Daktari Bingwa wa Mloganzila, Conrad Agonza, anayedaiwa kumshambulia Trafiki afikishwa Mahakamani, 10/09/2026

Daktari Bingwa wa Mloganzila, Conrad Agonza, anayedaiwa kumshambulia Trafiki afikishwa Mahakamani, 10/09/2026

Wanamng'ang'ania kweli kweli.....Kama mzaha atapigwa hukumu itakayobadilisha kabisa uelekeo wa maisha.Kwa ambao wanashangilia tusome hapa kuhusu Kanuni ya Adhabu inayohusu kumshambulia askari polisi.

  • Kifungu 243(b): Mtu yeyote anayemshambulia, kumpinga, au kumzuia kwa makusudi afisa yeyote wa polisi wakati anatimiza wajibu wake anatenda kosa la kisheria.
  • Adhabu: Mtu anayepatikana na hatia chini ya kifungu hiki anaweza kuhukumiwa kifungo cha jela cha hadi miaka mitano
Sasa umfunge daktari kama huyu upate faida gani, huyo sio chizi, lazima walikoseana mahali... Sisemi alikuwa sawa ila kulikuwepo na majibishano mpaka kupelekea kupigana. Hao wote ni watumishi wa serikalini, hekima itumike maisha yaendelee.
 
Mkuu;Mimi wala sihitaji kubishana na wewe.Mm nimekuonesha tu kwamba wakati mkiwa mnamshangilia Fahamuni kabisa kwamba Dakatri Bingwa anaweza kujikuta anabebeshwa miaka 5 bial kujali kama alinyang'anywa Mke au alinyang'anywa Funguo.Hayo mengine ni ya kwako na hisia zako ila Next time ukitaka kumpiga Askari hakikisha inakuwa ni self defence tena iwe nyumbani kwako n ni usiku na asiwe na silaha.
Utakuwa limbukeni wa sheria, hizo sheriq zimeandikwa sio maandiko matakatifu unazichukua kama zilivyo.

Ndio maana licha ya uwepo wa hizo sheria, bado kuna mawakili, kazi yao ni kumshawishi jaji au hakimu kama tukio lililofanyika ni kosa kweli au hapana.

Hapa habari sio kumshangilia daktari, ni kuchambua tukio lililotokea, ukija na habari yako ya kusema tunamshangilia daktari, basi nawe utakuwa unamshangilia askari bila kujua!.
 
Yaani sio anafikishwa mahakamani na kuhukumiwa, huyu ni wa kuonea huruma maana anaenda kufutwa udaktari
Kumpiga na tena ni mfanyakazi wa serikali hio sio miiko ya udaktari, kwa kweli ausahau.
Mwanzo wa maisha magumu
Wewe huna mamlaka au sio nabii wa kusema ANAENDA KUISHI MAISHA MAGUMU

punguza ushaur kwenye maisha ya WATU.

NB. From no where mtu timamu hawezi mpiga mtu bila kukerwa au kuchomozwa.. hao ma ASKARI MDEBWEDO wenye lugha chafu na wapenda rushwa amekutana na sizi yake
 
Kumbuka Hii kesi tayari Ina Public interest, Mwamba anaweza kupigwa Faini ama kifungo Cha nje ili kupunguza kelele Mitaani. Na kama ni kifungo Cha ndani hawawezi kumpa Miaka Gerezani.

All in all watamkuta na hatia..
Ndugu yangu Hii Public interest hii ndio inaweza hasa kumfanya atandikwa miaka mingi.Mimi ninafahamu jamaa yangu ambaye ameshatandika sana askari mpaka wana mjua wenyewe so hawahanagiki naye maana wanajua ni mtata na ana makosa mengi.Mara nyingi issue kama hizi zisipokuwa public huwa mnamalizana kituoni.Issue sasa ikishavamiwa na watu baki inakuwa sasa ni kisheria zaidi.Hakimu anaweza tu amua kukupa lihukumu la ajabu uhangaike nalo.Kama Daktari ukishakutwa na Hatia athari yake kwako ni kubwa sana.

Haya mambo yasikie tu kwa watu.Hapo alipo Dr.Akifikiria Outcomes alafu ukute ilikuwa ni minor issue ni lazima ajilaumu kwa Poor judgement.
 
Mimi Nina kaka askari ila alitimuliwa kazi kwa kumpiga MKUU WAKE WA KAZI OCD

brother angu yule ni Mtata tangia udogoni mwake fukuzwa sana shule mbambe

Akaenda police alikua ni askari haramia..

☺️😊 Alikua anapenda kuniambia Hawa ma bush lawyer KESI YA MFUKONI MWAKE NI KUMZUIA ASKARI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE. Hivyo jamaa ana kesi mbili MOJA KUMZUIA ASKARI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KESI YA PILI SHAMBULIO LA MWILI
Kesi ya kaka yako haifanani na tukio lililotokea Mwenge linalojadiliwa hapa .
 
Limbukeni wa sheriq, hizo sheriq zimeandikwa sio maandiko matakatifu unazichukua kama zilivyo.

Ndio maana kuna mawakili, kazi yao kumshawishi jaji au hakimu kama tukio lililofanyika ni kosa kweli au hapana.

