Elections 2010 Daily News: Slaa will not be the fifth president of Tanzania!

Elections 2010 Daily News: Slaa will not be the fifth president of Tanzania!

Hapa ndipo nilipokuwa napataka..yaani NINA HASIRA MPAKA NASIKIA KUTETEMEKA! Tutakutana October 31, 2010!
 
Wanangu hata msiogope, ndo kwanza wanatupa hasira ya kuona kwamba neno CHANGES linatoka kwenye dictiionary linaingia mtaani, waache tuu tunawakomesha kwenye kiboksi 31st .
 
Mkuchika tena?achukue action kwa nani. umewahi kuona kesi ya nyani inapelekwa kwa tumbuli?

apewe presha kisha ionekane kama ataleta unafiki au la
hawa jamaa wanadhidi kujifunua, walichemsha pingamizi la chadema dhidi ya Kikwete, sasa ngoja tuone watafanya nini kuhusu dailynews
 
hasira hadi vidole vinashindwa kuandika, Rev yuko wapi atoe maombi?
 
I am really shocked with a complete lack of professionalism on the part of the Daily News Editor. By declaring that Dr. Slaa will not be the fifth President of our country it shows the Paper knows the election outcomes. It means that the entire campaigning exercise is a charade and wastage of peoples' time. This means Tanzanians are not participating in a democratic exercise but in a political gimmick. One would have expected that Daily News of all papers, would be unbiased but alas the paper is 100% in support of CCM. The Editor has even the audacity to say that Slaa will not be the fifth president and it can be quoted on that. This is not a professional editor but a zealot who is all out to save his or her skin. Chadema should take action against this editor an lodge a formal complaint before the Media Council. This is because an editorial is considered stance of the paper which means a lot of thought has gone into it. This is not something to let go. It demands immediate action.
 
Ni lazima Chadema kudai kufukuzwa kazi mara moja kwa Mhariri wa Daily News alichokiandika kimekiuka kila mizani yote ya uandishi. Inawezekana vipi gazeti la serikali likasema kuwa mtu fulani ambaye anagombea Uraisi wa nchi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yetu kuwa hawezi kuwa Raisi. Kauli hii inaamaanisha kuwa ama zoezi zima la uchaguzi ni kiini macho na hivyo Watanzania wanapotezewa muda wao au nchi yetu haina lengo la kujenga demokrasia ya ushindani wa kisiasa. Kitendo cha Mhariri huyku kuandika kwa jaziba na kiwehu kinathibitisha wazi kuwa gazeti hili pamoja na Habari Leo ni vyombo vya uzushi vya CCM na si vyombo vya serikali ya Watanzania. Kitendo cha Mhariri huyu ni lazima kilaaniwe kwa nguvu zote na kila mtu mwenye mapenzi mema ni nchi yetu. Nipenda kuhitimisha kwa kusema Daily News haina Mhariri bali mnazi na mwandishi uchwara. Mtu huyu na utawala mzima wa Daily News pamoja na Habari Leo ni aibu kubwa kwa taifa letu. Washindwe na waendelee kushindwa.
 
Hakuna atakayelifungia Daily News, Mkuchika atakuja na spins zake za ajabu kama alivyokuja Tendwa na spins zake about JK kuvunja sheria za uchaguzi. Naamini kilichopo hapa ni watanzania kuonyesha maajabu kwa kuiadhibu CCM kwa kuinyima kura. Kisha tuone hiyo Daily News itafanya kazi kwa ridhaa ya nani.
 
Mhariri anaitwa MKUMBWA ALLY. Huyu anafahamika sana kwa kula RUSHWA, na ni kati ya wahariri waliopo kwenye payroll za mafisadi. Haishangazi kuona mafisadi hao hao wakimtumia kuua taaluma yake kwa kuandika ujinga kama huu. Kwa maoni yangu, huyu ana kesi ya kujibu. Nitashangaa sana iwapo hakutakuwa na hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yake. Daily News, Habari Leo na Mtanzania/Rai wasi-underrate intelligence ya Watanzania.
 
Wameshapata nyeti jinsi wizi utakavyofanyika, kwa hiyo wana uhakika!
 
Mwaka huu patakuwa hapatoshi..... Hili ni gazeti la umma lina andika habari za kichochezi kiasi hiki? hii inaweza kuleta matatizo... Mali ya umma inatumika kama mali ya chama, haya ndio matumizi mabaya ya vyombo vya umma wanavitumia kujilinda na kueneza propaganda zao za kizamani..

Hakika Chadema imewashika pabaya wanabaki kutapatapa tu.Ni kweli waliendesha Poll na niliziona na nika vote kwa Slaa baada ya mda walisitisha hilo zowezi.

Ukweli utajulikana October 31
 
msiichukie CCM chukieni viongozi wabaya wa CCM, CCM is just a name it can sound so sill for someone who gets disappointed whenever hears the name CCM, when life started CCM was not there, we should have to learn that life can go on no matter the party exists or what,''' CCM is not my mother''
 
Just for curiosity, haya hayawezi kuchukuliwa kama maoni ya mhariri na si ya gazeti. Please nisaidieni. The auditor has completely lost the plot.
 
if DR SIRAHA will not be the next president and they believe on that..then they have to put back ''vote online" again and we will see who is gonna be the next president os TZ. My friends 100% these polls they real reflect the result of 31 october.mvua ya mawe inakuja . Lazima tuvapige kipunde du!!
 
Katika editorial yao wameandika hivi (miongoni mwa mengine):



Yaani Dailynews wanahakika (au wanahakikisha) kuwa Dr Slaa hawezi kuwa raisi wa Tanzania.
Wao ni nani kujua na kutangaza hili? Wameambiwa nini na serikali ambacho wananchi wengine hawajui?
Je tume ya uchaguzi inafanya nini kuhusu hili? BTW- Dailynews ni gazeti la serikali ya watanzania wote.

Dailynews linaendeshwa kwa pesa za kodi ya watanzania wote na sio ccm pekee.
Kama DTV walifungiwa kwa kutangaza matokeo ya Zanzibar mwaka 1995 kabla ya NEC,
Mbona Dailynews wamefanya hivyo hata kabla kula zenyewe hazijapigwa? na ni kwa mamlaka yapi?

Serikali inabidi ichukue hatua mara moja kuhusu hili, na vyombo vingine huru vya habari nchini inabidi vikamate bango ili Dailynews wapate staili yao kwa hili.

Takwimu msee!! Usishangae hayo yapöo dunia nzima, unachek Baromita yako inakueleza na wala si uchawi.
 
Kajibuni kwenye Tanzaniadaima kila mtu na uwanja wake wa kujidai ati!
 
Back
Top Bottom