Daktari bingwa wa Watoto Kibosho, ajiua Kisa Msongo wa Mawazo

Wengi hawakunielewa nilipoamua kuacha kila kitu na kuhama kabisa Jiji, ila haya mambo ya ndoa na mahusiano mwisho wa siku nilikua najiona kabisa nafika huko. Imagine ndoa miezi mi 4 unaenda mwanaume kujinyonga. Soo sad kwakwel.
 
Daktari bingwa wa watoto kutoka Hospitali teule ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, Magreth Joseph Swai (30) ameripotiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya wa antena.
​
Akizungumza kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 10,2025 majira ya saa tatu kamili usiku katika makazi yake yaliyopo Longuo Kata ya Longuo,Tarafa ya Moshi Magharibi.

Amesema Marehemu alitumia waya wa ntena alioufunga kwenye nondo ya mlango wa chumbani katika nyumba aliyokuwa anaishi.

"Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na afya ya akili ambapo Marehemu alifunga waya huo kwenye nondo iliyopo juu ya mlango na kujitundika" alisema SACP Maigwa.

RPC Maigwa ameongeza kuwa marehemu alianza kuugua ugonjwa wa afya ya akili akiwa katika mafunzo kwa vitendo kama Daktari maalum wa watoto miaka minne iliyopita.

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo Mfanyabiashara mmoja mkazi wa Moshi,Msaranga Ronald Malisa (35) naye akiripotiwa kujinyonga Julai 10,2025 kwa shuka bafuni kwake kwa sababu zisizojulikana, miezi nane baada ya kufunga ndoa yake ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Julai 15,2025.

Je ana familia ya kisiasa?
 
Daaaah binti kaondoka na utamu wake
 
Tena hayo masuala ya ndoa ndo yanaumiza wengi!!!
Kabisaa mkuu.. nilikua sio muda najiangalia picha zangu za sasa na za miezi 9 kurud nyuma hukoo, dahh!! Nilikua nimezeeka sana aisee 😂.
Watu wana stress bila kujua kuwa wanatembea wana mizigo, wanafikiri ndio majukum ya kiapo kumbe una pambana na drama za mtu mzima mwenzio
 
Kumbi za starehe zinasaidia sana kuimarisha afya ya akili, upatapo nafasi tembelea huko hasa ile mida ya usiku mkali.
Utagundua uwepo wako una thamani sana.​
kumbi za starehe kumejaa mashetani ya kukuongezea matatizo. kimbilia kanisani, kaokoke, ukienda kanisani ukakuta walokole wanaimba, wanaomba na kutoa machozi usifikiri siku zote wamezama kiroho, wengine wapo pale kupunguza uchungu uliojaa moyoni, wakimaliza ibada wapo wepesiii. pia, ukiwa kwenye kundi la watu wa Mungu, pale Mungu anapowatembelea watu wake lazima na wewe utakutana naye tu. kumbuka Neno la Mungu linasema "walipo wawili watatu wamekusanyika kwa Jina langu mimi nipo papo hapo katikati yao", usipende kukaa peke yako, nenda kaabudu na wenzio, mkiwa mmekusanyika kwa ajili ya kumwabudu Mungu, kuimba na kusifu Mungu, ameahidi atakuwa katikati yenu. nani asiyependa Mungu awepo kwenye kusanyiko ambalo yeye ni mmoja wao? na Mungu akiwepo,stress itapotea. ushauri tu.
 
Daktari bingwa wa watoto kutoka Hospitali teule ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, Magreth Joseph Swai (30) ameripotiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya wa antena.
​
Akizungumza kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 10,2025 majira ya saa tatu kamili usiku katika makazi yake yaliyopo Longuo Kata ya Longuo,Tarafa ya Moshi Magharibi.

Amesema Marehemu alitumia waya wa ntena alioufunga kwenye nondo ya mlango wa chumbani katika nyumba aliyokuwa anaishi.

"Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na afya ya akili ambapo Marehemu alifunga waya huo kwenye nondo iliyopo juu ya mlango na kujitundika" alisema SACP Maigwa.

RPC Maigwa ameongeza kuwa marehemu alianza kuugua ugonjwa wa afya ya akili akiwa katika mafunzo kwa vitendo kama Daktari maalum wa watoto miaka minne iliyopita.

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo Mfanyabiashara mmoja mkazi wa Moshi,Msaranga Ronald Malisa (35) naye akiripotiwa kujinyonga Julai 10,2025 kwa shuka bafuni kwake kwa sababu zisizojulikana, miezi nane baada ya kufunga ndoa yake ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Julai 15,2025.

Mzuri PC ya kwenda Daa, Yaani Mungu amsamehe kwa Kujiua.
 
Back
Top Bottom