Dada aliyemuua jambazi katika harakati za kumuokoa mume wake: Sheria imekaaje? Je, ana kesi yoyote ya kujibu?

Mwanamke kama huyo ndo superwoman sasa na si hawa wa mjini hawa wanaojishaua kwenye maredio na matv wakijifana masuperwoman
 
Kesi ipo.

Atashtakiwa kwa kuua.

Na yeye atajitetea kwamba alikua ana-act in self defence na kulinda mali zake.

Tukumbuke kosa la jinai mshtaki ni jamhuri hivyo siyo lazima awepo wa kushtaki ndiyo kesi ifike mahakamani.

Kwakua mtu ana haki ya kulinda uhai wake kivyovyote natarajia asikutwe na hatia. Ila kesi ipo.
 
Kuna kundi likiua hamleti hivi vidubwasha vyenu vya mawazo.
Je dereva wa Lori na Kontena lake aliyeua jana ana Kesi ya kujibu kama yupo hai?
 
police wanavopenda misifa yaani baada kuuwa wenyewe jambazi ili apate misifa, ukauwa wewe.... watakuhenyesha apo mtonyo wa nguvu lazima aisee... utackia lete tumalize kesi!
 
Habari inaonesha alimpiga gongo halafu wananchi "wasiozipenda kampuni hewa za uchukuzi"(wenye hasira kali na kuwachukia majambazi) ndiyo wakampiga hadi akasema "haleluya tutaonana"!Sasa,mbona yeye hahusiki na kuua?Alimdhibiti kwa gongo asitoroke tu.
 
HUYO DADA NI SHUJAA/Japo polisi wanaweza kuhitaji chochiote kiajabu
 
Eti jambazi kapigwa na jiwe!!kibaka uyo
 
Kama sheria inafuatwa, je cases ambazo majambazi wanauawa na polisi katika matukio, huwa utaratibu huu unafuatwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…