Habari sio kumshangilia daktari, ni kuchambua tukio lililotokea, ukija na habari yako ya kusema tunamshangilia daktari, basi nawe utakuwa unamshangilia askari bila kujua!.
Kazi kweli kweli.Kwamba unafikiri sheria nimetunga mimi?Bwana Daktari angekuwa amemalizana kimya kimya angekuwa na uwezo wa kuondoka bila kesi.Shida sasa waliingia wanaharakati,mara sijui kapigwa yuko ICU mara hivi mara vile mpaka sasa imekuwa Issue kubwa wakati askari wanafahamu namna kazi zao zilivo na mavurugu na namna ya kuyamaliza.
 
Sasa umfunge daktari kama huyu upate faida gani, huyo sio chizi, lazima walikoseana mahali... Sisemi alikuwa sawa ila kulikuwepo na majibishano mpaka kupelekea kupigana. Hao wote ni watumishi wa serikalini, hekima itumike maisha yaendelee.
ingekuwa ugomvi wa baa na raia, wala hata asingekamatwa, ila unampiga polisi kabisa, ni ujinga wa hali ya juu
Mimi nina uwezo kupiga polisi wawili kwa wakati mmoja, yaani ninajiamni haswa napiga, lakini hapana ni kujitafutia majanga, bora hat aumtandike mwanajeshi kesi yako sio ngumu, mtasema ni masuala binafsi, ila unampiga polisi akiwa kazini, daah sijawahi kuona
 
Polisi huwa wanapigwa sana.Ila sasa mkishapigana hakikisha mnamalizana.Ama kwa kupigwa wewe au kwa kumalizana kiutu uzima.Ila Ukienda Mahakamani ni Kosa kubwa
 
ingekuwa ugomvi wa baa na raia, wala hata asingekamatwa, ila unampiga polisi kabisa, ni ujinga wa hali ya juu
Mimi nina uwezo kupiga polisi wawili kwa wakati mmoja, yaani ninajiamni haswa napiga, lakini hapana ni kujitafutia majanga, bora hat aumtandike mwanajeshi kesi yako sio ngumu, mtasema ni masuala binafsi, ila unampiga polisi akiwa kazini, daah sijawahi kuona
Hawa jamaa wakati mwingine wana maudhi sana na maneno ya kukera, huwezi kujua huyu daktari alikerwa na nini
 
Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk Conrad Agonza Kahyoza amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salaam, leo Septemba 10, 2026, baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia askari wa Usalama Barabarani katika eneo la Lugalo, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea Jumanne Septemba 8, 2026 saa 1:30 asubuhi katika Barabara ya Bagamoyo, Lugalo, wakati askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, F.8886 SGT Andrew, akitekeleza majukumu yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, askari huyo alikuwa akizuia magari yaliyokuwa yakitumia barabara ya huduma (Service Road) kinyume na utaratibu.

Soma pia
Mbona haonekani kuwa amevunjwa miguu na kutojiweza kutembea kama tulivyoaminishwa?
 
Wewe huna mamlaka au sio nabii wa kusema ANAENDA KUISHI MAISHA MAGUMU

punguza ushaur kwenye maisha ya WATU.

NB. From no where mtu timamu hawezi mpiga mtu bila kukerwa au kuchomozwa.. hao ma ASKARI MDEBWEDO wenye lugha chafu na wapenda rushwa amekutana na sizi yake

Kusema kuchokozwa ni utoto wa hali ya juu sana, au labda ndio akili ya mtu mweusi anadhani unaweza kusimama mbele ya hakimu kujitetea kusema ulichokozwa, aiseeee
Kutoka daktari, kuwa mfungwa na kutoka hujui mbele wa nyuma, na hapo hapo umefutiwa usajili wa kufanya kazi kama daktari ni maisha magumu sana kwa nchi za kiafrika, tena sana, ni sekunde kuwehuka
 
Kazi kweli kweli.Kwamba unafikiri sheria nimetunga mimi?Bwana Daktari angekuwa amemalizana kimya kimya angekuwa na uwezo wa kuondoka bila kesi.Shida sasa waliingia wanaharakati,mara sijui kapigwa yuko ICU mara hivi mara vile mpaka sasa imekuwa Issue kubwa wakati askari wanafahamu namna kazi zao zilivo na mavurugu na namna ya kuyamaliza.
Kuingia wanaharakati kunahusika vipi na kesi iliyopo mahakamani?

Hakimu hawezi kuacha kujadili matter iliyopo mbele yake aanze kuhangaika na wanaharakati, huko ni kuingiza siasa mahakamani.

Tatizo lako hili jambo unalichukulia kiushabiki ndio maana unaleta mambo yasiyohusiana na kesi yenyewe, ilimradi uiridhishe nafsi yako.

Au kuna sheria inayosema mwanaharakati akiingilia jambo, basi hakimu aongeze adhabu?!.
 
Hawa jamaa wakati mwingine wana maudhi sana na maneno ya kukera, huwezi kujua huyu daktari alikerwa na nini
Akili kubwa ni kujua wapi kuwa na self control
Huyu ni daktari mwenye miiko, alitakiwa kujua hivyo kuliko mimi
Huo ushahidi wa kusema nilikerwa labda utasikilizwa na mjumbe wa nyumba kumi, lakini mahakamani wanaangalia jinai, na kumpiga mfanyakazi wa serikali wa usalama mbele ya kadamnasi ni watamfanya iwe mfano kwa wengine
 
Back
Top Bottom