Daladala ziruhusiwe kupita Barabara za Mwendokasi Dar es Salaam



hapa nmekwelewa bro.
 
Mwisho umemalizia na brilliant idea ever.

Pia itatakiwa kuwepo na limit ya idadi ya magari ya watu binafsi yatakayopewa kibali cha kupita baada ya kulipia.

Bila kuwa na limit ya idadi pengine kunaweza tokea foleni tena katika hizo lanes.
foleni itatoka wapi wakati hizo lanes ni njia moja tu, wala huwezi kuover take, labda gari iharibikike katikati ya barabara. Yaani hii ikiruhusiwa itakuwa kila baada ya dk 5 magari 3 ya abiria yanaondoka kituoni na abiria.
 
Barabara yote hii kwa magari mawili tu ya mwendo kasi ni ubadhilifu, no value for money. Duniani kote hakuna vituo vya mabasi wala treni inavyowekwa karibu karibu barabarani kama hapa kwetu.
Mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. Mji hauna nafasi ya kuweka project yoyote ya maana, ni kulazimisha kinachowezekana kifanyike japo kidogo.
 
Kwa madereva hawahawa na konda mhasibu? Hapana aiseeee......
 
Kulipa kwa njia ya mtandao au kulipia benk kunapunguza corruption
 

Nimeona huo utaribu nje ya Tanzania kwenye Nchi tofauti kuna road tolls nyingi kwenye madaraja na kwenye private road kwa wenye haraka na matajiri

Shida ni kwamba serikali ita control vipi ili pesa itakoyoingia kutokana na hilo zoezi hisipigwe na wakatisha ticket

Suggestion :Jambo la msingi watu Watakaopenda kutumia bara bara za mwendo kasi walipie kwa kutumia control number ya serikali then waende ofisi za UDART waoneshe sms ya malipo wapewe cards kama za DSTV na Azam , card ziwe activated kwa kiwango ukichokilipia then from there kuepusha usumbufu siku ukilipia tena kwa Tigo pesa Card iwe activated automatically , halafu road tolls ziwepo chache kwenye hizo bara bara kwa ajili ya maswala ya technicality just in case card ikisumbua

na gharama za kupita iwe hata elfu 50,000 kwa siku ili kufanya bara bara zitumike na wastaarabu tu wasiojua kutanua na ku overtake
 
Usisahau kiwashauri na wabongo kutumia mwendokasi badala ya kung'ang'ana na vigari utadhani wote wahaya
Usafiri wa umma ukiboreka watu wataacha kutumia vigari vyao kwenda kazini. Traffic watatoa kipaumbele kwenye njia za mabasi ya umma kuliko njia za pembeni, hivyo watu wengi watachagua kupanda mabasi badala ya magari yao madogo.
 
Yaani inashangaza na watu wanaunga mkono hoja...watakua wa mikoani hawa...bora mada ingekua waongeze magari

hiko tunachokiunga mkono tumeona kinafanya kazi huko mambele, na serikali inapata faida kubwa sana wanahitaji kutengeneza controls za kubana wapigaji
 
Kweli kabisa, wazo zuri hilo mama. Kwa wenzetu sahivi tolls gate zina camera inakuchapa invoice ikishasoma plate number yako tu.

Huku kwetu tunatakiwa tupewe cards kama za magetini zile za kutokea kama Airport pale au Mlimani city. Ila ziwe debit cards kwamba unaijaza hela kisha ndio unaitumia katika shughuli kama hizo hela inanaenda direct serikalini
 
Yaani inashangaza na watu wanaunga mkono hoja...watakua wa mikoani hawa...bora mada ingekua waongeze magari

Wewe na huyo Jane wote washamba tu,kwani lengo la mradi ni nini,ni kupunguza kero ya foleni kutokana na magari kuwa mengi huku barabara finyu. Sasa kwa akili zako finyu waongeze magari kweli
 
Juma Mpango tanua wigo wa kodi kwa kulifanyiakazi hili wazo.
 
Daladala kwenye majiji hazifai, zinaongeza msongamano na hewa chafu. Majiji yanahitaji magari yenye kubeba abiria wengi kwa wakati mmoja. Miaka ya nyuma 'hiace' ziliondolewa Dar, zimerudi?
Well noted... umetambua haswa
 
Kuna siku mtasema wapishi wa Ikulu wafungue catering services kwakua wanajua kupika kuliko mama lishe...
 
Kuna magari yamezuiliwa kwa kutolipiwa kodi, hayo yakiingia yatajaza hizo barabara
 
Hili liko kwenye ilani ya chama 2020-2035.
Punde si punde utekelezaji wake utaanza kwa majaribio ili wenye haraka waweze kuchangia gharama za miundombinu hiyo ili fedha zitakazo patikana zitumike kutatua kero mbalimbali za wanyonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…