Daladala lateketea kwa moto Kimara, Dar

Daladala lateketea kwa moto Kimara, Dar

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
2,819
Reaction score
5,996
Za asubuhi ndugu zangu, inasemekana kuna daladala linawaka moto sasa hivi mitaa ya Kimara baruti, jijini Dar es Salaam. Chanzo cha moto hakijajulikana, ila taarifa kamili itapopatikana tutajulishana kwa kadri iwezekanavyo.

=====

Daladala inayofanya kazi njia ya Temeke Mbezi imeteketea kwa moto eneo la Kimara Baruti leo Septemba 14, 2022 huku chanzo cha moto huo hakikufahamika.

Video: Mwananchi
 
Usijali subiri mpaka fire watoke huko waliko lishaisha na msiwalaumu kwani fire station ni chache sana sana
Ya ni kweli. Haiwezekani jiji kubwa kama Dar liwe na kituo kimoja tu cha zimamoto. Matokeo yake ikitokea ajali kama hiyo inachukua masaa 3 hadi 5 gari za faya kufika katika eneo la tukio. So sad.
 
Ya ni kweli. Haiwezekani jiji kubwa kama Dar liwe na kituo kimoja tu cha zimamoto. Matokeo yake ikitokea ajali kama hiyo inachukua masaa 3 hadi 5 gari za faya kufika katika eneo la tukio. So sad.
Sekta muhimu sana hii sema ndio kipaumbele kiko nyuma tuna matukio mengi sana ya majanga na moto kwa siku moja tu nchini ila ngoja tuone picha litakavyoishia .
 
Za asubuhi ndugu zangu, inasemekana kuna daladala linawaka moto sasa hivi mitaa ya Kimara baruti, jijini Dar es salaam. Chanzo cha moto hakijajulikana, ila taarifa kamili itapopatikana tutajulishana kwa kadri iwezekanavyo.
View attachment 2356370
Serikali itunge sheria kwamba kila basi linalobeba abiria liwe na fire protection system, kwa ajili ya usalama wa abiria, dereva pamoja na gari zenyewe. Hii itasaidia kuepusha ajali mbalimbali zitokanazo na moto.

Watanzania wengi bado hawajawahi na elimu ya kudhibiti moto pale unapoanza kuwaka katika magari au majumba mbali mbali. Wengi hukimbilia kuuzima moto huo kwa njia ya maji na mchanga, kitu ambacho huchochea ongezeko la moto katika sehem husika.
images (6).jpeg
 
Labda tu kama lengo ni kulichoma moto gari Ili uvute jipya Bima, hii michezo ipo
 
Serikali itunge sheria kwamba kila basi linalobeba abiria liwe na fire protection system, kwa ajili ya usalama wa abiria, dereva pamoja na gari zenyewe. Hii itasaidia kuepusha ajali mbalimbali zitokanazo na moto.
Hii unataka kuleta siasa kwasababu ya hiyo gari moja! Fanya takwimu zako unapata case ngapi kwa mwaka kuhusu gari kuwaka moto kama hiyo ya leo? Magari yana kifaa cha kuzimia moto, ila kuna kipindi vinazidiwa na ndio maana unaona hata majengo yenye hizo system huungua pia
 
Serikali itunge sheria kwamba kila basi linalobeba abiria liwe na fire protection system, kwa ajili ya usalama wa abiria, dereva pamoja na gari zenyewe. Hii itasaidia kuepusha ajali mbalimbali zitokanazo na moto.
HAYO YASHATUNGWA na yapo ila kuna mengi nyuma ya pazia trafiki ndio wamejivika majukumu ya fire men nchi hii
 
Back
Top Bottom