Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hii ni barua ya wazi ya mtu akimuandikia Dada yake.

Japo Dada yake huyo ni mtu mzima, ameolewa na ana watoto, hivyo kwa watoto wake wanamwita Mama na ana wajukuu ambao wanamwita Bibi, lakini kwa sisi wa rika lake, wale watu wa 60s, huyu kwetu ni dada yetu mkubwa!, hivyo hili ni bandiko la kikubwa!.

NB: Ukiona halijatajwa jina lolote zaidi ya Dada Mkubwa, nakuomba na wewe usitaje jina lolote!.


Soma: Rais Samia aligoma alipoambiwa atoke ili wajumbe wapige kura na kumpitisha. Hii ina maanisha CCM wengi hawamtaki?

Dear Dada,

Kiafrika kwa vile wewe ni dada mkubwa, Shikamoo Dada Mkubwa!.

Naomba Kuanza na Angalizo la Declaration of Interest.

Mimi ni mwana CCM na ni kada wa CCM, baada kuibuka kwa kada mpya ya uchawa na machawa, ukisifu tuu utanyooshewa kidole cha uchawa, naomba kudeclare inte mimi sio chawa wa Mama, wala bandiko hili sio bandiko la kichawa kutafuta shavu au kusaka fursa! Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!, bandiko hili ni bandiko la kaka mtu kumsaidia Dada mtu, asiwasikilize machawa kwenye kila kitu, kuna baadhi ya vitu machawa hawamsaidii na wengine wanampoteza kwa kumpotosha, hivyo hapa kaka mtu anamsaidia Dada mtu atende haki abarikiwe zaidi na zaidi!.

Mimi mdogo wako, nilibahatika kuwepo Dodoma kwenye ule Mkutano wetu Mkuu, na kushuhudia kilichofanyika, hivyo kwanza niungane na Watanzania wengine wote kukuhakikishia tuna imani kubwa na wewe, na hatuna shaka na uwezo wako kuendelea, hivyo nijiunge na wengine wote kukupongeza ulivyoaminiwa hadi watu kuhamanika na kukupitisha kwa kishindo kinyume cha katiba ya chama chetu, lakini kwasababu kilichofanyika kimefanyika kwa nia njema, in good faith, pokea pongezi zangu za dhati na pia pokea ushauri wangu japo sio lazima, kuufuata au kuutekeleza!.

Japo najua utakuwa unanifahamu kutokana na jina langu, si geni masikioni mwa wengi wale wa zamani waliokuwa wakiisikiliza RTD, nikaja DTV kwa waliowahi kuangalia kipindi cha Mada Moto Uchaguzi 95, ni mimi ndie nilikuja Zanzibar na kuyatangaza yale matokeo ya kweli ya Uchaguzi wa Zanzibar ile 1995. Kisha nikaendesha kipindi cha Kiti Moto, na sio vibaya nikijitambulisha tena kwako kwa kukumbusha tuu, kwenye mtandao huu wa JF, ni mimi ndiye mtu wa kwanza kukutambulisha wewe humu jf ile 2010 kabla hata hujateuliwa Waziri wa serikali ya JMT. New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!



Wakati tukililia haki hii kurejeshwa, huku CCM ndio kwanza...

Kama nilivyosema hakuna ajuaye sababu za yule Kaka yako kutwaliwa, ila inawezekana kilichotokea uchaguzi wa 2019 na 2020 kimechangia!.

Tunakushauri Dada Mkubwa usitupeke kwenye uchaguzi mkuu na hii sheria batili, muda wa kuirekebisha upo tena wa kutosha tuu, kitu muhimu ni uwepo wa utashi wa kisiasa, political will!.


Sasa tuje kwenye kilichofanyika Dodoma.
Kwanza naomba kukukumbusha tuu Dada kwa faida ya wengine.
Ibara ya 4 ya CCM inasema :


Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:

Binadamu wote ni sawa.

Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

Hivyo wana CCM wote ni sawa mbele ya chama.

Ibara ya 7 inasema
Raia yeyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18, anaweza kuwa Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi

Hii maana yake Chama cha Mapinduzi ni chama cha wote!.

