Daftari la mauzo linapendeza lakini ukweli ni kwamba hakuna faida. Mzigo niliojumua 3.8M na kuuza 8.2M umenipa faida ya laki 1 tu

Daftari la mauzo linapendeza lakini ukweli ni kwamba hakuna faida. Mzigo niliojumua 3.8M na kuuza 8.2M umenipa faida ya laki 1 tu

Kijijini kwa biashara hapafai. Labda uende sehemu za machimboni au vijiji maarufu kwa kilimo cha mazao ya biashara. Ila hivi vijiji vya kawaida watu wanajilimia kwa ajili ya msosi ni pagumu sana.
Umesema sahihi Mkuu šŸ™

Miaka fulani nilikuwa nachinja ng'ombe na kubadirishana na Mazao ya nafaka, hii ni baada ya kuwa kule Kijijini wengi walikuwa wanashindwa ku-afford kununua nyama Kwa bei ya kilo kilo

Hivyo solution ilikuwa nawapa kilo ya nyama then wananipa sado 3 za mahindi/mtama

Baada ya muda unaondoka na gunia kadhaa za mazao 😜
 
Nilianza mwaka jana
Sasa unataka upate faida papo kwa papo?

Yaani ndani ya mwaka mmoja biashara iwe inajiendesha? sawa kuna biashara inaweza kujiendesha kwa muda huo ila sio zote, zinahitaji muda.

Ipe muda na ongeza bidii kuisimamia, itaanza kujiendesha.

NOTE: Niliwahi fanya biashara nikaangukia pua[emoji2][emoji2][emoji2], pia nimefanya kazi kwenye biashara ya mtu, nilichojifunza ndio hicho nilichokushauri
 
Nje ya mada..

Hivi kumbe hutu tudada dada natotuonaga tunauza maduka ya simu full kuringa ringa na kuongea kwa nyodo, kujidai tu slay queen, kumbe tunalipwa laki tu kwa mwezi..?[emoji849]
Shangaa sasa...

Wanapendeza na vi uniform, vichipsi, juisi kwa pembeni ila yaliyojificha ni mengi
 
Umesema sahihi Mkuu šŸ™

Miaka fulani nilikuwa nachinja ng'ombe na kubadirishana na Mazao ya nafaka, hii ni baada ya kuwa kule Kijijini wengi walikuwa wanashindwa ku-afford kununua nyama Kwa bei ya kilo kilo

Hivyo solution ilikuwa nawapa kilo ya nyama then wananipa sado 3 za mahindi/mtama

Baada ya muda unaondoka na gunia kadhaa za mazao 😜
Bado kuna vijiji vingi wanafanya hivyo
 
Kwa hayo mahesabu unakubalije kuwalipa tra 250000. Tra unawalipa kutokana na biashara ilivyo. Mambo ya msiba usiyaingize kwenye biashara.
pole Yako huijui Tanzania ww..Kodi unakadiriwa before hata ujaanza hyo biashara..wao Wanasema Wana uzoefu na kila aina ya biashara na eneo la biashara..shikamo t.r.a
 
Labda t.r.a Wana miongozo tofauti kulingana na eneo..mm biashara zangu zipo kigamboni na zote nikikadiriwa Kodi hata kabla sijaanza...
makadirio ya kodi yanakuwepo kwa biashara zote, ila kama unatunza kumbukumbu wewe ndio unajikadiria ukishafanya mahesabu kama itaonekana unapata ziada utalipa zaidi ila kama unalipata pungufu utapunguza makadirio kwa mwaka unaokuja.
Ndio maana unaona mhindi ana biashara kubwa lakini analipa kodi kidogo sababu anajikadiria na kufanya mahesabu kwa wakati.
wewe ukipiga simu za kazi unaotumia toka mfukoni, ukila chakula wakati wa kazi huweki kumbukumbu, unanunua mafuta huweki kumbukumbu wala kudai risiti.
 
Kwakua ushajua expenses zako ni zipi kwa mwaka sasa inabidi ukaze ujue utauza mzigo wa kiasi gani kwa mwaka ili utengeneze faida kubwa either mara mbili ya hzo expenses zako..

Cha kufanya hapo kikubwa anza kucheza na bei zako unazouza, tafuta watu wataokupa huo mzigo kwa bei nafuu kidogo lakini pia jitahidi sana kwny kujitangaza ili uweze kupata wateja wengi, hii itakusaidia sanaa..[emoji871]
 
Ukweli mkuu mauzo yako yapo chini ya 25k kwa siku, hivyo kwa biashara yeyote ile haya sio mauzo mazuri,
Pambana kuongeza mauzo ufike japo 50k ila sio hayo 25k na unasema biashara imenoga
 
Kwa hayo mahesabu unakubalije kuwalipa tra 250000. Tra unawalipa kutokana na biashara ilivyo. Mambo ya msiba usiyaingize kwenye biashara.
TRA wana njia 2 za kukadiria kodi. Kwanza ni mtu anayetunza kumbukumbu/hesabu pili ni mtu asiyetunza.

Sasa jamaa inaonekana hatunzi so wanamkadiria kutokana na uzoefu wao TRA.

Angekua anatunza hesabu zake angelipa kodi ndogo sana!
 
Kuna siku dukani nimepokea msg ya Silent Ocean mzigo umefika natakiwa nilipie kama 1.7m na kwa bahati mbaya kwa target zangu nilidhani utachelewa kwahiyo kwa hiyo siku sikuwa hata na laki kwa sababu ya kununua stock. Wakati ninawaza yule binti akaniuliza vipi mbona kama unawaza.. nikamjibu mzigo umefika na leo sina hela ya kuutoa. Akaniuliza ni Tsh ngapi nikamjibu. Nikashangaa ananiambia nimruhusu aende nyumbani kuniletea hizo pesa. Nilishtuka na kumuuliza mara tatu kama yuko serious. Baada ya muda karudi na hela. Hiyo ndo siku nilielewa kwanini anko wangu aliniambia USISHINDANE NA DADA YAKO. Huyo binti hakudumu sana kazini alikuja kuolewa na kuachishwa kabisa kazi.
Siku nyingine usilipe pesa kubwa kama hiyo kwa agent bila ku verify vipimo mwenyewe.

Mimi walinikadiria 1.8mil nikafunga safari kwenda dsm tukapima na tape measure nikiwa naona kumbe watu wao wa china waliover estimate! Badala ya 1.8mil nikalipa 1.3mil! Nika save laki5 nzima!
 
Back
Top Bottom