Daktari: Ulaya kamwe hawang'oi meno, wanakarabati

Mkuu tatizo kama hilo nilipata mwaka 2008 nilipata ajali ya pikipiki kati ya meno haya mawili ya mbele, moja lilikatika kipande kwa upande mmoja, siku lilipo katika hadi ile nerve ilikuwa exposed, sikwenda hospital likapona ila sasa kumbe kupitia ile nerve likaanza kuoza, likajenga tundu katikati, likaendelea mwaka huu likaanza kupasuka, maana limeoza ndani, kutokana na vhakula kuwa kinaingia, nikaamua kwenda hospitali, nilienda hospitali moja ipo maeneo ya posta nikaambiwa hapo nitoe niwekewe jino jipya kwa tsh 800000/= mbali na matibabu na vitu kama ivo. Nikasepa.

Nikaenda Regency, wakanambia jino 250000/= ni lazima ning'oe kisha nikae na pengo mpka lipone alafu kwa miezi kama sita nitapewa jino la bandia la kuvaa na kutoa kisha baada ya hapo nichonge permanent kama nitapenda na ila permanent ni kama laki 400k hivi.

Nikaondoka nikaenda hospital nyingine kariakoo ki dispensary kidogo hivi, Dr akasafisha lile tundu, akanichoma sindano, akanipiga pamba ndani, kisha akanambia niendr baada ya siku tatu atoe ile pamba, ang'oe jino, achukue kipimo anichongee la bandia la kudumu, bei yake tsh 70 elfu kufanyiwa kila kitu, nikaodoka

Nilipofika home sikuridhika maana kila hospital nilipita nikakuta maelezo mapya, kesho yake nikaelekea msasani kuna kio hospital cha meno pale, nilipofika nikamkuta yank mdogo tu nilipomuonesha jino, kwanza akanikaliza akaleta vitabu vya meno akaanza kunipa shule, jinsi jino lilivyo na linavyo athiriwa na kwa kuangalia jino langu nini kinaonekana, akanipiga x ray.. Akaona root yake ilivo

Baada ya hapo akatoa pamba niliowekewa k. Koo, aksema hapa hujafanya kitu, akasafisha jino lile tundu akafungia dawa, akajengea jino la cement akanipa vidonge akaniambia kanywe dose ikiisha uje. Siku iyo iyo akachukua kipimo cha jino.

Baada ya wiki nikarudi, akafumua ile cement nikafanyiwa root canal treatment, akasugua lile jino bila kung'oa mpk likabaki usawa wa fisi, akapachika jino jipya la kudumu la bandia, akanambia anisafishe kinywa, akasafisha jino moja moja.

Tulikaa masaa 6 akinishughulikia, akamaliza akanipa dawa na mouth wash, nikaondoka akanichaji kwa kila kitu tangu siku ya kwanza tsh 140000/= lak na arobaini tu. Nikashangaa. Nikawa mpya kinywani mpk leo

Yule jamaa ndie my best dentist nilieona anachukua muda wake mwingi kwa mteja kuelimisha na kumhudumia, amekuwa kama rafiki saizi na huwa nikija dar hapo ananiomba nipite anicheki meno

Unaweza ku-pm contacts zake na wapi yupo huyu dr.
 
Pole mkuu kwa matatizo. Nafurahi kwamba uliweza kupona. Uliponea wapi? Hapa hapa Bongo ama? Antibiotics zilitosha au ilibidi wafanye utaratibu mwingine?

Mambo haya sisi tulikuwa hatuyatilii maanani sana na jino unashughulika nalo wakati linakuuma otherwise unapeta tu. Sasa hali imebadilika na hata mfumo wa maisha yetu nao umebadilika. Ndo maana ikibidi ni lazima tuanze kuzingatia mambo kama

Nilitibiwa mbeya kwa Dawa na tatizo aliligundua Dr mabula specialist wa matatizo ya Moyo yupo mbeya maeneo ya sokomatola kuanzia wakati ule niko very serious kila baada ya miezi sita nafanya usafi wa meno yangu na kwa kuwa kuna watu huwa wana wamatatizo ya moyo but hawapati vipimo kama tabia ya Hospital nyingi za serikali na kupewa tu Dawa isiyotibu tatizo husika hvyo mara nyingi hupoteza maisha.
 
Sasa bongo hosp nzuri ya meno kufanya root canala na braces wapi wakuu?? Msaada
 
Hapa ntajifunza mengi...kuna mgojwa wa meno maeneo yetu hadi namuhurumia.
 
Mi naomba msaada kwa dentist yeyote kwani naona fizi(gums) zangu zinalika na kuisha mpaka meno ya nyuma yamesimama yenyewe sasa sijui nifanyeje
 
Hizo bei yaani hapa nna jino nalibembeleza.nikila sukari au kitu chochote cha ngano linauma. Nikila nyama kama ni ngumu ndo usiseme silaki usiku. Najipanga nipate bima ndo ning'oe.hela ndeefu ughaibuni
 
Nimeziba jino nikiwa england kwa pound 50 siku hiyohiyo nilianza kula lakini hapa bongo ni balaa wiki nzima huwezi kula.
 
Anayejua hospital nzur arusha inayosafisha meno na kuwa meupe anijuze
 
Mimi nang'oa jino kwa Dr Muya pale Kumbukumbu Morocco ,Kinondoni kwa bei ya kawaida tu lakini kwa utaalamu wa hali ya juu.
 
