Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

Kaka yangu Pascal Mayalla unaangaika sana kujipendekeza ndugu yangu. Yaani badala ua kuwa straight to the point unazunguka wee ilimradi uonekane haujamkosoa mama.
Lakini ndugu yangu nikukumbushe kwamba wewe ni mkristo, naa maadiko ya kikristo yanatukataza sana kuwa ndumilakuwili ieleweke wazi WEWE NI BARIDI AU JOTO NA SIO VUGUVUGU.

Wewe ulipaswa unyooshe rula (maelezo) kwa huyo dada yako kwamba jambo ulilofanya kwenye ule mkutano wa Dodoma ni UBAKAJI WA DEMOKRASIA NDANI YA CHAMA HIVYO TUBU URUDISHE MCHAKATO HALISI WA KUMPATA MGOMBEA WA CHAMA KWA KUPIGIWA KURA.
Nchi hii tukisimamia vizuri hii slogan ya No Reform No Election itakomesha hata tabia ya mwenyekiti wa ccm taifa kuleta mgombea mmoja kwa wajumbe kama surprise ya pete ya uchumba na kupigiwa kura ya ndio na hapana kama kipindi cha mfumo wa chama kimoja.
 
Unafikiri atasikia basi? Wamevunja katiba yao tena. Ilivunjwa mwaka 2015 kwa mwenyekiti kwenda na majina kwenye Kamati kuu wakati sheria yao ilitaka waombaji wote wapite kamati kuu kuhojiwa kisa majina matano yapelekwe Halmashauri Kuu. M

Halmashahri kuu ikishakujadili inapigia kura majina matatu ya kwenda mkutano mkuu. Kwenye mkutano mkuu unaamua mgombea.

2015 katiba na kanuni zilivunjwa, 2020 pia tukaenda mserereko japo haipo kwenye katiba na Sasa 2025 ndo bomu kubwa. Zimevunjwa kanuni zote maana ajenda za mkutano zinatakiwa zitumwe kwa wajumbe kabla ya kikao cha mkutano mkuu.

Ngoja tuone yetu macho.
 
Wahenga walisema sikio la kufa halisikii dawa, ila dada mkubwa kama angalikuwa anasikia basi kuna vitu angejitahidi kupingana navyo hata kama machawa wanamlazimisha vitokee.

Machawa wanaharibu sana taifa letu, viongozi wengi imekuwa kama fashion kuchukuliwa na upepo wa machawa bila kupima na kushirikisha ukweli unaotoka ndani ya nafsi yao.

Dada mkubwa alikuwa anakuja vizuri na alikuwa ana nafasi kubwa ya kutawala mioyo ya Watanzania ila kwa sasa jambo ambalo inabidi akubaliane nalo ni ukweli usiopingika hana ushawishi na wananchi wengi hawampendi.

Wananchi wengi ni wajinga kitu ambacho bado ni fursa kwa Taifa la Tanzania na ukiweza kuwawin wako tayari wakuone shujaa hata kama nyuma ya pazia unayoyafanya ni maovu kuliko, mfano mzuri ni mtangulizi wa dada.

Sitoacha kusema dada alikuwa na nafasi nzuri ila kwa namna ulivyodeal na issue ya bandari, muendelezo wa SGR, kuwaamisha wamasai, manunuzi ya ndege binafsi na mambo ya utekaji hasa kauli zake, hapa ulikuwa anabomoa utawala wake kwa mikono yake.

Mbaya zaidi amekuwa na hofu ambayo madhara yake ni makubwa sio tu kwa chama bali kwa mstakabari wa taifa letu, kitendo ulichokifanywa hakitafutika kwenye reference ya kuvunja katiba ya chama.

Chama chake kimekuwa hodari wa kutumia dola kubaki madarakani, kipi kilikuwa kigumu kufanya demokrasia hata ya uongo na kweli kwenye kuchagua na kujibakiza kwenye ushindi bila kuvunja katiba.

Kitendo cha kutofuata utaratibu na katiba ya chama inazidi kuchochea fukuto la hasira si tu kwa wapenda demokrasia hata kwa watu wasijihusisha na siasa.

Kwa matukio yote ya dada na kwa namna Chadema inavyopractise demokrasia ni rahisi sana kupata mass support pamoja na ushawishi wa kimataifa.

Dada alikuja vizuri ila yeye mwenyewe akajibatiza uchura kiziwi na kukubali TAL kuwa ni Simba dume, sasa acha apambane na maji ya moto tuone nani atashinda.
 
Nimesoma bandiko lako, hongera kwa kushauri! Kuna mambo kadhaa hayana mbadala, kama vile MUDA, MAJIRA, KUCHOKWA, HOFU YA KISICHOONEKANA, DESTURI, N.K. Ukaidi wa mtu dhidi ya mambo mema kwa wengine walio wema, huzidi kuharakisha jambo jema kujiri/ kutokea....
Hofu kwa binadamu ni ya muda mfupi na Ndiyo maana hakuna anayeweza kubuni kinga ya hofu ya zaidi ya mwaka mmoja yaani kifaa kinachoweza kutabili hofu ya miaka 2 ama zaidi inayo kuja wengi tunakuwa na hofu kwa muda wa miezi mitatu hata ukitendwa ile hali ya kulifikiria jambo haidumu kwa muda mrefu
Pia unaweza kutabili vizuri hofu ambayo una historia nayo siyo mpya
 
Kama alidiriki kuita katiba ya nchi iliyomuweka pale kwamba ni vijikarasi atashindwa vipi kusigina katiba ya chama ambacho ndio kinacho tengeneza na kuzalisha uozo wote uliojaa kwenye mfumo

kilichotokea anajua kabisa hana ushawishi hata kwa wanachama wake achilia mbali wenye nchi ambao wengi hawapendi hata kuiona sura yake wakisikia sauti yake wanaishia kusonya na kutukana, Dada yako amedoda na ndio maana kila kona ya nchi kuna mabango ya kumpamba na kumsifia
 
Back
Top Bottom