Daktari Bingwa wa Mloganzila, Conrad Agonza, anayedaiwa kumshambulia Trafiki afikishwa Mahakamani, 10/09/2026

Daktari Bingwa wa Mloganzila, Conrad Agonza, anayedaiwa kumshambulia Trafiki afikishwa Mahakamani, 10/09/2026

Kesi ya kaka yako haifanani na tukio lililotokea Mwenge linalojadiliwa hapa .
Sijasema ufanano ila nataka uelewe scenerio mbali mbali.
Mkuu wake wa kazi alikua na makosa ila kwakua OCD akamlalia na kufukuzwa kwa uonevu

Kwa jicho la sheria ASKARI police anaweza kua na makosa ndio ila AKALINDWA NA SHERIA KWA HARAKA DOCTA ANA KESI MBILI
Mosi KUMZUIA ASKARI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KAZII na PILI SHAMBULIO LA MWILI

All in all, Namtakia Kila lililo jema Daktari bingwa aweze kumaliza hii CHANGAMOTO na aweze kurejea kwenye majukumu yake.
 
Hii gari iliyo milango wazi ndio ya specialist? Au yake haipo pichani wakuu?
Hayo ndio maisha ya nchi yetu mkuu wataalamu kama hawa ni masikini
lqkini wabunge wa darasa la saba ni matajiri ajabu
mbuge analipwa mshara+posho mara 10 ya daktari bingwa wa Muhimbili

Alafu watu wakipata bahati wakaenda kusoma nje mfano marekani mnategemea huyu mtu atarudi au atakuwa mzalendo wa nchi yake akiludi atakuwa zumbukuku

serikali inatakiwa iwalipe vizuri sana hawa watu ikiwezekana walipwe sawa au karibu na wanasiasa
 
Hapa Kuna mambo mengi
Kuna sura ya jeshi la polisi

Iwapo atapewa hukumu dhaifu watu wataona kumbe ni rahisi kuwapiga na hakuna impact, hii itaweza kuzaa kwa matukio mengine zaidi.

Ikiwa atapewa hukumu ngumu, polisi watapata kiburi zaidi na kuona kumbe Dola inawajali.

Iwapo itaisha kwa kuogopa public
Maana jeshi la polisi litakuwa limetezwa na hadhi yake.

Iwapo hukumu yoyote itatoka maisha ya daktari yatakuwa yameharibika ikiwemo upotezaji wa kazi yake.

Kila upande mzani unapo lalia Kuna maumivu.
 
Kwa kweli hapa mje na utetezi wa kisheria ni jinsi gani huyu daktari anaweza kuchomoka kama kuna wanasheria humu.
Ushabiki hausaidii kabisa kesi yake, na hasa ushahidi wa tukio uko kila mahali kutokana na teknolojia ya utandawazi
Huyu hachomoki, na udaktari asahau hapa bongo hasa kwenye hospitali za serikali, labda baadae afanye magumashi ya kubadili jina apate usajili mpya afanye hospitali za vichochoroni
 
Security Guard
Receptionist
Cashier

Kuzibua machemba...nk
1-Security guard huuweka uhai wake rehani kwa ajili ya mali/nafsi za wengi hasa waajiri wao kwa ujira mbuzi.Huo ni wito unaosindikizwa na upendo.
2-Mapokezi-Hukutana na kila sampuli za watu wenye mchanyato wa hulka/tabia.Matusi,wajuaji,wenye dhihaka na dharau.Hutumia muda mwingi kwa malipo kidichu huku anapaswa kutunza siri na mipango ya watu wengi.Wito lazima ujiinue.
3-Mlipaji/mpokea fedha,huyo kazi yake kushika,kunusa,kulipa na kupokea mabulungutu ya mahela huku analamba vidole kutwa kucha kwa malipo hafifu na kuandamwa na tamaa za fedha za watu.Ni KAZI ya hatari inayoweza kumnyang'anya roho na moyo wake.Wito lazima ujiinue juu mawinguni.
 
