiko ya watu wengi (ibada, shule kufungwa etc) na kuencourage watu kufanyia kazi nyumbani atleast kwa wiki mbili tu. Sometimes inabidi tukubali hasara maana kinga ni bora zaidi
 
Ni huyu? Au tumtafute mwingine?
Screenshot_20200317-114654.png
 
Chain reaction. Hapo ni hatari hauwezi kutrack watu wote katika iyo chain muhimu. Mkoa wa Moshi, Arusha, Dsm kuiweka karantini kwa siku 14. Na kuzuia safari za muingiliano mkoa kwa mkoa kwa siku zingine 14 , jumla inakuwa 28. Tarehe 18 April tufingue mipaka hali ikiwa nzuri na wagonjwa wakiwa washatengwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona Ulaya inatarajiwa kupungua au kuisha majira ya joto yakianza Ulaya. Huyu Dada kaileta Arusha,jirani na Moshi ambapo majira ya baridi yataanza miezi michache ijayo. Mbona kama ni mpango maalum vile?!!!
Itabidi tukuweke chini ya ulinzi utupe maelezo ya kutosha.
 
Uko sahihi sana # Dubu. Matokeo ya mpango huu soon yataonekana
 
Huyo alikuwa anajua, Na alikuwa anafanya Kwa maelekezo, hivyo asingefanya kinyume cha maelekezo, angekuwa mstaarabu angeeleza pale uwanja wa ndege lkn alitaka atomize maelekezo ya Kazi yke.
Huwa wanafanya Kwa maelekezo maana wanakuwa wanalipwa .
mmmh.
 
Watu wana biashara zao na kula bata sio lazima uambiwe wanaenda kufanya nn, Mbona manara yuko wapi usha ambiwa kafata nn uko.

Hakuna mtanzania atakufa kwa Corona ni sawa na mafua kwa kuku wa kienyeji anapiga chafya yanatoka yenyewe yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malengo yao lazima yatumie ili wapige hela kote dunian bila muacha sent.
Kila taifa litaonja utamu wa huu ugonjwa kwa namna yoyote ilee
Mzungu akiamua kupga hela atapiga kweli sio mchezo.
 
Wewe nani ujue nyendo za kila anaeensa nje?mbona watu kila siku wanasafiri bila hata kusema wala kutoa sababu,huko walikopata kuna nini na ntie mukose muna nini,magonjwa yanatembea na watu.
Acha kuwaza siasa majitaka wewe mtoto wa mchikichini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana usitake kumtetea, kosa la huyo mama ni kutotoa taarifa pale tu alipowasili nchini. Yeye kujitenga ni jambo sawa lakini alipokwenda jitengea sio mahali sahihi kwani hakuna control measures zozote za kiafya pale. Na ndio maana hata serikali na wataalam wa afya hawatuambii tukijihisi kuumwa au kumwona mgonjwa wa corona basi tumpeleke hotelini au kumwacha home, bali tutoe taarifa kwao ili wao kama wataalam ndio waje na kumpeleka mahali ambapo ni sahihi kwa ajili ya quarantine.
Naelewa self quarantine ipo lakini amesafiri umbali na kukutana na watu hapo katikati ambao kwa namna moja ama nyingine kawaweka ktk hatari ya kuwaambukiza. Ningemuona wa maana kama pale alipowasili tu angetoa taarifa na kuomba basi hata afanyiwe self quarantine bila ya kusafiri mpaka hotelini.
Anapaswa kulaumiwa kabisa kwa namna moja ama nyingine na kikubwa zaidi ni kwa sababu alishajua kabisa kuwa mahali alipotoka kulikuwa na mgonjwa wa corona so hata yeye alikuwa kwenye hatari ya kuambukizwa.
Kweli kabisa yani huyo mama ana makosa sana,mbona hakwenda nyumbani kwake moja kwa moja? Na nahisi alivyofika airport alishaanza kujisikia vibaya.Alitakiwa ajisalimishe achukuliwe na ambulance apelekwe hospitali.Nashangaa wanaomuona shujaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom