Tuendeleee........
Ilifika saa saba na nusu tupo kiwanja na bro, nikamwambia siwez kuendelea kustay macho yani usingizi ulikuwa ushaanza kuniandama.
Bro alinambia kwamba leo haturud home tutalal hukuhuku. Nikamuliza kwanini ameamua vile si nikuharibu pesa tu wakati home ni karibu.
Alinijibu kwamba "dogo pesa ipo, ukiwa na pesa hayo mawazo ya kimaskini hayawezi kuja akilini mwako. Sometimes unatakiwa kubadirisha mazingira kulingana na mood ulonayo, akamalizia kwa kusema wewe enjoy na utafute pesa".
Yale maneno ya bro yalinivunja nguvu, nilikonekt na maneno ya Dokta siku Ile basi nikaona kama dunia ni uwanja wa mapambanno yani ili upate hitaji lako ni lazima ukomae.
Nikaitazama cm yangu hakuwa hata na dalili ay Mercy kunitafuta.
Nikaamua kufungua chats zangu za normal texts na Mercy nikazisoma zote nikamaliza nikarud za Whatsapp nikamaliza nazo nikabak nimejiinamia. Bro alinichukuwa kumbe alikuwa kashabook vyumba kitambo akanishika mkono akanielekeza chumba changu nikaenda kupumzika.
Mule room usingizi niliupata kwa mafungu mafungu yani nalala lisaa nashtuka, nalala tena dakika 45 nashtuka mpka ilafika asubuhi.
Kwakuwa kipindi cha kwanza chuoni kilikuwa ni saa4 na dk15 asubuh basi nilizuga room mpk saa 2 hivi then nikaanza kujiandaa. Nilienda pia room kwa bro kumbe alikuwa na manzi nilpishana naye mlangoni nilivomuona nikajuta kabisa huyu sio mpenz wake bali ni wale wa lipia kamata twende.
Tulipiga chama na mayai tukapanda kigari chetu tukasepa. Njiani nikamwambia bro kwamba alichokifanya ni kikubwa sana kwasababu kwa ule usiku wa jana endapo ningekuwa pekeangu room basi kuna hatihat ningejimaliza kabisa au ningehangaika sana room pekeangu.
Tulivofika geton bro alinambi nijiandae anipeleke chuo na gari.
Ilikuwa kama saa tatu na 40 kwahyo kudavulikuwa bado tukaamua kuzuga magetoni kwanza.
Muda ilipofika nilichukuwa vidaftar vyangu tukaanza safar mpka chuo. Bro alikuwa na kidem chake mwaka wa pili alikipitia mageton kwake tukaenda nacho. Nakumbuka tulifika tukakuta wanafunzi tyr wapo class. Ali-drive mpka karibu na venue, mimi na yule manzi wa bro tulishuka kila mmoja kaenda venue kwake.
Nilipoingia class wasera wakaanza kunizingua oya naona umeshuka na mtoto mkali mwanangu Mercy umepiga chini au sio, jamaa alivotaja jina la Mercy moyo wangu ulipasuka hakujua tu nini kilikuwa kinaendelea.
Kumbe Mercy naye aliniona wakat nashuka.
Gari anaijua na mwenye gari anamjua lakini yule binti ndo alikuwa hamjui.
Nilitaka kwenda kumsalimia Mercy mahali pale amekaa lakini moyo ukanizuia nikavunga na kujikaza kiume.
Katikati ya kipindi nikasikia kama mesej imeingia katika cm yangu. Nikaona kwanza Mungu kwamba Ile mesej tafadhari iwe ya Mercy maana nipo hoi sina nguvu zakuemdelea kukomaa.
Kutoa cm Bwana kweli Ile mesej ilikuwa ni ya Mercy ilisomeka "yani tayari umepata kidem kweli wewe mwanaume ni Malaya"
Nilikuta kwanini bro alimpitia yule dem wake japo yeye ndo kafaya Mercy kanitafuta.
Nikimjibu "tusome kwanza kama utahitaji maelezo kuhusu huyo dem utanambia baadae nikueleze" Mercy hakujibubtena.
Kipindi kikaisha nikatoka nikaenda pembeni kulikuwa na vimbeeta nikakata nachezea cm yangu. Nilistukia namuona Mercy kafika kimbwetani nilipo, akanisalimia kisha akakaa.
Mercy ni mschana mwenye akili na mwenye huruma sana na nitampenda mpka naingia kaburini sijawahi kukutana na mwanamke wa vile.
Mercy alinishika mkono mmoja huku akiniangalia hakuwaza watu walokuwa wanapita kando yetu.
Aliniomba msamaha kwa kumfukuza na akasema kwamba alikuwa a hasira juu ya Tecra na wala si Dokta ndo aliyemoa ujasiri ule.
Ndugu zangu machozi yalinilenga kidume mzima lakini nikajikaza nikaona Mercy angeniona mimi kavu kulia lia kama mzungu.
Hatujakaa sawa cm ya Mercy ikaita kuangalia ni Dokta, ebana sisi wanaume ni ving'ang'anizi ila Dokta alizi na jeuri ya pesa ikanifanya nimuone mwenye ROHO mbaya sana. MERCY alivoona ni Dokta ndo anapiga aliikata na kusonya kabisa. Sasa nikamwambia so bora tumblock tu ili asizngue tena, Mercy alikubali tukamblock pale pale.
Tulienda kunywa juice na chapati cafe tukarudi venue kwa ajili ya kipindi.
This time tulikaa sehem moja na Mercy hii ni kawaida yetu toka first year.
Basi mambo yangu na Mercy yalirudi kuwa poa tukawa tunaishi vzr tu kama mwanzo.
Niliwambia yule Dokta ana ROHO mbaya. Ilikuwa hivi....
Ilikuwa ni week imepita baada ya kumblock. Tulikuwa week ya mwsho ya kuingia darasani then iingie week ya maandalizi ya UE. Nilimwambia Mercy achunge tusivurugane tukafeli akanihakikishia yeye yupo serious na nisiwe na wasiwasi.
Mwisho wa hii wiki tulikuwa nayo nakumbuka tulikuwa tunasomea kimbwetani. Ghafla cm ya Mercy ikaita kuchek namba ngeni akapokea na kuweka loud speaker. Kuskia saut nibya Dokta yani niliishiwa nguvu ndugu zangu. Nikajiuliza hivi huyu Dokta hajaona madem wengine ila ni Mercy wangu tu au ni shetan anaingilia mapenz na masomo yangu ili nifeli. Mercy akamuliza yeye nani akajibu Dokta, Mercy akamwambia shida nini, Dokta kasema ameamua kumchek amsalimia na akasema ni ushamba alivomblock basi Mercy alikasirika akakata cm.
Hatujakaa sawa mesej ikaingia kwa Mercy kuchek ni muamala wa tigopesa tsh 110k. Hafu ikaingia nyingine kaandika, mchukue huyo dogo mkanunue mahitaji yenu ya magetoni mwenu mnapojifichia.
Kweli pesa ni kitu cha ajabu sana, niliwaza nikasema inamaana mule magetoni sisi tunajificha sio nyumba za kuishi zile, nikawaza tena kwahiyo mimi naitwa dogo mbele ya mpenzi wangu.
Nikasubiri Mercy aseme nini juu ya ile pesa hafu mimi ndo niongee. Mercy alikuwa kimya nikamuliza what is next juu ya hii pesa kajibu niseme mimi.
Mimi kwa Ile hasira nikasema hii pesa mrudishie mbele yangu naona irudishe hapahapa nashuhudia.
See you there..........
===
Muendelezo soma
Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy