Daktari bingwa wa Watoto Kibosho, ajiua Kisa Msongo wa Mawazo

Mimi ni bodaboda. Nikiwa stressed sana huwa naanza kuwasimulia abiria wangu baadhi hasa wanawake kupata ushauri. Huwa inasaidia sana kupata relief. Na ikizingatia abiria kwangu hawajirudii maana ni bolt
Yah ukizungumza na watu sahihi inasaidia,angalau unapunguza vitu fulani

Ova
 
Miaka 30 anakuwa bingwa mmmmm sio rahis ufanis utakuwa zero
Inatakiwa awe bingwa baada ya miaka mingapi? Umefanya research miaka ya siku hizi watu wanamaliza shahada za pili za udaktari wakiwa na miaka mingapi?
 
  • Thanks
Reactions: apk
Daktari bingwa wa watoto kutoka Hospitali teule ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, Magreth Joseph Swai (30) ameripotiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya wa antena.
​
Akizungumza kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 10,2025 majira ya saa tatu kamili usiku katika makazi yake yaliyopo Longuo Kata ya Longuo,Tarafa ya Moshi Magharibi.

Amesema Marehemu alitumia waya wa ntena alioufunga kwenye nondo ya mlango wa chumbani katika nyumba aliyokuwa anaishi.

"Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na afya ya akili ambapo Marehemu alifunga waya huo kwenye nondo iliyopo juu ya mlango na kujitundika" alisema SACP Maigwa.

RPC Maigwa ameongeza kuwa marehemu alianza kuugua ugonjwa wa afya ya akili akiwa katika mafunzo kwa vitendo kama Daktari maalum wa watoto miaka minne iliyopita.

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo Mfanyabiashara mmoja mkazi wa Moshi,Msaranga Ronald Malisa (35) naye akiripotiwa kujinyonga Julai 10,2025 kwa shuka bafuni kwake kwa sababu zisizojulikana, miezi nane baada ya kufunga ndoa yake ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Julai 15,2025.

Elimu yake haijamsaidia!

Note: There is no genius in medicine.
 
Ila jamani she was cute 🥰. Yaani Mungu amsamehe dhambi zake huko aliko.
 
Back
Top Bottom