Daktari bingwa wa Watoto Kibosho, ajiua Kisa Msongo wa Mawazo

Daktari bingwa wa Watoto Kibosho, ajiua Kisa Msongo wa Mawazo

Kuna dada mmoja nilikutana nae hospital,hanijui simjui akaanza kunielezea matatizo yake tuliongea zaidi ya Lisaa kama watu tunaofahamiana,niliamua kumpa muda wangu ili atoe ya moyoni!!!!
Tatizo la depression ni kubwa ukipata nafasi ya kumsikiliza mtu msikilize Tu pengine unaweza kusaidia!!
 
Daktari bingwa wa watoto kutoka Hospitali teule ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, Magreth Joseph Swai (30) ameripotiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya wa antena.
​
Akizungumza kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 10,2025 majira ya saa tatu kamili usiku katika makazi yake yaliyopo Longuo Kata ya Longuo,Tarafa ya Moshi Magharibi.

Amesema Marehemu alitumia waya wa ntena alioufunga kwenye nondo ya mlango wa chumbani katika nyumba aliyokuwa anaishi.

"Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na afya ya akili ambapo Marehemu alifunga waya huo kwenye nondo iliyopo juu ya mlango na kujitundika" alisema SACP Maigwa.

RPC Maigwa ameongeza kuwa marehemu alianza kuugua ugonjwa wa afya ya akili akiwa katika mafunzo kwa vitendo kama Daktari maalum wa watoto miaka minne iliyopita.

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo Mfanyabiashara mmoja mkazi wa Moshi,Msaranga Ronald Malisa (35) naye akiripotiwa kujinyonga Julai 10,2025 kwa shuka bafuni kwake kwa sababu zisizojulikana, miezi nane baada ya kufunga ndoa yake ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Julai 15,2025.

Kusali muhimu Dunia Ina mambo mengi na Siri nyingi, wapumzike wanapostahili
 
Itakuwa kapigwa chini na wanaume kadhaa kapata stress na sonona akaona ajiue and nothing else

WTF
 
Pale unapomuona mtu akitembea Kwa kujiamini lakini kwa ndani anakufa pole pole!

Hadi anafikia maamuzi magumu hakuna anaejua anachopitia!

Ndivyo ya kisasa yalivyo yenye maumivu ya kimya kimya na hasira kali zikiwaka kifuani!!

Rip boss!
 
Back
Top Bottom