Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

Just thinking aloud:

Ingetokea kwenye Mkutano Mkuu wa CHADEMA, likatokea Tangazo kwamba Kamati Kuu imeamua kuleta jina moja tu la Makamu Mwenyekiti ili kuthibitishwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu.

Hali ingekuwaje?
(Just thinking aloud).

Wachambuzi wa Siasa na Demokrasia wangekaa kimya, kama walivyokaa kimya baada ya Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma?

UHALISIA HAPA UKO WAZI.

Sisi Watanzania bado tuko nyuma sana ya Utaratibu wa Kidemokrasia hapa duniani.
 
Mkuu

Hon. Adv & Snr Journalist P.

I salute you; you have spoken my mind for the valuable, and wise words through a professional and decent approach to delivering the precious message to the head of 'BOMA'. I sincerely appreciate your moral and ethical intuition and I subscribe to having represented my feelings and the rest.

I am eagerly waiting for the response from the 'Queen' to prevent the consequential aftermath for violating the cultural rituals of the kingdom undertaking...!!
 
Just thinking aloud:
Ingetokea kwenye Mkutano Mkuu wa CHADEMA, likatokea Tangazo kwamba Kamati Kuu imeamua kuleta jina moja tu la Makamu Mwenyekiti ili kuthibitishwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu.
Hali ingekuwaje?
(Just thinking aloud).
Wachambuzi wa Siasa na Demokrasia wangekaa kimya, kama walivyokaa kimya baada ya Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma?
UHALISIA HAPA UKO WAZI.
Sisi Watanzania bado tuko nyuma sana ya Utaratibu wa Kidemokrasia hapa duniani.
Kuna mda nikikaa nikatafakari kuhusu mstakabari wa Taifa letu inanifanya niwaze uenda kuna kizazi kitakuja kuleta ukombozi wa kweli wa hili Taifa.

Tumekuwa na viongozi wasiofikiria kuhusu hili Taifa, licha ya mali nyingi wanazoiba na kutumia ila bado wamekosa uungwana hata kidogo na kuliwazia mema hili taifa.

Wazee ambao wangekuwa na busara hata kushauri juu ya mienendo ya kidemokrasia wao ndio wameketi na kupitisha mambo ya hovyo kuwahi kutokea.

Hii nchi ni mali yetu kama Watanzania kukaa kimya hakuwezi kuondoa ukweli wa mambo, tunakoelekea kutakuwa kubaya zaidi ya tunakotoka.
 
Usizunguke sana, CCM haina uwezo tena wa kushindana kwenye demokrasia ya kweli. Magufuli ndio alikuja kuua uwezo mdogo uliokuwa umebakia wa wanaccm kushindana kihalali. Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, CCM ilitaka kujitutumua kushindana kwa haki, ikawa inapoteza kwa kasi ya ajabu. Alipoingia Magufuli akaona aiokoe ccm na ushindani wa kweli, maana haina uwezo huo.

Ulichokiona kwenye kile kikao cha juzi Dodoma kumtoa Mwali, ndio uhalisia wa ccm. Usitake kuwashauri kitu kitakachowapoteza. Uchaguzi wa kweli wa kidemokrasia upo cdm tu.
 
Wajumbe ñi wanafiki sana! Hela zimeisha ndo mnakuja kulia mtandaoni! Kwenye kikao si mlikuepo?? Mtu ambaye sio mnafiki ni mpina tu! Yeye hakuunga mkono kwa kutosimama kushangilia lakini wengine wote ni wachumia tumbo tu! Pesa ikiisha ndo akili zinawarudi
Mpina naye akapinge uamuzi kwenye vukao au hata mahakamani. Kutosimama kushangikia si kigezo cha kusema kapinga, mtu anaweza kusema alikuwa kachoka tu.
 
Kufuru kubwa.. eti adui yako kama unammudu usimwachie Mungu (sikiliza vizuri)..wanashangilia kama mazuzu.
Hawa wanasiasa wanajua hoja ya kwamba Mungu hayupo, kwa sababu angekuwepo wasingehitajika kumsaidia kuendesha nchi.

Ndiyo maana wanatoa kauli hizi ambazo wewe unazioma za kufuru.
 
Wajumbe ñi wanafiki sana! Hela zimeisha ndo mnakuja kulia mtandaoni! Kwenye kikao si mlikuepo?? Mtu ambaye sio mnafiki ni mpina tu! Yeye hakuunga mkono kwa kutosimama kushangilia lakini wengine wote ni wachumia tumbo tu! Pesa ikiisha ndo akili zinawarudi
Hata huyo Mpina ni muoga tu, alitakiwa apinge humo humo kikaoni na sio kugoma kushangilia.
 
Baada ya Baba mwenye nyumba kufa Dada yako mwenye asili ya kiunguja hapendwi na watoto.. kitu alichowaghadhabisha ni kuuza mali za familia kwa mahawara zake wa Umangani...watoto wemekuja juu hawamtaki ndani ya familia na alichofanya ni kumfuata mlima mananasi mmoja kaka wa marehemu kuja kuwakemea waendelee kumheshimu mama yao...
 
sasa kiongozi umeleta hoja hapa ili kutoa nafasi sie wengine tuchangie lakini umeishia kumtaja huyo ni dada mkubwa wako. kiongozi mbona kama unataka kutuingiza kwenye ugomvi wa familia yenu?
 
Back
Top Bottom