Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hii ni barua ya wazi ya mtu akimuandikia Dada yake.

Japo Dada yake huyo ni mtu mzima, ameolewa na ana watoto, hivyo kwa watoto wake wanamwita Mama na ana wajukuu ambao wanamwita Bibi, lakini kwa sisi wa rika lake, wale watu wa 60s, huyu kwetu ni dada yetu mkubwa!, hivyo hili ni bandiko la kikubwa!.

NB: Ukiona halijatajwa jina lolote zaidi ya Dada Mkubwa, nakuomba na wewe usitaje jina lolote!.


Soma: Rais Samia aligoma alipoambiwa atoke ili wajumbe wapige kura na kumpitisha. Hii ina maanisha CCM wengi hawamtaki?

Dear Dada,

Kiafrika kwa vile wewe ni dada mkubwa, Shikamoo Dada Mkubwa!.

Naomba Kuanza na Angalizo la Declaration of Interest.

Mimi ni mwana CCM na ni kada wa CCM, baada kuibuka kwa kada mpya ya uchawa na machawa, ukisifu tuu utanyooshewa kidole cha uchawa, naomba kudeclare inte mimi sio chawa wa Mama, wala bandiko hili sio bandiko la kichawa kutafuta shavu au kusaka fursa! Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!, bandiko hili ni bandiko la kaka mtu kumsaidia Dada mtu, asiwasikilize machawa kwenye kila kitu, kuna baadhi ya vitu machawa hawamsaidii na wengine wanampoteza kwa kumpotosha, hivyo hapa kaka mtu anamsaidia Dada mtu atende haki abarikiwe zaidi na zaidi!.

Mimi mdogo wako, nilibahatika kuwepo Dodoma kwenye ule Mkutano wetu Mkuu, na kushuhudia kilichofanyika, hivyo kwanza niungane na Watanzania wengine wote kukuhakikishia tuna imani kubwa na wewe, na hatuna shaka na uwezo wako kuendelea, hivyo nijiunge na wengine wote kukupongeza ulivyoaminiwa hadi watu kuhamanika na kukupitisha kwa kishindo kinyume cha katiba ya chama chetu, lakini kwasababu kilichofanyika kimefanyika kwa nia njema, in good faith, pokea pongezi zangu za dhati na pia pokea ushauri wangu japo sio lazima, kuufuata au kuutekeleza!.

Japo najua utakuwa unanifahamu kutokana na jina langu, si geni masikioni mwa wengi wale wa zamani waliokuwa wakiisikiliza RTD, nikaja DTV kwa waliowahi kuangalia kipindi cha Mada Moto Uchaguzi 95, ni mimi ndie nilikuja Zanzibar na kuyatangaza yale matokeo ya kweli ya Uchaguzi wa Zanzibar ile 1995. Kisha nikaendesha kipindi cha Kiti Moto, na sio vibaya nikijitambulisha tena kwako kwa kukumbusha tuu, kwenye mtandao huu wa JF, ni mimi ndiye mtu wa kwanza kukutambulisha wewe humu jf ile 2010 kabla hata hujateuliwa Waziri wa serikali ya JMT. New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!



Ukiwa Waziri Ofisi ya Makamo wa Rais, mimi nilikufanyia mahojiano ya zaidi ya saa nzima na kuyarusha TBC, ITV, Star TV na Channel Ten.

Ukiwa M/Mwenyekiti Bunge Maalum la Katiba, nilikufanyia mahojiano mengine pale Bwawani Zanzibar ya kipindi cha 30 min na kukirusha TVZ, TBC , ITV, Star TV na Channel Ten, na hapa nilipo nina vipindi vyako 4 , Mzee Stephen Wasira na Getrude Mongela wakiwafundisha Watanzania kuhusu Falfasa yako ya 4R, Vipindi hivi bado havijapata udhamini, vikipata udhamini vitakwenda hewani, kupitia TBC, ZBC, Azam TV, ITV, Channel Ten na Star TV.

Kitaaluma mimi mdogo wako ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, na pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea.

