Dada yangu anapitia mateso makali sana sababu ya kijana wake kushika Dini hadi imemfanya amekuwa mjinga

Huyo ameshakuwa gaidi, mark my words. Soon atamwona Somalia na alshabab.
 
Andika tukuelewe bhana
 
Kitendo cha kutomuheshimu mama yake tu kishakosea. Tumeambiwa Tumuamini Mungu na Mtume wake na tuwaheshimu wazazi wawili.

Huyu hajasoma dini bali kakutana na vigenge vya wahuni

Na Allah Amhidi
 
Tunaweza kuwa tunamuonea huruma mother kumbe mtoto alishakuwaga mwehu kitambo tu ndiyo maana mzee akaachana naye.
 
Huyo dada mbona anajitesa mwenyewe? Mwambie kosa analo yeye kwa kutumainia mwanadamu hasa huyo Dr wake, yeye ilipaswa azae katika uwezo wake wa kulea kama jukumu lake na huku akipanga mipango yake ya baadaye, je huyo Dr angekufa mapema yeye akiwa amechukua hiyo mikopo kwani asingeishi?, Yeye alifanya nafasi yake kama mzazi Sasa kama huyo kijana hataki kazi Wala kujenga maisha yake na ameongea naye wakashindwa kuelewana amuache, na mwambie ukifanya wema huku unategemea malipo huwa hao unaowategemea wanaharibika ili upate fundisho.

Mtu kama huyo dada yako yupo tayari hata kuumiza watu wengine ili watoto wake wapate vitu vizuri na waje walimpe vitu vizuri ila angefanya kama wajibu wake huku akiwa rafiki na watoto au huyo mtoto hao watoto ndo wangebaki na hatia kukumbuka wema wa mama Yao, yeye hakupaswa kuweka mategemeo kwao na thamani yake ingeonekana tu.
 
Pepo zipo ktk chini ya nyayo za mama zenu
 
Wazungu walituweza, hasa ulimwengu wa tatu dini imenasa kwenye damu za watu. Unaacha utamadumi wako unafuata wa kizungu!!
Hakuna mzungu atakwambia huo upumbavu wa kumpigania Mungu ukakosana na wazazi na kuacha kazi uteseke mtaani. Dini za wazungu unazijua, dini ijenge shule na hospitali kisha ikusumbue kusoma na ukiajiriwa hospitalini ikushawishi uache?

Huo sio utamaduni wa kizungu haijalishi wana dini au hawana
 
Dini ya uislamu unamfunza muumini wake kumtii mola wake na mtume wake na kuwafanyia wema wazazi wawili (ikiwemo kuwatunza uzeeni kwao).
Dini ya uislamu inasisitiza wauminini wake kufanyakazi kwa bidii na kwa uadilifu.

Hapa nimeona tatizo lililoainishwa ni uvaaji wa kanzu kazini na kufuga ndevu. Huu sio ugaidi kwa mujibu wa uislamu au katiba ya nchi.
Hapa naona uelewa wa kijana kuheshimu mwongozo wa mavazi ya kitabibu ulikua mdogo, na kwa menejimenti ya hospitali huenda reaction yao kwa kijana ilikua kubwa na ya kumhukumu zaidi.
Huenda pia bada ya apo kijana akatengwa naye akaamua kuondoka jumla
na nafasi ya mzazi naye ikiwa laana na maneno makali ((kijana kaamua kupotea kabisa)).

Ni ushauri wangu kulingana mada jinsi ilivyowasilishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…