Daktari bingwa wa Watoto Kibosho, ajiua Kisa Msongo wa Mawazo

Daktari bingwa wa Watoto Kibosho, ajiua Kisa Msongo wa Mawazo

Kabisaa mkuu.. nilikua sio muda najiangalia picha zangu za sasa na za miezi 9 kurud nyuma hukoo, dahh!! Nilikua nimezeeka sana aisee 😂.
Watu wana stress bila kujua kuwa wanatembea wana mizigo, wanafikiri ndio majukum ya kiapo kumbe una pambana na drama za mtu mzima mwenzio
Kabisaa mkuu.. nilikua sio muda najiangalia picha zangu za sasa na za miezi 9 kurud nyuma hukoo, dahh!! Nilikua nimezeeka sana aisee 😂.
Watu wana stress bila kujua kuwa wanatembea wana mizigo, wanafikiri ndio majukum ya kiapo kumbe una pambana na drama za mtu mzima mwenzio
Hongera mkuu kwa kuvuka salama,kuna mdada kazini almanusura awe Chizi,alikuwa amevurugwa kiasi hawezi hata kuandika jina lake,ukimuita anakuagalia Tu mpaka umstue🙁🙁🙁🙁
 
kumbi za starehe kumejaa mashetani ya kukuongezea matatizo. kimbilia kanisani, kaokoke, ukienda kanisani ukakuta walokole wanaimba, wanaomba na kutoa machozi usifikiri siku zote wamezama kiroho, wengine wapo pale kupunguza uchungu uliojaa moyoni, wakimaliza ibada wapo wepesiii. pia, ukiwa kwenye kundi la watu wa Mungu, pale Mungu anapowatembelea watu wake lazima na wewe utakutana naye tu. kumbuka Neno la Mungu linasema "walipo wawili watatu wamekusanyika kwa Jina langu mimi nipo papo hapo katikati yao", usipende kukaa peke yako, nenda kaabudu na wenzio, mkiwa mmekusanyika kwa ajili ya kumwabudu Mungu, kuimba na kusifu Mungu, ameahidi atakuwa katikati yenu. nani asiyependa Mungu awepo kwenye kusanyiko ambalo yeye ni mmoja wao? na Mungu akiwepo,stress itapotea. ushauri tu.
Huko unaenda kujiongezea hofu kwa maneno ya kusadikika, unapoenda kiwanja unakuwa huru, na mwili unakuwa uko huru kwa mazingira husika; ukitoka hapo unakuwa na furaha ya kutosha.​
 
Daktari bingwa wa watoto kutoka Hospitali teule ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, Magreth Joseph Swai (30) ameripotiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya wa antena.
​
Akizungumza kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 10,2025 majira ya saa tatu kamili usiku katika makazi yake yaliyopo Longuo Kata ya Longuo,Tarafa ya Moshi Magharibi.

Amesema Marehemu alitumia waya wa ntena alioufunga kwenye nondo ya mlango wa chumbani katika nyumba aliyokuwa anaishi.

"Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na afya ya akili ambapo Marehemu alifunga waya huo kwenye nondo iliyopo juu ya mlango na kujitundika" alisema SACP Maigwa.

RPC Maigwa ameongeza kuwa marehemu alianza kuugua ugonjwa wa afya ya akili akiwa katika mafunzo kwa vitendo kama Daktari maalum wa watoto miaka minne iliyopita.

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo Mfanyabiashara mmoja mkazi wa Moshi,Msaranga Ronald Malisa (35) naye akiripotiwa kujinyonga Julai 10,2025 kwa shuka bafuni kwake kwa sababu zisizojulikana, miezi nane baada ya kufunga ndoa yake ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Julai 15,2025.

Matarajio na uhalisia ni kama mashariki na magharibi
 
Sifikirii Kama huyo amefika viwango vya kuitwa Daktari bingwa
Ni daktari bingwa ukisoma historia kamaliza degree 2019 na msc 2024 ya paediatrician . Kwenye page Facebook ya paediatrician wamempost . Mimi nilisimamiwa research ya msc na mru tunayelingana age yeye alikuepo PhD holder at 20s. Ila ilikuepo ni asian countries na supervisor wangu alikuepo kichwa balaa.
 
Huko unaenda kujiongezea hofu kwa maneno ya kusadikika, unapoenda kiwanja unakuwa huru, na mwili unakuwa uko huru kwa mazingira husika; ukitoka hapo unakuwa na furaha ya kutosha.​
hakuna amani ya kweli inapatikana nje ya Yesu Kristo, na Yesu hapatikani bar wala kwenye club. Yesu alisema, amani niwapayo mimi sio kama ile ulimwengu uwapayo. Ndugu yangu, Yesu Kristo akiingia moyoni mwako, unapata amani ambayo haielezeki na hakuna stress wala depression itapambana na amani ya Yesu. ndio maana unaona waumini wa gwajiboy wapo tayari hata wapigwe virungu na polisi ila wasali kwa sababu wanajua thamani yake.ninyi watu wa club na dunia hamuwezi kujua tunachoongea hadi mumpate Yesu. nafasi ni sasa.

na unapoongea na sisi usifikiri unaongea na watu ambao hawajawahi kupata stress, au hatujawahi kwenda club,kwamba tulijidanganya uzinzi, pombe na miziki ya duniani ni furaha yetu, tulipokuja kukutana na Yesu, hakika yote yale tunayaona kama mavi ukilinganisha na amani ya Yesu Kristo. hata kama hauna sumuni akiwa ndani yako, amani ipo palepale, na ukiwa na hela pia ipo palepale.
 
Back
Top Bottom