Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk Conrad Agonza Kahyoza amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salaam, leo Septemba 10, 2026, baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia askari wa Usalama Barabarani katika eneo la Lugalo, Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea Jumanne Septemba 8, 2026 saa 1:30 asubuhi katika Barabara ya Bagamoyo, Lugalo, wakati askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, F.8886 SGT Andrew, akitekeleza majukumu yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, askari huyo alikuwa akizuia magari yaliyokuwa yakitumia barabara ya huduma (Service Road) kinyume na utaratibu.
Matukio ya picha wakati alipofikishwa Mahakamani kusomewa shtaka moja la kushambulia mwili, katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Soma pia