Daktari bingwa wa Watoto Kibosho, ajiua Kisa Msongo wa Mawazo

Daktari bingwa wa Watoto Kibosho, ajiua Kisa Msongo wa Mawazo

Daktari bingwa wa watoto kutoka Hospitali teule ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, Magreth Joseph Swai (30) ameripotiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya wa antena.
​
Akizungumza kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 10,2025 majira ya saa tatu kamili usiku katika makazi yake yaliyopo Longuo Kata ya Longuo,Tarafa ya Moshi Magharibi.

Amesema Marehemu alitumia waya wa ntena alioufunga kwenye nondo ya mlango wa chumbani katika nyumba aliyokuwa anaishi.

"Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na afya ya akili ambapo Marehemu alifunga waya huo kwenye nondo iliyopo juu ya mlango na kujitundika" alisema SACP Maigwa.

RPC Maigwa ameongeza kuwa marehemu alianza kuugua ugonjwa wa afya ya akili akiwa katika mafunzo kwa vitendo kama Daktari maalum wa watoto miaka minne iliyopita.

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo Mfanyabiashara mmoja mkazi wa Moshi,Msaranga Ronald Malisa (35) naye akiripotiwa kujinyonga Julai 10,2025 kwa shuka bafuni kwake kwa sababu zisizojulikana, miezi nane baada ya kufunga ndoa yake ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Julai 15,2025.


#Depression is real

#Msongo wa mawazo umejaa sana miongoni mwa watu wengi kwenye jamii zetu.

Ni muhimu sana kuchukua hatua mapema kukabiliana nao dalili zinapoanza.
 
Watu wabaya sana..huyo itakua ametupiwa "kitu" ...tuishi kimachale sana watu sio Wazuri kabisa. ..watu Wana Husda wivu sana na mafanikio ya watu
Kajinyonga kwa msongo wa mawazo na sio kutuliwa kitu, hujaisoma habari shekhe??
 
Back
Top Bottom