Daladala rasmi kurudi upya katikati ya Jiji la Dar-es-salaam mara baada ya mradi wa mwendokasi kushindwa kutoa huduma ipasavyo

Daladala rasmi kurudi upya katikati ya Jiji la Dar-es-salaam mara baada ya mradi wa mwendokasi kushindwa kutoa huduma ipasavyo

😁

Bongo kweli nyoso, walipokuwa wanajenga BRT waliondoa vituo vyote vya daladala...

Sasa wanarudisha daladala na vituo hakuna...
Hakika nchi inasikitisha sana hii.
 
LATRA wametoa mkeka mpya ukionesha kutoa ruhusa kwa mabasi makubwa ya abiria kuanza kufanya safari zake katikati ya jiji kutokea stendi ya Mbezi Louis.

Kwa muda mrefu sasa mradi wa Mabasi yaendayo kasi jijini dar-es-salaam umeonesha kukwama/kushindwa/kuhemewa/kufeli kutoa huduma kwa wakazi wa jijini dar-es-salaam waendao katikati ya jiji kutokea Mbezi-Louis...hali iliyopelekea watu wengi kuchelewa kufika katika shughuli zao za ujenzi wa taifa kutokana n uchache wa mabasi yaliyopo katika mradi wa mwendokasi (UDART).

LATRA imeshatoa ruhusa kwa wamiliki wa mabasi kwenda kuomba leseni ya kubeba abiria kutokea mbezi-louis kuelekea mnazi mmoja ili kusaidia kupunguza adha ya usafiri jijini Dar-es-salaam iliyochangiwa na huduma mbovu za UDART.View attachment 2920148
Hahaha waruhusu tupite mwendokasi
 
Izo tata 20 zitachezea sana vyeti kwa maaskari kwa sababu hakuna vituo maalum vya kushusha na kupakiA

Mradi wa matrafiki huo
 
Mwendokasi akabidhiwe hata mchina wa New Force
 
Sisi tunachoweza ni
Uchawi,
Majungu
Roho mbaya
Ngono
Na ufisadi basi
 
Nashauri hizi daladala zitumie njia na vituo vya mwendokasi; kwa sababu kilichowakwamisha mwendokasi ni kuwa na magari machache yanayofanya kazi.
Sasa kama daldala zitakuwa nyingi kwenye hiyo njia, na kwa spidi ile ile; jiji litakuwa liko vizuri.
 
Wangekuwa serious kwanza kile kituo chao kisingejengwa pale jangwani
 
Swali, Je ni njia ipi itatumika? Hii ya mwendokasi au foleni itahamishiwa kwenye barabara ya "wote"? Maana tunaijua adha ya daladala kusimama kila mahali.
si imeandikwa hapo si usome tangazo?wacha uvivu,wacha kuwa kupe.
 
Inasikitisha mno ,mradi kama huu kufeli , najiuliza tu kwa pesa ambazo wanakusanya kwa siku na kwa mwaka mzima, wanashindeane kuleta basi mpya?
 
Back
Top Bottom