Muendelezo..........
Kesho yake tuliamka chuo kwenye paper na mtihani ulikuwa unaanza saa mbili kamili yani moja na nusu tulikuwa tayar kwenye chumba Cha mtihani.
Tulifanya paper tukamaliza, tulivotoka nikamchekua Mercy kwenda cafe kunpata tea ili tuendeleee kujiandaa na ppaer jengine jioni.
Week Ile ilokuwa imepita home walinitumie pesa kama 165k, nkatoa 45k nimpe Mercy kwa ajili ya Ile calculator.
Lengo langu Mercy asione kama vile pesa ya Dokta ndo imemnunulia calculator.
Nilivompa Ile pesa aliikataa akasema niiweke tutaitumia lakini nikagoma nikaongea kwa ukali "ichukue hii pesa". Mercy akapokea kaweka kwenye handbag.
Tukiwa cafe Mercy akasema "yani baby hili somo la leo mimi nishasup yani sijui niliandika manini". Nikamwambia kama atasup basi ni kwa uzembe kwasabb nilikuwa nishamhakikishia kwamba mimi simcheat ila yeye alikuwa haniamin nafikiri kilichomvunja moya kabisa ni ile text ya yule mjinga Mercy fek.
Nikajitahid sana kumrudisha Mercy kwenye pace tukasoma na jioni tukakaa pamoja kwenye paper na tukafanya vizur tu. Paper lilipoisha tukajikusanya, baiki yetu tukarud magetoni. Kipindi cha paper kulikuwa hakuna kugegedana mpaka paper liishe.
Sasa akili yangu ikawa makini sana juu ya nini kinaendelea kati ya Mercy na Dokta nikiangalia Mercy haniambii kama Dokta anamtafuta, nikapanga nisubir mpka hiyo j5 nione ile pesa ikishatumwa Mercy atanambia au vipi itakuwaje.
Mpaka hapa wadau nilikuwa nishaanza kuona nashindwa kuzuia Mercy asiwasiliane na Dokta nikawaza nimuache tu nisimfatilie maana niliona kumfatilia kwangu ndo kulikuwa kunaibua mambo mengine mengi na ya kuharibu sio kujenga.
Sasa nikajiapiza sitamuliza Mercy kuhusu Dokta labda yeye ndo anambie na sitamuliza kuhusu ile pesa japo swala la pesa nilikuwa najua mimi tu na Mercy fek.
Nikakumbuka kuwa kunahaja ya kumtafuta Mercy feki nimsiaitizie asimtafute Dokta na tushajua kwamba kampiga mshindo wa laki tano na Dokta kastukia mchezo na hawez tena kutuma Ile hela.
Mercy fek akaniahid kwamba hatomtafuta Dokta nisiwe na wasiwasi, bas nikawa nimemzima Mercy feki kwa dizain hii. Ila baadae mtakuja kuona Dokta alikuwa anawasiliana na Mercy fek na nadhani alimla.
Basi kesho yake ilikuwa j4 na tulikuwa na paper moja, tulienda tukafanya paper then tukabak chuo kujisomea kwasbb kesho yake ambayo ilikuwa j4 tulikuwa na papers 2 asubuhi na jioni.
Sikutaka kuwa karibu na sm ya Mercy kwani niliamua kujizima data yani nisimfatilie Mercy had kuhusu Dokta maana niliona kumfatilia kwangu ndo kulikuwa kunaibua mambo mengine mengi na ya kuharibu sio kujenga.
Tulirud mtaani na sikufika kwa Mercy tuliagana njia panda mimi nikaenda kwangu na Mercy akaenda kwake kwasabb tulitoka chuo tushakula dinner.
Kesho yake j5 ndo siku Dokta alikuwa anatuma Ile pesa, nikaamka nikajiandaa nikampitia Mercy tukasepa chuo.
Tulipiga zile papers vizur tu ile siku ikaisha tukazuga chuo kidogo then tukarud magetoni.
Mpka muda ule Mercy hakuwa amenambia chochote kuhusu pesa kutoka kwa Dokta wala kunigusia chochote kuhusu Dokta.
Nikaanza kuingiwa na baridi maana kwa nilivokuwa naona Dokta aliuwa serious na ni lazima ile pesa angeituma.
Niliamua kumuaga Mercy nikasepa kwangu, nilipofika kwangu nilikuwa na mawazo sana kwamba Dokta hajatumaaa au katuma Mercy kaisigina na mguu.
Sikupata majibu sahihi, nikakumbuka kesho kulikuwa na paper gum somo lenye mambo mengi ma calculation ya kutosha (somo ya Biochemistry) wanaolijua washanielewa, kuna kutafuta ma rancidity, percentage of saturation na mengine mengi. Basi nikajifua pale nikapiga maswali mawili matatu then nikajiridhisha kwamba nimeiva then nikamchek Mercy nimtakie usikute mwema.
Nilimcheki tukapiga stor kidogo then nikalala.
Kesho yake kama kawaida tukaenda kupga lile paper la Biochemistry na ijumaa hatukuwa na mtihani.
Tulipomaliza paper tulikaa chuo kuzuga na vistor stor na Mercy.
Uvumilivu ni kama ulinishinda nikamuliza vipi Dokta anasemaje.
See you..........
====
Muendelezo soma
Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy