Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Stay patient
Hata Bila Patient hivi unafahamu kukosa Imani kwako kutoka kwa Mercy aliyekupenda kulitengeneza Fear ya kuachwa na hiyo ndo ilifanya Ajibandue taratibu bila wewe kujua..

Ile Glue aliyokuwa nayo mwanzoni iliondoka kutokana na uoga wa Maumivu ambayo angeyapata kama angekukosa..

Ndo ilipelekea hata ukifanya kosa dogo ana hisi na yeye anao uwezo wa kukulipiza ili na wewe uumie au usikie maumivu kama yeye aliyosikia..
Hiyo ni simple tu hapo dakari hakuuhusika..
Hata kama angetokea mwanaume mingine kuonyesha anamjali na kumpenda angemchukua tu

Hiyo Ni Logic simple sana kuijua mpaka hapo haihitaji umalize story..

Mpaka ulipofikia tayari Huyo.msichana ameshaweka maumivu moyoni hata kama asipokuonyesha ila alihifadhi ili aje akuonyeshe
 
Mmmh kweli wanawake tunapenda vitu vya kijinga lakini sio kupanda baiskeli[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Dogo nakulaumu sana, ulikuwa na njia shortcut sana ya kumaliza hili sekeseke, ungeweza kukata mahusiano ya Dr. na Mercy, na mahusiano yako na malaya wako wa nyuma, ungemwingia Mercy kwa gia ya kubadili namba zenu za simu basi
Namba ya Mercy mwenyewe alidai home kwao wasingemuelewa na ndugu zake wengi wameizoea ile kwahyo wazo la kubadili line halikumuingia akilini na aliona haina haja
 
Les goo........

Cm ya Mercy ilipoita Mercy akaitoa tukaona ni namba ngeni lakini nikakumbuka ni kama ile ya Dokta
Mercy akapokea akaweka loud speaker, ikasikika saut ya kiume "Mercy mbona texts na cm zangu hujibu" basi pale pale nikampokonya Mercy cm nikaikata.
Mercy akasema yani huyu Dokta sijui hata ameona nini kwangu kwingine haoni maana kaniganda hatari.
Tulikuwa kwenye ugomv lakini nilisahau kabisa kwamba nilitakiwa kuendelea kujielezea kwa Mercy kuhusu Ile text ya Mercy fek mjinga yule.

Cm ya Mercy nilikuwa nayo bado, nikajiuliza kwahiyo Mercy fek kaamua kunikomoa haendelei tena kuwasiliana na Dokta mpka Dokta kaamua kumtafuta Mercy kupitia line yake halisi.
Nikaona kabisa mpka Dokta kaamua kumtafuta Mercy og bas walikuwa na mawasiliano mazuri na Mercy fek na usikute wamepanga mambo mengi tayar.

Yale mawazo yalinifanya niamue kubadiri umuzi kama ifuatavyo.
...nimchek Dokta kupitia namba og ya Mercy na nimwambie kwamba asiitumie tena Ile line ya Mercy fek kwani ilikuwa ni ya dharula tu na kwanzia hivi sasa anitafute kwa line yangu og na asjibu wala kupokea cm za ile namba nyingine (ya Mercy feki). Nilimtahadharisha kwamba anaweza kutafutwa maana Ile namba ni ya rafiki yangu na rafiki yangu anajua kinachoendelea kati yetu Mercy og na Dokta) kwahyo anaweza kufanya kama ku-overtake.

Niliamua vile kwasababu...
1. Sikutaka ukarbu uendelee kati ya Mercy fek na mimi.
2. Niliona kuna kila dalili za mission kubuma na endapo Mercy atasanuka basi ataniona mimi hamnazo.
3. Nilihitaji kuona msimamo wa Mercy katika mapenz yetu maana nilikuwa tyr nishaanxa kunusa dalili mbaya huko mbele.

Nilitumia mbinu ya kuomba nitumie dakika katika cm ya Mercy niongee na maza nimkumbushe pesa ya matumizi na niongee naye kuhusu swala la likizo kama nitaenda au vipi.
Nilifanya vile ili nipate muda wa kuwasiliana na Dokta.
Nikatoka nje mbali kidogo ili Mercy asinotice kwamba sikuongea na cm maana nisingeweza kumpigia Dokta na sauti yangu ya kiume, nilipanga nimchatishe tu.