Ibara ya 14, inazungumzia Haki za Wanachama


Mwanachama yeyote atakuwa na haki zifuatazo: -
  1. Haki ya kushiriki katika shughuli zote za CCM kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
  2. Haki ya kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya CCM pale ambapo anahusika kwa mujibu wa Katiba.
  3. Haki ya kuomba kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa CCM na ya kuchagua viongozi wake wa CCM kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na Taratibu za CCM.
Kwa ibara hiyo inamaanisha ule utaratibu wa mserereko, ni utaratibu batili, unaofifisha haki za wanachama kugombea nafasi za juu za uongozi, na haupo mahali popote kikatiba, ndani ya katiba ya CCM.

Kwa vile wewe uliingia kwa kudra tuu bila kusailiwa, na hii kwako awamu ya kudra inahesabika ni awamu yako ya kwanza, awamu yako ya pili ya 2025-2030 unapaswa kuendelea kwa mserereko.


Kwa vile dhima ya mserereko ni kuepuka duplicity kwa rais ambaye amekwisha sailiwa, wewe hapo mwanzo hukusailiwa, na kufuatia your wonderful performance, wana CCM katika umoja wetu kupitia Mkutano wetu Mkuu kwa kauli moja tumeamua ni wewe tuu, na tumekupitisha, bila kujaza fomu, bila kusailiwa na bila kupigiwa kura! .

Japo kwa mujibu wa Ibara ya 100 (2)ya katiba ya CCM, Mkutano Mkuu una mamlaka yote ya kufanya jambo lolote, Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa utakuwa ndicho Kikao Kikuu cha CCM kupita vyote na ndicho kitakachokuwa na madaraka ya mwisho.

Lakini kama hilo jambo limewekewa kanuni na utaratibu wa jinsi ya kufanyika, utaratibu ni huu
Ibara ya 101 (4) inauruhusu Mkutano Mkuu, Kubadili sehemu yoyote ya Katiba ya CCM kwa uamuzi wa theluthi mbili za Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka Zanzibar.

Mfano halisi ni mgombea urais wa JMT, lazima ajaze fomu kuomba, ajadiliwe na secretariat, apendekezwe na Kamati Kuu, ateuliwe na Halmashauri Kuu na kuchaguliwa kwa kura na Mkutano Mkuu, Mkutano huo Mkuu hauna mamlaka ya kufanya vinginevyo, mpaka kwanza kutengua vifungu hivyo vilivyopo ndipo kisha kulipitisha jambo letu hilo lifanywe vinginevyo!.

Pale Dodoma, hakukuwepo azimio lolote la kutengua kwanza kifungu chochote cha katiba, taratibu na kanuni, kwa mujibu wa ibara ya 101 (4)ndipo azimio la kumpitisha kwa utaratibu mpya likapitishwa.

Sasa CCM kama Chama ndicho kimeshika hatamu kuiongoza serikali, kama kinaweza kuikiuka katiba yake kwenye jambo kubwa kama hili, itakuwaje kwa katiba ya nchi?.

A Way Forward

  1. Katiba ya nchi, ndio sheria mama ya nchi hii, katiba zote za vyama lazima zifuate sheria mama, ule utaratibu wa mserereko wa CCM, ni kinyume cha katiba ya nchi, na kinyume cha katiba ya CCM, Dada naomba ukiondoe, ukubali usailiwe tuu na tutakupa kura zote!.
  2. Kufuatia kazi kubwa, nzuri na iliyotukuka iliyofanywa na Dada katika awamu yake ya kwanza, naamini hakuna mwana CCM yeyote atakayethubutu kujitokeza kumpinga.
  3. Na hata wakitokea, maadam tumeisha amua kwenda na Dada, a due process ifanyike, kumsaili na wote watakao jitokeza, chinjilia mbali baharini, litoke jina moja, tuu lipigiwe kura zote za ndiooo!.
  4. Hii due process ikifanyika, kiukweli Dada Mkubwa atabarikiwa na serikali yake itabarikiwa.
  5. Siku zote nimekuwa nikiwasisitiza Wapinzani kujifunza kutoka CCM, lakini leo nashauri hakuna ubaya chama changu CCM kujifunza kutoka Chadema kuhusu uchaguzi wa demokrasia ndani ya Chama kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama.
  6. Kwa mujibu wa katiba ya JMT, Dada Mkubwa anaweza kushauriwa tuu, hapaswi kulazimishwa kupokea ushauri wowote kutoka kwa yeyote, atafikia maamuzi yeye mwenyewe kama yeye, hivyo Dada Mkubwa, mwisho wa uwezo wetu ni ushauri tuu, uamuzi wa kuusikia na kuufuata ni wako, au kuusikia na kuuignore au hata kutousikia kabisa!.
Nahitimisha kwa ule utangulizi, kukuhakikishia Dada Mkubwa, Watanzania tunakupenda sana tuu, na tunakukubali sana. Kama ni wewe, uliyetueliwa na YEYE kuendelea 2025 -2030, then ni wewe tuu na hakuna mwingine yeyote zaidi yako!. Usiruhusu ule uhuni uliofanyika kwenye katiba ya nchi, kufifisha haki kuu ya kuchagua na kuchaguliwa, ukaingizwa ndani ya chama chetu cha haki, usiwasikilize wahafidhina, wewe shikilia kufuata katiba ya CCM na katiba ya nchi kwa kuruhusu ile the due process, kufanyika, you'll have everything to gain, and nothing to loose, na utabarikiwa sana!. Ukiendelea na kilichofanyika, you'll have everything to loose and nothing to gain!.
Nakutakia kazi njema
Mungu Ibariki CCM itende Haki.
Mungu Ibariki Tanzania.


Kaka yako mdogo
Paskali.
 
Wajumbe ñi wanafiki sana! Hela zimeisha ndo mnakuja kulia mtandaoni! Kwenye kikao si mlikuepo??

Mtu ambaye sio mnafiki ni mpina tu! Yeye hakuunga mkono kwa kutosimama kushangilia lakini wengine wote ni wachumia tumbo tu! Pesa ikiisha ndo akili zinawarudi
 
Nilishangaa sana katika wakati ambao Upinzani ulionekana uko vipande vipande, bado MTU anataka mseleleko?

Hata hivo nikaandika, Kosa lilelile alofanya JPM kufurahia habari za Machawa kumtaka aongoze milele, ndio hilohilo analofanya Dada yako yaan wote walifurahia uvunjajinwa Katiba.


Ukiangaliaa Kwa mbali sana, Utagundua Amejaa kwenye Mfumo wa Kuondoshwa kama ilivyokua .

Mungu anaweza kukupa Uongozi ila Kwa mpito tu yaan kipindi fulan, kikishapita, Usilazimishe .
 
Dodoma ulikuwepo na yalio jiri uliyashuhudia.
Hapa umekuja kuleta hoja ambayo pia umejitahidi kuzunguka weeeee hata sijui unahofia nini kumtaja wakati andiko lako nime muweka wazi.
Anyways........
Naskia unasubiria uteuzi, na kuna tetesi kwamba uliomba kuonana nae lakini black suits wakakutosa.
Nami sijataja jina kama ulivyo elekeza mkuu...😊
 
🤣🤣
 
Katika siku za karibuni walau Leo umeongea neno, heko.

Nachelea kusema chama hakina mwanasheria, kwani wakati mama alikua anafanya consultation alipaswa kutoa ushauri uliuleta hapa.

JK alijaribu kusema kitu lakini akaona umma unataka kumgeukia ikabidi atulie lakini maelezo mengi aliyoyatoa unaona kabisa alikua anaona ni kinyume lakini aliona isiwe taabu.

WanaCCM hawajapewa nafasi ya kugombea kama katiba Yao inavyosema bali wamepewa wenyechama.

Kwenye kikao hicho kilipiga marufuku watia Nia kupitia huko majimboni kutoa Nia ila wao na kupitishwa wamepitishwa, je hii sio double standard?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…