1-Secirity guard huuweka uhai wake rehani kwa ajili ya mali/nafsi za wengi hasa waajiri wao kwa ujira mbuzi.Huo ni wito unaosindikizwa na upendo.
2-Mapokezi-Hukutana na kila sampuli za watu wenye mchanyato wa hulka/tabia.Matusi,wajuaji,wenye dhihaka na dharau.Hutumia muda mwingi kwa malipo kidichu huku anapaswa kutunza siri na mipango ya watu wengi.Wito lazima ujiinue.
3-Mlipaji/mpokea fedha,huyo kazi yake kushika,kunusa,kulipa na kupokea mabulungutu ya mahela huku analamba vidole kutwa kucha kwa malipo hafifu na kuandamwa na tamaa za fedha za watu.Ni KAZI ya hatari inayoweza kumnyang'anya roho na moyoewake.Wito lazima ujiinue juu mawinguni.
Ok Rudi kwenye maana ya wito ni nini?
 
Kuingia wanaharakati kunahusika vipi na kesi iliyopo mahakamani?

Hakimu hawezi kuacha kujadili matter iliyopo mbele yake aanze kuhangaika na wanaharakati, huko ni kuingiza siasa mahakamani.

Tatizo lako hili jambo unalichukulia kiushabiki ndio maana unaleta mambo yasiyohusiana na kesi yenyewe, ilimradi uiridhishe nafsi yako.

Au kuna sheria inayosema mwanaharakati akiingilia jambo, basi hakimu aongeze adhabu?!.
Haya bwana.Wacha niache washabiki muendele kushabikia.Ila Fahamu kwamba atakapofikishwa mahakamani kuna kauli inasemaga ili awe fundisho kwa wengine.Unajua maana ya kumfanya mtu awe fundisho kwa wengine wenye tabia za kupiga askari?Unafahmu kwa hadhi yake ya kuwa Specialist wa Internal Medicine wakitaka kumfanya mfano wanamfanyaje?Inawezekana wewe hujawahi pata kesi ambayo unakuja kugundua uzito wa kosa tayari ushalifanya na namna ambavyo huwa unatamani urudishe muda nyuma usirudie makosa.

Kwa sasa hivi fahamu tu kwamba Bwana Daktari yuko chini ya huruma ya Mahakama na Hakimu anaweza mpa adhabu yoyote ile kwa mujibu wa sheria inaweza kuwa miezi 6,mwaka au hata akapaewa kazi ya kufanya usafi polisi ila tu HILO ni KOSA KUBWA na sio kosa DOGO.Ukishaelewa hilo basi fahamu kabisa hakimu akiwa ameamka vibaya anaweza Mtandika miaka 5 amwache nayo ahangaike nayo kwenye RUFAA.

Jela sio sehemu nzuri kwa mtu aliyekaa Darasani akisome Udaktari mapaka anafikia hatua ya KUWA Specialist
 
Mpongeze ila sasa hapo alipo ameshasomeshwa sheria na akilini mwake anatamani hata kuomba msamaha ila sasa shida ni kwamba mnamshangilia sana na akishangiliwa anapewa mvua ya miaka.Au Hamjui mchezo wa siku hizi nchini?
  • Kifungu 243(b): Mtu yeyote anayemshambulia, kumpinga, au kumzuia kwa makusudi afisa yeyote wa polisi wakati anatimiza wajibu wake anatenda kosa la kisheria.
  • Adhabu: Mtu anayepatikana na hatia chini ya kifungu hiki anaweza kuhukumiwa kifungo cha jela cha hadi miaka mitano
Ni kawaida sana kwenye maisha tena maisha ya mwanaume.

Kwa nchi ambayo geshi la polisi liko juu ya sheria, Yule mhadhari wa UDSM alisema sisi sote ni wafungwa watarajiwa.
 
Wanamng'ang'ania kweli kweli.....Kama mzaha atapigwa hukumu itakayobadilisha kabisa uelekeo wa maisha.Kwa ambao wanashangilia tusome hapa kuhusu Kanuni ya Adhabu inayohusu kumshambulia askari polisi.

  • Kifungu 243(b): Mtu yeyote anayemshambulia, kumpinga, au kumzuia kwa makusudi afisa yeyote wa polisi wakati anatimiza wajibu wake anatenda kosa la kisheria.
  • Adhabu: Mtu anayepatikana na hatia chini ya kifungu hiki anaweza kuhukumiwa kifungo cha jela cha hadi miaka mitano
Pumbafu wewe na waliokutuma!
 
Back
Top Bottom