Daladala rasmi kurudi upya katikati ya Jiji la Dar-es-salaam mara baada ya mradi wa mwendokasi kushindwa kutoa huduma ipasavyo

😁

Bongo kweli nyoso, walipokuwa wanajenga BRT waliondoa vituo vyote vya daladala...

Sasa wanarudisha daladala na vituo hakuna...
Hakika nchi inasikitisha sana hii.
 
Hahaha waruhusu tupite mwendokasi
 
Izo tata 20 zitachezea sana vyeti kwa maaskari kwa sababu hakuna vituo maalum vya kushusha na kupakiA

Mradi wa matrafiki huo
 
Mwendokasi akabidhiwe hata mchina wa New Force
 
Wee daladala kulitunza labda utunze injini ila muonekano ishu sana aseee Ukute TATA namba DBK au CZV ipo vizuri kumuonekano huo ni uongo....

Ya nini kuandikia mate na kuweka vigezo visivyo na msingi? Si yakakaguliwe tu?
 
Sisi tunachoweza ni
Uchawi,
Majungu
Roho mbaya
Ngono
Na ufisadi basi
 
Nashauri hizi daladala zitumie njia na vituo vya mwendokasi; kwa sababu kilichowakwamisha mwendokasi ni kuwa na magari machache yanayofanya kazi.
Sasa kama daldala zitakuwa nyingi kwenye hiyo njia, na kwa spidi ile ile; jiji litakuwa liko vizuri.
 
Wangekuwa serious kwanza kile kituo chao kisingejengwa pale jangwani
 
Swali, Je ni njia ipi itatumika? Hii ya mwendokasi au foleni itahamishiwa kwenye barabara ya "wote"? Maana tunaijua adha ya daladala kusimama kila mahali.
si imeandikwa hapo si usome tangazo?wacha uvivu,wacha kuwa kupe.
 
Inasikitisha mno ,mradi kama huu kufeli , najiuliza tu kwa pesa ambazo wanakusanya kwa siku na kwa mwaka mzima, wanashindeane kuleta basi mpya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…