Tulipoanza kuzungumzia uwezekano wa Tanzania kutawaliwa na rais mwanamke ile 2015, jina lako ndilo lilishika number moja!. Hivyo japo umeupata urais wa JMT kwa kudra tuu za Mwenyeezi Mungu, Mungu aliisha kupangia siku nyingi kabla na akakuandaa. Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?

Japo hakuna binaadamu yeyote anayeijua mipango ya Mwenyeezi Mungu, kwanini alimtwaa yule Kaka yako na nafasi yake akakuweka wewe, lakini tuko baadhi yetu tunazijua sababu ambazo zinaweza kuwa zimechangia kumletea machukizo na hivyo kupelekea kutwaliwa!. Sasa tunapokuona na wewe unanza kunyemelewa na sababu zitakazo kuletea machukizo, hatuwezi kunyamaza. Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe?

Sababu zilizopelekea machukizo kwa kaka yako ni nyingi tuu naomba tusizitaje humu ili kumwacha apumzike kwa amani, lakini sababu hizo zinapoibuka awamu yako, naomba tusizinyamazie!. Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao! na ulipotoa taarifa ya wewe kuua mbu tuu au mende, tulishauri Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Tangu ukiwa VP umekuwa ukisisitiza haki, haki, haki, na mimi humu nilandika maandiko yangu mawili kukuhusu wewe kwa kukusifu na kupendekeza kwa yule kaka yako akupishe wewe 2020, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza lakini kufuatia ule utaratibu wa mserereko wa CCM, (ambao ki haki ni haram) , ile 2020 JPM aliendelea kwa mserereko, na matokeo ndio kama vile!. Japo wewe unajihesabu uliingia kwa kudra, kuna watu hiyo kudra yako, wao waliikudrisha tokea mwaka 2017!. Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020

Kama nilivyojitambulisha mimi ni mwandishi na pia ni mwanasheria, kwasawa vile wewe sio mwanasheria, unawategemea wasaidizi wako sheria ndio wakusaidie kukuambia hili jambo ni sawa au sio sawa, kiukweli dada yangu mkubwa, sometimes hao wasaidizi wako sheria, ukweli wanaujua, lakini wanakuacha ufanye mambo ya ajabu, sisi huku mabarabarani, vichochoroni na vichakani huwa tunajaribu kukusaidia ili ufanye the right things, lakini wasaidizi wako hawakuelezi ukweli.

Kwenye sheria, kiukweli tumefanya mambo ya ajabu, tukianzia na Ile ya DP World, Dubai sio nchi kisheria, haina sovereignty, therefore has no capacity to contract an international treaty, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
Nilijiuliza kuhusu wanasheria wetu "IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Dubai sio nchi, status yake ni kama ya Zanzibar, nikashauri kama nchi tumeweza kuingia treaty na an entity ambayo sio nchi, tunashindwa nini kuiruhusu Zanzibar iwe kama Dubai? Zanzibar Kama Dubai, Hazina Sovereignty, - No Capacity to International Treaty, Kama Tumeingia Mkataba na Dubai, Kwanini Zanzibar Izuiwe Kujinga OIC?!


Wakati mkataba ule unaingiwa, sheria zetu za rasilimali za taifa, haziruhusu kitu kama kile, tulipaswa kwanza kurekebisha sheria zetu kisha ndio tuingie ile IGA, hivyo IGA ile kwa jicho la kisheria ilikuwa illegal!. Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts? tumeingia illegal contract!, Bunge likapitisha!, Bunge pia tukalishangaa!

Kiukweli hatujui kilikuja kufanyika nini chini ya kapeti, lakini hatimaye ikatoka HGA safi ! na sasa mambo safi kazi inaendelea!.

Ukaunda Kikosi Kazi cha Prof. Mkandala, mimi binafsi nikabahatika kuchangia mara 3, na zote nikashauri kitu kile kile!.
Muswada wa sheria ulipotoka tukakupongeza, kwasababu ulifuta sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa na kuunda sheria moja ya uchaguzi chini ya Tume Huru ya Uchaguzi, hivyo tukapendekeza uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2025 ufanyike siku moja, na usimamiwe na Tume Huru.
Sijui ni nini kilikuja kufanyika mara uchaguzi wa serikali za mitaa ukatangazwa na kusimamiwa na sheria ilioshafutwa!.