Kabla ya kufanya vile nilimchek kwanza Mercy fek ili nimwambie asijarbu kumtafuta Dokta tena maana issue ishajulikana itakiwa soo zaid na tutaonekana matapeli. Lengo ni ili nipate kumrudisha Dokta kwa Mercy og pasipo kusanuka kwamba kulikuwa na mchezo unaendelea.
Mercy fek akasema poa, lakini naona kanitumia texts nying na kapiga sana mimi nilikuwa mbali na cm nilikuwa na bwana wangu. Nikasema poa wewe usimtafute zingatia hilo.
Nilimtafuta Dokta kwa mesej yeye akapiga nikakata nikamuandikia tuchat maana nipo discussion si unajua kesho paper.
Basi akaelewa nikampanga vile vile nilivojitaji na akasema hatoitumia tena ile namba.
Ghafla katuka mesej "ile laki tano uloomba ya kod na mahitaji yako mengine na nauli nitakutumia cku ya j5".

Wazee nilistuka nikajisemea asee kuna watu wanajua kutumia fursa yani Mercy fek alikuwa tyr kashamuingiza kwenye line mbaba wa watu ampigie pesa yote Ile.
Nikaona nasisi wanaume na maboya sana yani show hujapewa bado ila ushajicommit kuhonga moka laki tano.
Hii kitu ilinifanya nizid kumuona Dokta ni bogus na swaga ni zero kwake. Basi nikamjibu sawa kwaheri tutawasiliana kesho ngoja nijiandae na mtihani.

Sasa hapa nikawaza what is next maana nishawakonect Mercy wangu na Dokta, na Mercy wangu hajui kuwa yeye na Dokta mambo ni mazur je Dokta akimtafta Mercy itakuwaje?
Sikutaka kuumiza kichwa sana nikarud zangu ndani. Huwa nafutaga namba nazopigaga kupitia namba ya mtu mwingine na Mercy anajua kwahyo so rahis kuangalia call history na kuuliza mbona sioni namba uloipigia kwasababu anajua Huwa mafuta.

Basi tukazuga pale Mercy akapika tukala japo alikuwa bado na hasira sana. Hii siku kiukweli Mercy hakuwa poa na nilimsihi sana awe sawa asijaki kwani mimi simsaliti lakini Mercy alisema "mtihani wa kesho ni wa organic chemistry nahisi nitaenda kufeli na nikipata sup somo la kesho jua chanzo ni wewe" na of course kweli hii ndo sup pekee Mercy aliipata tukiwa chuoni. Mimi sikubahatika kupata sup yani kifupi nilitoka na clean sheet.

Nilimsihi sana Mercy asitangulize kufeli na tukawa tunapiga msuli wa mwsho mwsho lakini Mercy hakuwa pale kbsa akawa ananambia kwahyo hilo rungu jana umepiga nalo huyo malaya au sio. Duh nikaona mambo yanarud upya nikamuomba Mercy mini niondoke tu lbda asipiniona atakuwa sawa.
Mercy alijibu we sepa, basi nikachukua uamzi wa kufutika pale kwa Mercy kuelekea magetoni kwangu.

Jamani see you later ndo kumekucha saiz asubuhi.........
Wewe ulikuwa unatumia akili yako kuwaza upumbavu. Dah! Ulikuwa mpumbavu kinoma
 
Muendelezo..........

Kesho yake tuliamka chuo kwenye paper na mtihani ulikuwa unaanza saa mbili kamili yani moja na nusu tulikuwa tayar kwenye chumba Cha mtihani.
Tulifanya paper tukamaliza, tulivotoka nikamchekua Mercy kwenda cafe kunpata tea ili tuendeleee kujiandaa na ppaer jengine jioni.
Week Ile ilokuwa imepita home walinitumie pesa kama 165k, nkatoa 45k nimpe Mercy kwa ajili ya Ile calculator.
Lengo langu Mercy asione kama vile pesa ya Dokta ndo imemnunulia calculator.
Nilivompa Ile pesa aliikataa akasema niiweke tutaitumia lakini nikagoma nikaongea kwa ukali "ichukue hii pesa". Mercy akapokea kaweka kwenye handbag.

Tukiwa cafe Mercy akasema "yani baby hili somo la leo mimi nishasup yani sijui niliandika manini". Nikamwambia kama atasup basi ni kwa uzembe kwasabb nilikuwa nishamhakikishia kwamba mimi simcheat ila yeye alikuwa haniamin nafikiri kilichomvunja moya kabisa ni ile text ya yule mjinga Mercy fek.
Nikajitahid sana kumrudisha Mercy kwenye pace tukasoma na jioni tukakaa pamoja kwenye paper na tukafanya vizur tu. Paper lilipoisha tukajikusanya, baiki yetu tukarud magetoni. Kipindi cha paper kulikuwa hakuna kugegedana mpaka paper liishe.

