Katika editorial yao wameandika hivi (miongoni mwa mengine):
Yaani Dailynews wanahakika (au wanahakikisha) kuwa Dr Slaa hawezi kuwa raisi wa Tanzania.
Wao ni nani kujua na kutangaza hili? Wameambiwa nini na serikali ambacho wananchi wengine hawajui?
Je tume ya uchaguzi inafanya nini kuhusu hili? BTW- Dailynews ni gazeti la serikali ya watanzania wote.
Dailynews linaendeshwa kwa pesa za kodi ya watanzania wote na sio ccm pekee.
Kama DTV walifungiwa kwa kutangaza matokeo ya Zanzibar mwaka 1995 kabla ya NEC,
Mbona Dailynews wamefanya hivyo hata kabla kula zenyewe hazijapigwa? na ni kwa mamlaka yapi?
Serikali inabidi ichukue hatua mara moja kuhusu hili, na vyombo vingine huru vya habari nchini inabidi vikamate bango ili Dailynews wapate staili yao kwa hili.