Mi naomba msaada kwa dentist yeyote kwani naona fizi(gums) zangu zinalika na kuisha mpaka meno ya nyuma yamesimama yenyewe sasa sijui nifanyeje
Kama upo Dar jaribu pale kwa Dr Muya Morocco Kinondoni karibu na makao makuu ya Airtel
 
Hizo bei yaani hapa nna jino nalibembeleza.nikila sukari au kitu chochote cha ngano linauma. Nikila nyama kama ni ngumu ndo usiseme silaki usiku. Najipanga nipate bima ndo ning'oe.hela ndeefu ughaibuni

we ka mm asee,,ni nouma
 
Wadau Hiyo teknolojia sio mpya hapa Tanzania,ipo kwenye hospitali nyingi tu za wahindi hapa Dar es salaam.Kuna ndugu yangu alikuwa na mawazo kama hayo lakini tiba ya namna hiyo ameipata hapa hapa Dar na huu ni mwaka wa 6 sasa sijamsikia akilalamikia jino.Tafadhari acheni kupotosha,Inawezekana kuwa hospitali zetu za taifa na za kiswahili na kisanii ndiyo majanga lakini utalaam huo upo hapa kwa muda mrefu sana.
 
Usiingize siasa katika kila kitu na always usijione kuwa ni victim wa mfumo tu. Change your outlook a little bit and take some personal responsibility. Jichunguze na uone wapi ulifanya maamuzi ambayo siyo sahihi at personal level; na unawezaje kujirekebisha. Kujiona tu wewe ni victim na kulaumu wanasiasa for everything won't help. You think the politicians care?

Hata huko Ulaya na Marekani ambako CCM haipo kuna wengi wanasugua visigino. Cha muhimu ni kutokata tamaa na kuchacharika regardless of the situation. Go be what you want to be. With a good mindset, creativity, hard work and good luck inawezekana. kuwalalamikia wanasiasa (whether CCM/CHDM or whoever will come haitakusaidia)

Excellent piece of advice. The minute you start blaming someone for your problems you are declaring defeat. The only person who can make you succeed is yourself. u only need Persistence, courage and open mindset towards life.
 
Mkuu tatizo kama hilo nilipata mwaka 2008 nilipata ajali ya pikipiki kati ya meno haya mawili ya mbele, moja lilikatika kipande kwa upande mmoja, siku lilipo katika hadi ile nerve ilikuwa exposed, sikwenda hospital likapona ila sasa kumbe kupitia ile nerve likaanza kuoza, likajenga tundu katikati, likaendelea mwaka huu likaanza kupasuka, maana limeoza ndani, kutokana na vhakula kuwa kinaingia, nikaamua kwenda hospitali, nilienda hospitali moja ipo maeneo ya posta nikaambiwa hapo nitoe niwekewe jino jipya kwa tsh 800000/= mbali na matibabu na vitu kama ivo. Nikasepa.

Nikaenda Regency, wakanambia jino 250000/= ni lazima ning'oe kisha nikae na pengo mpka lipone alafu kwa miezi kama sita nitapewa jino la bandia la kuvaa na kutoa kisha baada ya hapo nichonge permanent kama nitapenda na ila permanent ni kama laki 400k hivi.

Nikaondoka nikaenda hospital nyingine kariakoo ki dispensary kidogo hivi, Dr akasafisha lile tundu, akanichoma sindano, akanipiga pamba ndani, kisha akanambia niendr baada ya siku tatu atoe ile pamba, ang'oe jino, achukue kipimo anichongee la bandia la kudumu, bei yake tsh 70 elfu kufanyiwa kila kitu, nikaodoka

Nilipofika home sikuridhika maana kila hospital nilipita nikakuta maelezo mapya, kesho yake nikaelekea msasani kuna kio hospital cha meno pale, nilipofika nikamkuta yank mdogo tu nilipomuonesha jino, kwanza akanikaliza akaleta vitabu vya meno akaanza kunipa shule, jinsi jino lilivyo na linavyo athiriwa na kwa kuangalia jino langu nini kinaonekana, akanipiga x ray.. Akaona root yake ilivo

Baada ya hapo akatoa pamba niliowekewa k. Koo, aksema hapa hujafanya kitu, akasafisha jino lile tundu akafungia dawa, akajengea jino la cement akanipa vidonge akaniambia kanywe dose ikiisha uje. Siku iyo iyo akachukua kipimo cha jino.

Baada ya wiki nikarudi, akafumua ile cement nikafanyiwa root canal treatment, akasugua lile jino bila kung'oa mpk likabaki usawa wa fisi, akapachika jino jipya la kudumu la bandia, akanambia anisafishe kinywa, akasafisha jino moja moja.

Tulikaa masaa 6 akinishughulikia, akamaliza akanipa dawa na mouth wash, nikaondoka akanichaji kwa kila kitu tangu siku ya kwanza tsh 140000/= lak na arobaini tu. Nikashangaa. Nikawa mpya kinywani mpk leo

Yule jamaa ndie my best dentist nilieona anachukua muda wake mwingi kwa mteja kuelimisha na kumhudumia, amekuwa kama rafiki saizi na huwa nikija dar hapo ananiomba nipite anicheki meno
Dumelang, Tafadhali na mimi naomba mawasiliano ya huyu DR. wako. Mama yangu anahitaji hasa msaada kwenye hili. Please!
 
Dumelang weka contact za huyo dentist, mzazi wangu meno yanamsumbua nahitaji kumpeleka huko.
 
Ni vema mkaja private kama wengine walivofanya, sijisikii kuweka namba ya mtu hapa hadharani kabla yeye hajataka iwe ivo
 
Back
Top Bottom