Sasa akili yangu ikawa makini sana juu ya nini kinaendelea kati ya Mercy na Dokta nikiangalia Mercy haniambii kama Dokta anamtafuta, nikapanga nisubir mpka hiyo j5 nione ile pesa ikishatumwa Mercy atanambia au vipi itakuwaje.
Mpaka hapa wadau nilikuwa nishaanza kuona nashindwa kuzuia Mercy asiwasiliane na Dokta nikawaza nimuache tu nisimfatilie maana niliona kumfatilia kwangu ndo kulikuwa kunaibua mambo mengine mengi na ya kuharibu sio kujenga.

Sasa nikajiapiza sitamuliza Mercy kuhusu Dokta labda yeye ndo anambie na sitamuliza kuhusu ile pesa japo swala la pesa nilikuwa najua mimi tu na Mercy fek.

Nikakumbuka kuwa kunahaja ya kumtafuta Mercy feki nimsiaitizie asimtafute Dokta na tushajua kwamba kampiga mshindo wa laki tano na Dokta kastukia mchezo na hawez tena kutuma Ile hela.
Mercy fek akaniahid kwamba hatomtafuta Dokta nisiwe na wasiwasi, bas nikawa nimemzima Mercy feki kwa dizain hii. Ila baadae mtakuja kuona Dokta alikuwa anawasiliana na Mercy fek na nadhani alimla.

Basi kesho yake ilikuwa j4 na tulikuwa na paper moja, tulienda tukafanya paper then tukabak chuo kujisomea kwasbb kesho yake ambayo ilikuwa j4 tulikuwa na papers 2 asubuhi na jioni.
Sikutaka kuwa karibu na sm ya Mercy kwani niliamua kujizima data yani nisimfatilie Mercy had kuhusu Dokta maana niliona kumfatilia kwangu ndo kulikuwa kunaibua mambo mengine mengi na ya kuharibu sio kujenga.

Tulirud mtaani na sikufika kwa Mercy tuliagana njia panda mimi nikaenda kwangu na Mercy akaenda kwake kwasabb tulitoka chuo tushakula dinner.
Kesho yake j5 ndo siku Dokta alikuwa anatuma Ile pesa, nikaamka nikajiandaa nikampitia Mercy tukasepa chuo.

Tulipiga zile papers vizur tu ile siku ikaisha tukazuga chuo kidogo then tukarud magetoni.
Mpka muda ule Mercy hakuwa amenambia chochote kuhusu pesa kutoka kwa Dokta wala kunigusia chochote kuhusu Dokta.
Nikaanza kuingiwa na baridi maana kwa nilivokuwa naona Dokta aliuwa serious na ni lazima ile pesa angeituma.

Niliamua kumuaga Mercy nikasepa kwangu, nilipofika kwangu nilikuwa na mawazo sana kwamba Dokta hajatumaaa au katuma Mercy kaisigina na mguu.
Sikupata majibu sahihi, nikakumbuka kesho kulikuwa na paper gum somo lenye mambo mengi ma calculation ya kutosha (somo ya Biochemistry) wanaolijua washanielewa, kuna kutafuta ma rancidity, percentage of saturation na mengine mengi. Basi nikajifua pale nikapiga maswali mawili matatu then nikajiridhisha kwamba nimeiva then nikamchek Mercy nimtakie usikute mwema.

Nilimcheki tukapiga stor kidogo then nikalala.

Kesho yake kama kawaida tukaenda kupga lile paper la Biochemistry na ijumaa hatukuwa na mtihani.

Tulipomaliza paper tulikaa chuo kuzuga na vistor stor na Mercy.
Uvumilivu ni kama ulinishinda nikamuliza vipi Dokta anasemaje.

See you..........


====
Muendelezo soma Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy
 
WANAWAKE NI WATU WA AJABU SANA, UNAONA KIPINDI HIKI KUNA UHABA WA SUKARI WEWE KIDUME UNAWEZA UKAWA NAPESA ZAKO ZA KUTOSHA ILA UPO BIZE NA MAMBO YAKO HAUPAMBANII MKEO APATE SUKARI NDANI KWASABABU YA KUADIMIKA KWAKE MTAANI, UNAWEZA UKAJA KUSTUKA MKEO KAGAWA MBUSUSU KWA FALA MMOJA TU KISA KILO MBILI ZA SUKARI ILI AANDAE KEKI YA BIRTHDAY YA MWANAE, HAWA WATU NI SHIDA.
 
1. Wanawake tunapenda vitu vya kijinga kama kupanda baskeli
2. Kushona sare za vitenge chuo
3. Kula Chama na mayai
4. Juice na chapati kwa ajili ya lunch

Mkuu najifunza vingi sana kupitia uzi wako
Hata wew kuna baadhi ya mitego ya wanaume ulinasa kwa vitu vya kijinga sana sema huwez kuweka wazi tu hapa jamvini
 
Back
Top Bottom