Bunge letu tukufu chini ya mwalimu wangu wa sheria, likakutungia sheria batili, ukaisaini, ndio tunakwenda nayo uchaguzi mkuu hii October.
Kwa vile wewe sio mwanasheria, kiukweli tumekusamehe wewe hauna kosa kweli hili kwasababu mtu ambaye sii mwanasheria, hategemewi kuubaini ubatili wa sheria kwenye vifungu vya kisheria, lakini wasaidizi wako wanajua kila kitu, ila wamekuacha!. Asking Aloud: Rais Samia anajua Katiba yetu ni batilifu, na Sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini ni sheria batili kinyume cha katiba?

Kwa vile huu ni mwaka wa uchaguzi, naomba univumilie Dada Mkubwa, niseme yote, ili hata huko mbeleni yakija kutokea ya kutokea, I will have a clear conscious kuwa nilitimiza wajibu wangu

Mimi kila Jumapili kwenye gazeti la Nipashe na Jumatano kwenye gazeti la Mwananchi natoa
makala elimishi za kwa maslahi ya taifa, ambazo huwa na maswali, hoja, majibu utaweka mwenyewe, swali la leo ni kujiuliza kwa sauti, asking aloud: "Je Rais Samia anajua kuwa Katiba yetu ina ubatili fulani, uliochomekewa kiubatili hivyo kuifanya Tanzania kuwa na katiba Batilifu?. Je anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini hapa juzi kati ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya Mwaka 1977?. Je, anajua ubatili huu unadhulumu haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa?. Je anajua kila dhulma ya haki, huwa ina consequences?

Hili shurti la wanasiasa kudhaminiwa na chama cha siasa, ili kugombea uongozi ni shurti batili liko kinyume na katiba ya JMT ya mwaka 1977, na limechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu. Shurti la Mgombea Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Shurti Batili, Lililochomekewa Kiubatili Ndani ya Katiba Yetu. Kwanini Tunalikumbatia?

Mahakama Kuu iliishalifutaSerikali, Bunge, Ziheshimu Mahakama! Kwanini Serikali na Bunge Hazijatekeleza Hukumu ya Mahakama kuhusu Ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?

Kufuatia ubatili huu, unamaanisha katiba yetu ni katiba batilifu, ina ubatili, na sheria mpya ya uchaguzi ni sheria batili!. Serikali yetu tukufu imetunga muswada wenye kipengele batili, Bunge letu likatunga Sheria batili, na Rais akaisaini hiyo sheria batili kuanza kutumika bila yeye Rais kujua kuwa amesainishwa sheria batili!.

The only excuse ya rais kusaini sheria batili kuanza kutumika, ni kwa vile Rais wetu sio mwanasheria, hivyo hategemewi kuujua ubatili wa Katiba, ila kwa vile anawasaidizi wake sheria, wakiongozwa na Waziri wa sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hawa ni manguli wa sheria, wabobezi na wabobevu ambao wanaujua kabisa ubatili wa sheria hiyo, na ubatili wa Katiba, lakini hawajamweleza Dada Mkubwa kuhusu ubatili huu kwa excuse kuwa ubatili huu umefanywa na awamu zilizotangulia, Dada Mkubwa kaingia kaukuta, hivyo wakamtungia tuu sheria batili kwasababu sheria ikiyokuwepo nayo ni batili lakini ilikuwa inatumika!

Kuna kanuni ya the doctrine of separation of powers between mihimili inayokwenda na kitu kinachoitwa checks and balance inayoitaka kila mhimili kuwa kiranja wa mhimili mwenzake usikiuke mamlaka yake wala usikiuke katiba.

Licha ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuutangaza ubatili huu na kuubatilisha, lakini Serikali ya awamu ya Sita, bado imetunga muswada wa sheria wenye ubatili ule ule, na Bunge letu, likaupokea muswada huo batili na kuutungia sheria kitutusa, hali iliyowafanya wabunge wetu makini kugeuka kama mazuzu vile, checks and balance inatoka wapi?

Bunge letu chini mwalimu wangu, mwanasheria mbobezi na mbobevu, Dr. Tulia Akson, alipaswa kulitumia Bunge to i check Serikali kuwa haiwezi kututungia muswada batili, na Bunge lina mamlaka ya kuuondoa ubatili huo na kutunga sheria safi isiyo na ubatili, lakini Bunge letu, likatunga Sheria Batili kitutusa na kumpelekea Rais Samia kuisaini!. Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?

Kwavile Dada Mkubwa anawaamini sana wasaidizi wake, wamemtungia muswada batili na Bunge likitunga Sheria batili, Rais Samia yeye amesaini with very clear conscious kuwa anasaini sheria halali bila wasaidizi wake kumweleza kuwa sheria hiyo ni batili, hivyo kwenye hili la ubatili wa sheria mpya ya uchaguzi, Rais Samia hana kosa kabisa, wenye makosa ni Serikali kutunga muswada batili na Bunge kutunga sheria batili!.
- Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?

Je inawezekana Dada Mkubwa anasikia kabisa kilio hiki, ila Wahafidhina wa Chama Chake Ndio Hawataki, Katiba ni Sheria Mama. Sheria Yoyote Kinyume na Katiba ni Batili. Wanasheria Wetu, Waliwezaje Kufanya Madudu Haya Kuchomeka Batili Ndani ya Katiba?
Tumefanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa sheria batili na mambo yanaendelea, na mwaka huu tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu na katiba batili na sheria batili!.

Kwa vile Mungu ni haki, no one knows for sure kwanini yule aliitwa na kuondoshwa mapema, usikute na hii dhulma ya haki za Watanzania, zimechangia, naendelea kusisitiza Dada yetu mkubwa, if there is anything you can do to help out Watanzania kurejeshewa haki zao, Please do, utabarikiwa, tutabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!.

Swali la msingi la bandiko hili. Jee Rais Samia anajua kuwa Katiba yetu ina ubatili fulani, uliochomekewa kiubatili hivyo kuifanya Tanzania kuwa na katiba Batili?. Je anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini hapa juzi kati ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya Mwaka 1977?. Jee anajua ubatili huu unadhulmu haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa?. Jee anajua kila dhulma ya haki, huwa ina consequences?.
Jee Rais Samia Afanye Nini?.

Mungu Mbariki Dada Mkubwa, jicho ona lake liione hii dhulma kubwa ya haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa airejeshe,
Wakati tukililia haki hii kurejeshwa, huku CCM ndio kwanza...

Kama nilivyosema hakuna ajuaye sababu za yule Kaka yako kutwaliwa, ila inawezekana kilichotokea uchaguzi wa 2019 na 2020 kimechangia!.

Tunakushauri Dada Mkubwa usitupeke kwenye uchaguzi mkuu na hii sheria batili, muda wa kuirekebisha upo tena wa kutosha tuu, kitu muhimu ni uwepo wa utashi wa kisiasa, political will!.


Sasa tuje kwenye kilichofanyika Dodoma.
Kwanza naomba kukukumbusha tuu Dada kwa faida ya wengine.
Ibara ya 4 ya CCM inasema :


Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:

Binadamu wote ni sawa.

Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

Hivyo wana CCM wote ni sawa mbele ya chama.

Ibara ya 7 inasema
Raia yeyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18, anaweza kuwa Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi

Hii maana yake Chama cha Mapinduzi ni chama cha wote!.

Ibara ya 14, inazungumzia Haki za Wanachama


Mwanachama yeyote atakuwa na haki zifuatazo: -
  1. Haki ya kushiriki katika shughuli zote za CCM kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
  2. Haki ya kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya CCM pale ambapo anahusika kwa mujibu wa Katiba.
  3. Haki ya kuomba kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa CCM na ya kuchagua viongozi wake wa CCM kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na Taratibu za CCM.
Kwa ibara hiyo inamaanisha ule utaratibu wa mserereko, ni utaratibu batili, unaofifisha haki za wanachama kugombea nafasi za juu za uongozi, na haupo mahali popote kikatiba, ndani ya katiba ya CCM.

Kwa vile wewe uliingia kwa kudra tuu bila kusailiwa, na hii kwako awamu ya kudra inahesabika ni awamu yako ya kwanza, awamu yako ya pili ya 2025-2030 unapaswa kuendelea kwa mserereko.


Kwa vile dhima ya mserereko ni kuepuka duplicity kwa rais ambaye amekwisha sailiwa, wewe hapo mwanzo hukusailiwa, na kufuatia your wonderful performance, wana CCM katika umoja wetu kupitia Mkutano wetu Mkuu kwa kauli moja tumeamua ni wewe tuu, na tumekupitisha, bila kujaza fomu, bila kusailiwa na bila kupigiwa kura! .

Japo kwa mujibu wa Ibara ya 100 (2)ya katiba ya CCM, Mkutano Mkuu una mamlaka yote ya kufanya jambo lolote, Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa utakuwa ndicho Kikao Kikuu cha CCM kupita vyote na ndicho kitakachokuwa na madaraka ya mwisho.

Lakini kama hilo jambo limewekewa kanuni na utaratibu wa jinsi ya kufanyika, utaratibu ni huu
Ibara ya 101 (4) inauruhusu Mkutano Mkuu, Kubadili sehemu yoyote ya Katiba ya CCM kwa uamuzi wa theluthi mbili za Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka Zanzibar.

Mfano halisi ni mgombea urais wa JMT, lazima ajaze fomu kuomba, ajadiliwe na secretariat, apendekezwe na Kamati Kuu, ateuliwe na Halmashauri Kuu na kuchaguliwa kwa kura na Mkutano Mkuu, Mkutano huo Mkuu hauna mamlaka ya kufanya vinginevyo, mpaka kwanza kutengua vifungu hivyo vilivyopo ndipo kisha kulipitisha jambo letu hilo lifanywe vinginevyo!.

Pale Dodoma, hakukuwepo azimio lolote la kutengua kwanza kifungu chochote cha katiba, taratibu na kanuni, kwa mujibu wa ibara ya 101 (4)ndipo azimio la kumpitisha kwa utaratibu mpya likapitishwa.

Sasa CCM kama Chama ndicho kimeshika hatamu kuiongoza serikali, kama kinaweza kuikiuka katiba yake kwenye jambo kubwa kama hili, itakuwaje kwa katiba ya nchi?.

A Way Forward

  1. Katiba ya nchi, ndio sheria mama ya nchi hii, katiba zote za vyama lazima zifuate sheria mama, ule utaratibu wa mserereko wa CCM, ni kinyume cha katiba ya nchi, na kinyume cha katiba ya CCM, Dada naomba ukiondoe, ukubali usailiwe tuu na tutakupa kura zote!.
  2. Kufuatia kazi kubwa, nzuri na iliyotukuka iliyofanywa na Dada katika awamu yake ya kwanza, naamini hakuna mwana CCM yeyote atakayethubutu kujitokeza kumpinga.
  3. Na hata wakitokea, maadam tumeisha amua kwenda na Dada, a due process ifanyike, kumsaili na wote watakao jitokeza, chinjilia mbali baharini, litoke jina moja, tuu lipigiwe kura zote za ndiooo!.
  4. Hii due process ikifanyika, kiukweli Dada Mkubwa atabarikiwa na serikali yake itabarikiwa.
  5. Siku zote nimekuwa nikiwasisitiza Wapinzani kujifunza kutoka CCM, lakini leo nashauri hakuna ubaya chama changu CCM kujifunza kutoka Chadema kuhusu uchaguzi wa demokrasia ndani ya Chama kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama.
  6. Kwa mujibu wa katiba ya JMT, Dada Mkubwa anaweza kushauriwa tuu, hapaswi kulazimishwa kupokea ushauri wowote kutoka kwa yeyote, atafikia maamuzi yeye mwenyewe kama yeye, hivyo Dada Mkubwa, mwisho wa uwezo wetu ni ushauri tuu, uamuzi wa kuusikia na kuufuata ni wako, au kuusikia na kuuignore au hata kutousikia kabisa!.
Nahitimisha kwa ule utangulizi, kukuhakikishia Dada Mkubwa, Watanzania tunakupenda sana tuu, na tunakukubali sana. Kama ni wewe, uliyetueliwa na YEYE kuendelea 2025 -2030, then ni wewe tuu na hakuna mwingine yeyote zaidi yako!. Usiruhusu ule uhuni uliofanyika kwenye katiba ya nchi, kufifisha haki kuu ya kuchagua na kuchaguliwa, ukaingizwa ndani ya chama chetu cha haki, usiwasikilize wahafidhina, wewe shikilia kufuata katiba ya CCM na katiba ya nchi kwa kuruhusu ile the due process, kufanyika, you'll have everything to gain, and nothing to loose, na utabarikiwa sana!. Ukiendelea na kilichofanyika, you'll have everything to loose and nothing to gain!.
Nakutakia kazi njema
Mungu Ibariki CCM itende Haki.
Mungu Ibariki Tanzania.


Kaka yako mdogo
Paskali.
 
Wajumbe ñi wanafiki sana! Hela zimeisha ndo mnakuja kulia mtandaoni! Kwenye kikao si mlikuepo??

Mtu ambaye sio mnafiki ni mpina tu! Yeye hakuunga mkono kwa kutosimama kushangilia lakini wengine wote ni wachumia tumbo tu! Pesa ikiisha ndo akili zinawarudi
 
Nilishangaa sana katika wakati ambao Upinzani ulionekana uko vipande vipande, bado MTU anataka mseleleko?

Hata hivo nikaandika, Kosa lilelile alofanya JPM kufurahia habari za Machawa kumtaka aongoze milele, ndio hilohilo analofanya Dada yako yaan wote walifurahia uvunjajinwa Katiba.


Ukiangaliaa Kwa mbali sana, Utagundua Amejaa kwenye Mfumo wa Kuondoshwa kama ilivyokua .

Mungu anaweza kukupa Uongozi ila Kwa mpito tu yaan kipindi fulan, kikishapita, Usilazimishe .
 
Dodoma ulikuwepo na yalio jiri uliyashuhudia.
Hapa umekuja kuleta hoja ambayo pia umejitahidi kuzunguka weeeee hata sijui unahofia nini kumtaja wakati andiko lako nime muweka wazi.
Anyways........
Naskia unasubiria uteuzi, na kuna tetesi kwamba uliomba kuonana nae lakini black suits wakakutosa.
Nami sijataja jina kama ulivyo elekeza mkuu...😊
 
Dodoma ulikuwepo na yalio jiri uliyashuhudia.
Hapa umekuja kuleta hoja ambayo pia umejitahidi kuzunguka weeeee hata sijui unahofia nini kumtaja wakati andiko lako nime muweka wazi.
Anyways........
Naskia unasubiria uteuzi, na kuna tetesi kwamba uliomba kuonana nae lakini black suits wakakutosa.
Nami sijataja jina kama ulivyo elekeza mkuu...😊
🤣🤣
 
Katika siku za karibuni walau Leo umeongea neno, heko.

Nachelea kusema chama hakina mwanasheria, kwani wakati mama alikua anafanya consultation alipaswa kutoa ushauri uliuleta hapa.

JK alijaribu kusema kitu lakini akaona umma unataka kumgeukia ikabidi atulie lakini maelezo mengi aliyoyatoa unaona kabisa alikua anaona ni kinyume lakini aliona isiwe taabu.

WanaCCM hawajapewa nafasi ya kugombea kama katiba Yao inavyosema bali wamepewa wenyechama.

Kwenye kikao hicho kilipiga marufuku watia Nia kupitia huko majimboni kutoa Nia ila wao na kupitishwa wamepitishwa, je hii sio double standard?
 
Back
Top Bottom