Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Enhee!, Sasa unaanza kuwa na maamuzi ya kiume...
 
Uko sahihi.
Although cheating ina consequences psychologically kwa wote ila mwanamke akicheat ni tofauti na mwanaume akicheat.
 
Mdogo wangu achana na hilo lipumbavu haya mambo sometime inabidi uwe na roho mbaya kima kama huyu mercy sio wa kumchekea mshenz kama huyu ashapigwa mimba huko saiz ndio anajileta kwako aisee huyu angejichanganya kwangu ningemuonyesha show Q**mmke
 
Kama mmekubaliana na mage kufunga ndoa fanyeni haraka, hicho Ndio kitamfanya mercy apunguze kukusumbua. Kwa Sasa anaamin anaweza kupindua meza maana hamjafunga ndoa. Funga ndoa fasta umsaidie na mercy aanze kumove on bila wewe
 
Ulifeli sana,we hugongi unanyonya chuchu,piga dyudyu
 
Kama mmekubaliana na mage kufunga ndoa fanyeni haraka, hicho Ndio kitamfanya mercy apunguze kukusumbua. Kwa Sasa anaamin anaweza kupindua meza maana hamjafunga ndoa. Funga ndoa fasta umsaidie na mercy aanze kumove on bila wewe
Ni sawa kabisa
 



Tuendeleee..........

Kwanza kabisa kuna kitu ni kama ninakihisi, ni kwamba ninahisi Mercy aliwambia kwao kwamba mwanaume mwenye mtoto ni mimi na siyo Dokta.
Nahisi pia kawadanganya kwamba nimekengeuka sitaki kumuoa mtoto wao kwasababu sasahivi hili sekeseke hadi wao wazaz wa Mercy wameingilia kati. Na bila shaka kama Mercy angekuwa kawambia ukweli kwamba yule mtoto sio wangu ni wa Dokta basi wazazi wangedili na Dokta na siyo mimi.

Mercy namuona ni kama anatumiwa na shetani kunivurugia mambo yangu.
Mercy amepanga mipango ya kuhamia Tanga mahali nilipo ili awe karibu na mimi. Nilijaribu sana kumpiga biti nyingi za makatazo juu ya mpango wake kwani ataniharibia mipango yangu na Mage na ukizingatia Mage tayari tupo naye vizuri sana yani mapenzi ni moto sana saivi.

Mage ni mwanamke mzuri na mpka sasa siamini ni kwanini nilimkuta Mage akiwa single Hana mtu najiuliza je alikuwa anawakataa watu au alikuwa hatongozwi maana Mage ni wife material haswa. Ila nachokiamini Mage hakuwa single ila kaamua kuweka utoto pembeni na kuwa na mimi 100%.

Nahisi pia ni mpango wa Mungu Mage kuwa namimi kwasababu amekuja wakati sahihi wakati ambao nilikuwa nahitaji sana mtu wa karibu ambaye ataridhia kuwa namimi no matter what.

Yale matatizo ya moyo niliyoyapataga
nahisi bado kwa kiasi kidogo yapo bado japo kadri siku zinavokwenda yanazidi kupotea na nazido kuimarika.
Kuna muda nahisi hasira kwa vitu vidogo vidogo, pia kuna muda nadhoofika moyo unakuwa unapiga kwa nguvu mpka nikiweka kiganja juu juu tu katika sehem ya moyo nakuwa nafeel moyo unavopiga kwa nguvu Sasa hii hali inanifanyaga nidhoofike na pia nakuwa na shorten breath.

Mage tayari anafaham hali yangu halisi na ananipa kampani ya dhati sana mpka naona kama vile ni special from God.

Kuna siku nipo na Mage nakumbuka ilikuwa siku ya j pili weekend maana Mage anakuwaga na nafasi ya kuja kunitembelea siku za weekend.
Siku hiyo tupo bed tunapiga stors meseji ya Mercy ikaingia "DeMostAdmired mimi nawewe tulipanga mengi makubwa, kilichotokea mimi kukusaliti mpka kuzaa na Dokta ni kama ajali tu na sikufanya kwa kukusudia naomba unielewe. Dokta nimeshampiga marufuku hanitafuti tena na Hana kabisa mazoea na mimi. Nisamehe kila siku nakuomba msamaha siyo kwamba sitongozwi natongozwa ila nahitaji kuolewa nawewe niambie nini nifanye ili urudishe moyo wako kwangu mimi nipo tayari".

Hii mesej hata Mage ilimpa mashaka japo tayari ameshamzoea Mercy na vimbwanga vyake lakini siku hii Mage alisimama akanambia " baby huyu mwanamke sasa naona anavuka mipaka, mimi sipo tayari kuona unatumiwa mamesej ya kubembelezwa namna hii na wewe ni binadamu kuna kipindi kitafika utaanza kuregea na kuanza kumpenda huyu Mercy"

Mage alinambia either tubadirishane laini yeye atumie yangu namimi nitumie yake au lah basi nivunje hii yangu nisajili nyengine ili Mercy asinipate tena.
Niliona option ambayo kidogo ni nzuri ni hii Option ya pili japo niliwahi kubadirisha laini lakini alipata namba yangu kupitia watu tulomaliza nao chuo ndo walimpa namba yangu na wembe ukawa ni uleule.

Nilimuahidi kwamba atulie mimi ni mwanamume ninaakiki timamu nafahamu Mercy siyo mtu mzuri kwahiyo asiwe na wasiwasi kabisa.
Alikubali japo kwa shingo upande

Siku hii Mage aliwaka sana mpka nikaona kama vile Mercy anaenda kuniharibia mipango yangu na Mage kwasababu mage tayari ameridhia tuanze taratibu za kutambulishana ili tuanze kuishi pamoja kama mume na mke na hapo baadae tufunge ndoa. Hii kitu bado naona ni mapema kwasababu ndo kwanza hata mwaka hatujamaliza.


See you........
 
utoto raha sana!
 
Wazazi wakikupigia wanasemaje?
 
Lamomy Bhana😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…